NA MOZA SHABAN, PEMBA@@@@
SERIKALI
ya awamu ya nane, imekuwa ikigeuza sekta ya elimu kwa vitendo, ikiwemo ujenzi
wa dahalia.
Maana lengo hasa ni kuwapunguzia
umbali wa kutembea masafa marefu wanafunzi, pale wanapokwenda na kurudi skuli.
Dahalia hizo, zimekuwa zikiwasaidia wanafunzi hao,
katika kuongeza ufaulu na maarifa ya kujifunza, masomo yao na kupata utulivu,
wa kujiepusha na vitisho vya udhalilishaji.
Maana alishasema mara kadhaa, Ofisa Mdhamini wa
wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salum kuwa, wamekuwa
wakipokea kesi za vitisho vya ubakaji kwa wanafunzi.
Anasema, wapo wanafunzi hasa kuanzia kidato cha nne,
wamekuwa wakiviziwa vichakani, iwe wanapokwenda ama wanaporudi masomoni.
‘’Mazingira haya ya ujenzi wa dakhalia, ni
kuwahakikishia ulinzi wao, maana mingi yapo karibu mno na skuli,
wanazosoma,’’anasema.
Anakiri kuwa, wahalifu wa ubakaji, walishazoea
kutumia vichaka, ili kuwadhalilisha wanafunzi.
‘’Sasa wanafunzi wetu hasa wakike, wako salama baada
ya serikali ya awamu ya nane, kuja na mpango wa ujenzi wa dakhalia,’’anasema.
Anakumbuka miaka 10 nyuma, suala la kupokea kesi za
wanafunzi wa kike kuviziwa kwa kutaka kudhalilishwa, lilikua jambo la kwaida,
ingawa kwa sasa wako salama.
Kwani anasema, serikali imekuwa ikiipa kipaumbele
sekta ya elimu, kwa kuzimarisha dahalia zilizochaka na kuzijenga upya.
Hussein Ali Mwinyi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Braza la Mapinduzi, alipokuwa akizindua dahalia ya wanawake mkoa wa
kaskazini Pemba, alisema malengo ni kuiimarisha sekta ya elimu.
Na tayari serikali ilitenga shilingi bilioni 864 kwa
mwaka wa fedha 2025/2026, ili kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akaongeza kuwa, wanaowanyemelea wanafunzi iwe wakati
wa kurudi ama kwenda masomoni, sasa watabakia peke yao vichakani, maana kasi ya
ujenzi wa dakhalia inaendelea,
Kumbe sehemu moja wapo ya uumarishaji wa miundombinu
ya elimu, ikiwemo ujenzi wa dahalia ni makakati wa sehemu ya mageuzi ya elimu.
‘’Serikali tayari imetenga kiasi hicho cha fedha,
lengo likiwa ni uimarishwaji wa miundombinu ya elimu ikiwemo huo ujenzi wa dakhalia,’’anafafanua.
Dk. Mwinyi anasema kwa mwaka ujao wa fedha bajeti ya
elimu, anatamani ifikie shilingi trilioni 1, ili kuimarisha sekta hiyo.
‘’Serikali imekuwa ikiimarisha miundombinu ya elimu,
hivyo ni vyema kuyatunza na yaonekane katika uhaliasia wake, ili yaweze
kutumiwa na wingine,’’ anafafanua.
Kwani kuna baadhi ya maeneo, wanafunzi hukosa fursa
za kujisomea, wanapokwa majumbani, kwa sababu mbalimbali, hasa wanafunzi wa
kike.
Kumbe anasema, uwepo wa dahalia hizo zitaongeza
fursa na kuimarisha ufaulu wa wanafunzi hao, na kuwa salama na wadhalilishaji.
Tena akakazia kuwa, serikali itaendelea na utaratibu
wa ujenzi wa dahalia, kila wilaya ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika
kwa kufikia 10,00 ifikapo mwaka 2030.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar Khamis Abdalla Said, anasema dakhalia la wanafunzi hao wa wanawake
skulini hapo, lilikuwa limechakaa na kuhatarisha sualama wa wanafunzi hao.
