NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
TAASISI zinazoshughulikia masuala ya uongozi wa wanawake vimeviomba vyama vya siasa kuzingatia na kuhakikisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika mikutano ya kampeni zinazoendelea ili kuweza kufuatilia sera zinazotolewa na wagombea wa vyama vya siasa katika nafasi za Urais, Uwakilishi, Ubunge na Udiwani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Taasisi hizo ambazo ni pamoja na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) zimesema kuwa kuna baadhi ya vyama havijazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika mikutano yao jambo ambalo linawanyima haki yao ya msingi ya kufuatilia sera za vyama na hivyo kufanya maamuzi sahihi ya kura zao.

Walisema kuwa kuna baadhi ya vyama vimeshuhudiwa vikiendesha mikutano ya kampeni bila ya kuandaa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu hali inayopelekea kushindwa kushiriki na kufuatilia kampeni.
“Mikutano mingi imekosekana kwa miundombinu wezeshi, wakalimani wa lugha ya alama, maandiko makubwa kwa wenye ulemavu wa macho, na vifaa vya msaada wa kusikia, ambapo huwanyima watu wenye ulemavu fursa ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni," alifafanua.
Alieleza kuwa chama kimoja tu ambacho kimeweka wakalimani katika mikutano yake na ambao huonekana zaidi wakati wa mikutano inayofanywa na mgombea wa Uraisi na hivyo katika nafasi nyengine mazingira hayo bado yanakosekana isipokuwa kwa jimbo moja tu katika mkoa wa mjini magharibi ambapo kumeandaliwa wakalimali maalum kwa ajili ya kundi hilo muhimu.
Alifafanua kuwa ni vyema kuiga chama hicho ili kuhakikisha sera ya ilani ya vyama zinawafikia kwa urahisi, kuweka maandiko makubwa, vifaa vya msaada wa kusikia katika maeneo yote na wakalimani wa lugha za alama ili kujenga demokradia ya kweli.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) jumla ya watu wenye ulemavu wapatao 8,021 wanatarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 visiwani Zanzibar.
Pia Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD, 2006) Kifungu cha 9 kuwa nchi zihakikishe kuwa watu wenye ulemavu wanaishi kwa kujitegemea na kuweka utaratibu wa kufikia huduma zote pamoja na mawasiliano na teknolojia.
Sheria ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar Namba 8 ya mwaka 2022, kifungu cha 29 kinaeleza umuhimu wa watu wenye ulemavu kuweza kufikia miundo mbinu mbali mbali pamoja, taarifa, mawasiliano na haki zote za kibinaadamu na za msingi.
Aidha kutokana na haki walizopewa watu wenye ulemavu za kushiriki kikamilifu katika kampeni za kisiasa, viongozi wa vyama vya siasa wanawajibika kuhakikisha ushiriki huo unatekelezwa bila vikwazo kwa kuweka miundombinu rafiki katika viwanja vya kampeni, kutoa taarifa zinazoweza kufikiwa kwa urahisi, na kuwezesha upatikanaji wa usafiri pamoja na vifaa vya msaada.

Tume ya Uchaguzi na wadau wengine wanapaswa kutoa motisha kwa vyama na wagombea wanaojumuisha watu wenye ulemavu, hatua ambayo itachochea usawa na kudhihirisha mfano bora wa demokrasia jumuishi.
Imetolewa na JUWAUZA, PEGAO, ZAFELA na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania ambao ni watekelezaji wa program ya kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi.
Mwisho
Mwisho
Comments
Post a Comment