NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MGOMBEA
Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha United Democratic
Party ‘UDP’ Saumu Hussein Rashid, amesema lengo la chama hicho ni kufungua fursa za kiuchumi kwa kila mtanzania,
ili aweze kujitosheleza kupitia biashara zao.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wa
soko la Tibirinzi Chake chake Pemba alipokuwa akitoa sera ya chama hicho na kuomba
kura kwa wafanyabiashara hao.
Alisema kuwa atahakikisha
anakuza kipato cha watanzania, ili
kuifungua kiuchumi kwa kila
mjasiriamali, aweze kujitosheleza katika mahitaji yake.
Alifafafanua kuwa atahakikisha anaweka miundombinu mizuri,
itakayowawezesha wajasiriamali wadogo
wadogo, ili waweze kuwa wafanyabiashara
wakubwa kwa kuongeza pato lao.
‘’Niwambie wajasiriamali nina nia njema na ilani ya chama
change ni kuwanyanyua kiuchumi, ili muwe wafanyabiashara wakubwa, muweze
kujitosheleza katika mahitaji yenu,’’ alifafanua.
Alieleza kuwa chama hicho kimejidhatiti katika suala la
upendo daima, pamoja na kuendeleza kudumisha amani, umoja na utulivu.
Nae mfanyabiashara wa soko hilo kwa niaba ya wenzake Mohamed Juma, wamemuomba mgombea huyo kuwaimarishia
soko hilo, ili liwe katika mjumuiko na muanganiko wa biashara zote, ili wawe
pamoja wajasiriamali hao.
Alisema kuwa kwa sasa soko hilo, limewatenganisha
wafanyabiashara hao kupitia bidhaa zao, na limepoteza haiba yake kibiashara.
‘’Sisi wafanyabiashara tumejitenga kupitia biashara zetu
mbali mbali, tunakuomba utuimarishie
soko letu, liwe la kisasa na lenye muonekano mzuri,’’ alifafanua.
Akati huo huo mgombea huyo wa Urais, alitembelela kaburi
la Dk. Omar Ali Juma na alisema kuwa ni muhimu
kuwaenzi na kufuata misingi bora ya viongozi, wenye kawaletea amani
utulivu na mshikamamo.
Alisema kuwa ni
muhimu kumuenzi na kuthamini mchango mkubwa aliokuwa akitoa ndani ya uongozi
wake, na ametukuka katika madaraka yake.
Mmoja wa familia Zuberi Ali Juma, akitoa historia ya fupi
ya Dk. Omar Ali Juma alisema alikuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kuanzia 1995 hadi mwaka 2001 na amezaliwa mwaka 1941 na kufariki mwaka
2001.
Alisema kuwa alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya
Zanzibar, ambapo katika uhai wake alikuwa ni kiongozi imara na mwenye
kuunganisha watanzania na kuwa mstari wa mbele kwenye kuleta maendeleo.
MWISHO.
Comments
Post a Comment