Changamoto nyingine, ilikuwa ni uchakavu na uhaba wa
vyoo pamoja na hayo, halikuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi wengi.
Akasema kuwa, ingawa kutokana juhudi anazozichukua Dk.
Mwinyi ndio maana akamua kuwajengea wanafunzi hao jengo hilo la kisasa.
Katibu Mkuu huyo akafafanua kuwa, sio dakhalia hiyo
pekee, lakini zipo nyingine katika skuli za Kiwani, Maziwa Ng’ombe, Bubwini
Misufini, Donde, Lumumba, Mikindani, Hasnuu Makame na Paje Mtule.
Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Khamis Abdalla Said, anasema dahalia hiyo, ina vyumba 12, vyoo
31 na ina uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 288 wastani wa wanafunzi 24 kwa kila
chumba.
Inasehemu maalum na ya kisasa ya kufulia, uwanja
pamoja chumba cha muangalizi wa wanawake ‘matron’.
WADAU WA ELIMU
Tatu Abdalla Msellem wa Ole, anasema kumalizika kwa
dakhalia kadhaa mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwemo ya Chwaka Tumbe, ni kuwakinga
wanafunzi na udhalilishaji.
‘’Unajua wanafunzi wa kike, wapo waliokuwa
wakikatisha masomo, kwa hofu ya kuvuuka vichaka na kwenda skuli, ingawa kwa
sasa dakhalia ni mkombozi,’’anasema.
Hija Hamad Ali, anasema dakhalia ni eneo salama kwa
wanafunzi hasa wa kike, kwa kule kupata muda wa kujisomea zaidi.
Asia Hakim Makame kutoka TAMWA Zanzibar, anasema,
dakhali zikisimamiwa vyema, wanafunzi wa kike, watakuwa salama na
udhalilishaji.
Anasema, kuzurura zura ovyo, hasa wanapokwenda
kwenye masomo ya zaida, huwa chanzo cha wao kudhalilishwa.
Anasema, serikali imefanya jambo jema na kubwa,
kawajengea dakhalia za kisasa wanafunzi, wakiwemo wanawake.
WANAFUNZI WA KIKE
Mwanafunzi Asha Hamad wa skuli ya sekondari ya Chwaka
Tumbe, anasema aliamua kuomba uhamisho hapo, ili kupata utulivu.
Mwanafunzi anasoma Utaani kidato cha tatu, anasema
kwa sasa, wanaishi kwenye mazingira salama, hasa kwa wale waliokuwa
wakiwanyemelea kwa ubakaji.
‘’Kwa sasa tuko salama, sio kawaida kuikuta skuli
haina dakhali, hili ni jambo jema, maana wadhalilishaji walikuwa wanatunyemelea
vichakini,’’anasema.
Aisha Hamad Mjaka, anasema ijapokua wanaishi kwenye jengo
ambalo sio dakhalia rasmi, la skuli ya Maziwa Ng’ombe, ingawa utulivu
umepakatikana.
Mkuu wa mkoa wa kuskazini Pemba Mgeni Khatib Yahya,
anasema hayo ni mafanikio makubwa ya mageuzi ya sekta ya elimu, wakati huu wa
uongozi wa Dk. Mwinyi na imeleta faraja kwa wanafunzi.
Maana mwaka 2021 kulikuwa na ufaulu wa asilimia 91.
kutokana na uboreshaji wa sekta ya elimu, na kiwango hicho kimeongezeka na
kufikia asilimia 100 tangu kuingia madarakani.
Mzazi wa mwanafunzi Raudhat Abrahman Ali anasema
hakika ni faraja, kujengwa kwa dakhalia katika skuli mbalimbali.
Anasema hofu yao juu ya watoto wao hasa wa kike, kwa
sasa imepungua, maana wako katika mikono salama saa 24.
Hamida Haji Mzale wa Konde, anasema sasa ni
wanafunzi wenyewe, kuhakikisha wanasoma kwa bidii, na kutimiza ndoto zao.
Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Wete
Salma Saleh Hamad, anashauri kuwa, ili wanafunzi waepukane na ukatili na
udhalilishaji, dakhalia ni eneo salama.
TAKWIMU ZA MAKOSA
Miaka mitatu, Zanzibar iliripoti matukio 4,991
ya udhalilishaji yakiwemo 2,416 yaliohusisha ubakaji, takwimu kutoka Ofisi ya
Mtakwimu wa serikali Zanzibar, imebainisha.
Ikafafanua kuwa, kati ya matukio hayo, wilaya
ya Wete iliripotia matukio 261, ambapo mwaka 2023 yalikuwa 93.
Mwaka uliofauta, yaliripotiwa matukio 77 na
mwaka 2025 yaliripotiwa 91, huku wilaya ya Micheweni kwa kipindi cha miaka
mitatu, ilikusanya matukio 142.
Aidha, wilaya ya Wete kwa mwezi Machi pekee
mwaka huu, kumesharipotiwa matukio 103 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia.
Ambapo waathirika walikuwa 103, watoto wakiwa
84, sawa na asilimia 81.6, wakifuatiwa na wanawake 17, sawa na asilimia 16.5 na
wanaume wawili sawa na asilimia 1.9.
MIONGOZO
Sheria ya Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011, kuanzia kifungu cha 12 (1), kinatamka
wazi kuwa, wazazi na mtu mwingine yeyote anayewajibika kisheria, atakuwa na
wajibu wa kuhakikisha haki za ikiwemo ya ulinzi na majanha mbalimbali kama ya
udhalilushaji, analindwa.
Kifungu cha kidogo cha 12 (2) (a), kinasisitiza kuwa, kila mzazi
au mtu anayewajibika kisheria kwa mtoto, atakuwa na wajibu kuhakikisha maslahi
bora ya mtoto ndiyo jambo lake la msingi wakati wote.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu 12
kinafafanua usawa wa mbele na kile cha 15 cha haki wa faragha na usalama wake.
Sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018
kuanzia kifungu chake cha 108 na 109, kimebainisha pindi mahkama ikimtia
hatiani kwa kosa la ubakaji, adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 ama
cha maisha.
Hutuba ya makadirio ya mapato wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya mwaka 2025/2026 ilisoma na
aliyekuwa waziri Riziki Pembe Juma anasema, wizara inatekeleza mradi
wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji, unaotekelezwa kwa ushirikiano
na shirika la kimataifa la UN- WOMEN.
Kupitia mradi huo wizara imeandaa na kuzindua
mpango kazi wa pili wa kitaifa wa kupambana na vitendo hivyo, wa mwaka
2025/2030 na kuandaa sera ya maendeleo ya jamii.
NINI ATHARI
Mwanajuma Hija Hamad, anasema ni kuwatishia
ndoto zao wanafunzi, pindi wakiishi na majeraha ua kudhalilishwa akilini mwao.
Mwanafunzi Khadija Haji Makame, anasema kwanza
ni kukatisha masomo na kujiongezea mzigo wa maisha hapo baadae.
Daktari Mafunda Mohamed Khamis, anasema hata
kupoteza uhai, wakati mwingine huwa rahisi mtoto au msichana akifanyiwa
udhalilishaji
KIPI KIFANYIKE
Mkuu wa wilaya ya Wete Abdalla Rashid, anasema
ni elimu zaidi kwa wanafunzi, ili kujitoa kwenye vishawishi.
Sheikh Mohamed Issa Haji wa Wete, anasema
jingine ni kuwepo kwa adhabu kali kwa wanaowadhalilisha wanafunzi.
Msaidizi wa sheria wilaya ya Wete Said Rashid
Hassan, anasema elimu ya stadi za maisha, ni vyema ikowepo kila wakati kwa
wanafunzi.
Kaimu Mratibu wa TAMWA-Pemba Amina Ahmed
Mohamed, anasema moja ni waandishi wa habari, kuongeza elimu hasa kupitia
mitandao ya kijamii.
MWISHO.





Comments
Post a Comment