NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MATUMIZI ya pombe na dawa za kulevya kwa wazazi na walezi, imetajwa
kuwa ni chanzo cha watoto wao, kuishi katika mazingira magumu, yanayoweza kuwaingiza
katika majanga.
Hayo
yameelezwa leo Januari 24, 2026 na mtoa mada Rashid Said Nassor, alipokuwa
akiwasilisha mada ya kuwasaidia wazazi na familia, kwenye muendelezo wa mafunzo
ya siku tano, ya ulinzi na hifadhi ya mtoto, yanayofanyika ukumbi wa zamani wa
TASAF, yakifadhiliwa na UNICEF.
Alisema,
matumizi ya pombe na dawa za kulevya, huwapa wakati mgumu wazazi hao, katika
kupanga mipango na mikakati ya malezi ya watoto wao, jambo ambalo linaweza
kuwaingiza kwenye majanga.
Alieleza
kuwa, watoto hao wanaweza kujiongoza wenyewe kwenye malezi na makuzi yao, na
ikiwa jamii iliyowazunguruka ni yenye tabia mbaya, huwa rahisi kwa watoto hao
kudhalilishwa.
Rashid
alifafanua kuwa, khatma ya matumizi ya pombe na dawa za kulevya kwa wazazi na
walezi, ni kuwakosa watoto waliozaliwa ndani ya familia, kimalezi na kimakuzi.
‘’Tuwaombe
wazazi na walezi, waache matumizi ya pombe na dawa za kulevya, kwani hukosa
muda wa kuendeleza malezi sahihi ya watoto wao,’’alifafanua.
Katika
hatua nyingine, alisema ni vyema wazazi wakaunda mitandao ya kijamii yenye tija
kwa maslahi yao ya sasa na baadae, kwani huwa ni dalili ya kuwa na watoto wema.
‘’Familia
ikiwaunganisha watoto na majira wema, wajomba, kaka na ami zao, huwa na uhakika
wa kuishi katika mazingira salama,’’alifafanua.
Aidha
aliwashauri wazazi na walezi hao, kuwashirikisha watoto kwa mambo yanayowahusu,
ikiwemo eneo la kupata elimu kwa maendeleo yake.
Hata hivyo
amewakemea wazazi kuacha kuwafanyia ukatili watoto wao, kwani hujenga ukuta mbovu
wa maelewano, na kuwakosa katika namna ya kujenga familia bora.
‘’Wazazi
ukimfanyia udhalilishaji ama jinai nyingine mtoto wako, huwa ni changamoto endelevu,
na kusababisha kuvunja uhusiano wa milele,’’alifafanua.
Afisa
ustawi wa Jamii kutoka Unguja Fatma Maulid, alisema changamoto nyingine iliyopo
kwa watoto, ni kutolewa na baadhi ya familia zao na kutumikishwa kwa kazi za
ndani.
Alisema,
ijapokuwa bandarini ya Unguja, wapo maafisa wao, ambao wakati mwingine huchukua
hatua, wanapowagundua na kuwasafirisha walikotoka, ikiwa wameingia Zanzibar kwa
lengo la kufuata ajira.
Akiwasilisha
mada ya madhara ya udhalilishaji kwa mtoto, mtoa mada Husna Haji Othman ambae
ni Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Chake chake, alisema kufanya hivyo kunaweza
kumsababishia kukosa kutimiza ndoto zake.
Alieleza
kuwa, athari nyingine, ni kuwepo kwa msongo wa mawazo, jambo ambalo linaweza
kumsababishia hata kifo hapo baadae.
Katika
hatua nyingine, alisema aina nne kuu ambazo zimeanishwa kwenye kanuni ni udhalilishaji
wa kingono utekelezaji, kihisia na udhalilishaji katika ajira.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo hayo, walisema suala la kumuadabisha mtoto huwa sio
kosa kisheria, bali jambo baya ni kumuadhibu kama ilivyo baadhi ya wazazi.
Kassim
Ali Omar, alisema suala la kumuadabisha mtoto, ni jambo la kawaida, ili mtoto
ajue namna ya kuishi na jamii yake.
Mdau
wa haki za watoto, Abduu Salim Mohamed alisema uwepo wa mikataba na sheria aa
kupinga adhabu kwa watoto, ni eneo jipya la kulea watoto bila ya adhabu kama
ilivyokuwa zamani.
Mafunzo
hayo ya siku tano yalioandaliwa na Kamati ya kupamba na udhalishaji ya wilaya
ya Chake chake, yamefadhiliwa na UNICEF na mada kadhaa ikiwemo malezi, makuzi
ya awali ya mtoto pamoja na madhara ya udhalilishaji ziliwasilishwa.
mwisho
Comments
Post a Comment