1. 01/// Kamishna wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi
ya Zanzibar, Khatib Mwinyichande (wa pili kulia) akizungumza kwenye kikao cha
pamoja baina ya tume hiyo na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC kilichofanyika
ofisi za INEC zilizopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni
utaratibu wa THBUB kukutana na wadau wa Uchaguzi wakiwa kwenye mwendelezo wa
Uangalizi kuelekea Uchaguzi mkuu 2025 wakati wa kampeni kwa vyama mbalimbali
vya siasa. Wa kwanza (kulia) ni Mratibu wa Uchaguzi Unguja (REC) Bw. Abdallah
Bakar Khamis, Katibu Msaidizi THBUB Bw. Juma Msafiri Karibona (katikati), Bw.
Wilfred Msagati Afisa Sheria, THBUB Unguja (wa pili kushoto) na Bitizani Kejo,
Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka THBUB Dar es Salaam.
2. 02/// Kamishna wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi
ya Zanzibar, Khatibu Mwinyichande (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
maofisa wa tume hiyo pamoja na maofisa wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC
mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanywa na tume mbili hizo kwenye ofisi za
INEC zilizopo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni utaratibu wa
THBUB kukutana na wadau wa Uchaguzi wakiwa katika mwendelezo wa Uangalizi
kuelekea Uchaguzi mkuu 2025 wakati huu wa kampeni zinazoendelea kwa vyama vya
mbalimbali vya siasa.
3. Timu ya maofisa wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)
wakiwa kwenye mwendelezo wa kukutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi vikiwemo
vyama vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba 2025. Pichani ni Maofisa wa
THBUB (kushoto) wakiwa kwenye kikao cha pamoja na wanachama wa Chama Cha ACT
Wazalendo (kulia) ofisi za ACT, Vuga Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi,
hivi karibuni.
4. Maofisa kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), (kulia)
wakizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima
Taifa (AAFP), ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, Bw.
Said Soud Said huko ofisi za Chama hicho Mwera, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa
Mjini Magharibi. THBUB inafanya mwendelezo wa kuwatembelea wadau wa uchaguzi
zikiwemo Tume za Uchaguzi za ZEC na INEC, vyama vyote vya siasa wakiwemo
viongozi na wadau wa vyama hivyo, THBUB inafanya zoezi maalumu la uangalizi wa
uchaguzi kuelekea Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, 2025.
KUTOKA PEMBA
5. Maofisa kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), wakiwa
kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo ya Haki za binadamu na misingi ya
utawala bora kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba,
kuelekea Uchaguzi mkuu Oktoba 2025, waliokaa katikati ni Kamishna wa (THBUB)
ofisi ya Zanzibar, Khatib Mwinyichande, Afisa Mfawidhi THBUB kituo cha Pemba
Bw. Suleiman Salim (kulia) na Mratibu kutoka Idara ya Habari Maelezo ofisi ya
Pemba, Bi. Jamila Abdallah Salim (wa Kwanza kushoto). Mafunzo hayo yalifanyika
hivi katika ofisi za THBUB zilizopo Mtaa wa Kichungwani, Wilaya ya Chachake,
Mkoa wa Kusini Pemba.
Comments
Post a Comment