Skip to main content

WAFANYABIASHARA WANAWAKE MASOKONI WATAKIWA KUTOVUMILIA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

 




NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

WANAWAKE wanaofanya biashara katika masoko ya Mjini Wete na Kifumbikai Wilaya ya Wete Kaskazini Pemba, wameshauriwa kuripoti  vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa viongozi wao wa masoko, ili kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana navyo.

Ushauri huo umetolewa na Msimamizi wa masoko na mazingira Wilaya ya Wete Sadri Mussa Said,  wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Wete Kaskazini Pemba.

Alise katika masoko yote kuna viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kusimamia wafanyabiashara na kuwatatulia changamoto zao mbali mbali za kimazingira na kinidhamu, hivyo ni vizuri kuwatumia ili kupata msaada wa changamoto hizo wanapokua katika shughuli zao za kibiashara.

"Masoko yote kuna viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kusimamia wafanyabiashara na kuwatatulia changamoto zao mbali mbali za kimazingira na kinidhamu, hivyo  tunawashauri wanawake kuwatumia kuripoti matukio ya udhalilishaji yanapotokezea, ili kupata msaada zaidi" alieleza.

Alisema kufanya hivyo kutawawezesha wanawake kufanya kazi zao vizuri, kwa kua na uhakika wa Ulinzi na usalama wao wanpokua katika maeneo ya soko, ambayo ndio matakwa ya serikali na sheria za nchi kwa ujumla.

Alisema uongozi wa soko umekua ukiwashajihisha wafanyabiashara hao kuripoti changamoto zao mbali mbali ikiwemo ya udhalilishaji, lakini bado muitikio ni mdogo jambo linalopelekea kuendelea kwa vitendo hivyo.

Aidha alitoa wito kwa wanawake kua na tahadhari juu ya viashiria vitakavyopeleka udhalilishaji, kwa uepuka michanganyiko   pamoja na majibizano yasio ya lazima ya wao kwa wao na wateja wao.




Kwa upande wake Mfanyabiashara Tahiya Said Abeid wa soko la Mjini Wete alisema,   katika ufanyajikazi wao sokoni hapo wamekua wakikabiliwa na udhalilishaji wa kihisia utokanao na maneno machafu na udhalilishaji wa kimwili, ambao huwakatisha tamaa katika utafutaji.

Alisema changamoto hizo mara nyingi husabishwa  na hali duni za kiuchumi na uhaba wa mitaji , unaopelekea kua wategemezi kwa watu wengine, hali inayotoa fursa ya kudhalilishwa.

Hivyo aliiomba serikali na wadau wengine wa maendeleo kuungamkono harakati za kuwainua wanawake  kiuchumi, ili kuimarisha vipato vyao na kupunguza matendo hayo.

Nae mfanyabiashara Maryam Muhammed Mgeni wa soko la Kifumbikai Wete Pemba alisema, wanawake wengi sokoni hapo hawana muamko wa kuripoti vitendo hivyo kutokana na kushindwa kuelewa pakuanzia na wakati mwengine kuoana vitendo hivyo ni vya kawaida kutokea hasa katika mazingira yao.

Hivyo ameomba mamlaka husika kuendelea kutoa elimu zaidi juu ya viashiria na athari za udhalilishaji na ukatili, namna ya kujikinga na hatua za kuchukua pale vinapotokezea, ili kudumisha usalama wa wanawake katika  shughuli zao za kiuchumi.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Wete Kaskazini Pemba Salma Saleh Hamad alisema, kunauwekano mkubwa wa wanawake kufanya biashara zao masoko bila kudhalilishwa, iwapo wataelewa haki zao na kuweza kujipambania, huku akisisitiza umuhimu wa kuripoti vitendo hivyo vinapotokezea.

                                                         MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...