NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@
ILE dhamira ya Dk. Hussein Ali Mwinyi
kuifungua Pemba kiuchumi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa, sasa imefana.
Kwani
uzinduzi wa ujenzi wa uwanja huo na barabara ya Chake Chake- Mkoani,
umezinduliwa rasmi Septemba25, mwaka huu, katika uwanja wa ndege uliopo Furaha
Pemba.
Ni furaha
kubwa kwa wananchi wa kisiwa cha Pemba, kuona kwamba kitu ambacho wamekisubiri
kwa muda mrefu, sasa kinakwenda kufungua uchumi wao.
Maana serikali ya awamu ya nane, imedhamiria kufanya mageuzi ya
makubwa katika sekta ya usafiri wa anga Zanzibar, kwa lengo la kuimarisha
miundombinu ya utoaji wa huduma katika uwanja wa ndege wa Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amezindua
ujenzi huo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi, jemedari wa uchumi.
Makamu huyo anasema, ujenzi wa miradi hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
ya CCM ya mwaka 2020/2025 ambapo malengo ya serikali, ni kuhakikisha kuwa,
Pemba inakuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa.
‘’Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa, katika sekta ya anga
na dhamira hiyo ilianza kwa vitendo mwaka 2023 kwa kutiliana saini na Serikali
ya Hispania, lengo ni kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi,’’ anafafanua.
Lengo ni kuwa na uwanja wa ndege wa kimataifa, kwa ajili ya kukuza
utalii, uwekezaji na biashara ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa, kukuza
uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.
Hemed anafahamisha kuwa, serikali imejipanga, katika kuhakikisha
barabara zote za Zanzibar zinajengwa kwa kiwango cha lami, na kuwa katika hali
nzuri kwa kuhakikisha zinafanyiwa matengenezo pale inapohitajika.
‘’Miradi hiyo itakapokamilika itapelekea kuimarika kwa huduma za
usafiri wa anga na kuifungua Pemba kiuchumi, kwa kuongezeka shughuli za
kibiashara, kuimarika kwa sekta ya utalii itakayochangia kuongezeka kwa pato la
taifa.
Makamo huyo amemtaka Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huo kampuni ya
PROPAV INFRASTRUCTURES na mshauri elekezi Dar Alhandasah Consultant, kujenga
uwanja huo ka kiwango kinachokubalika kimataifa.
Anakumbusha, maendeleo yoyote yanahitaji kuwepo kwa amani, umoja na
mshikamano, hivyo amewaasa wazanzibari kuendelea kuidumisha amani iliyopo
nchini.
Dk. Khalid Salum Mohamed yeye ni waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi anasema, Dk. Hussein Mwinyi amedhamiria kuifungua Pemba kiuchumi, kwa
kujengwa miradi mikubwa ya maendeleo.
Hapa akatolea mfano kuwa, ujenzi wa uwanja wa ndege Pemba na barabara
ya Mkoani -Chake Chake, yenye urefu wa kilomita 43.5.
Wizara ya Ujenzi inaendelea na ukarabati wa bandari ya Mkoani, ambayo
itakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa, kutoka nje, jambo litachochea ukuwaji wa uchumi kisiwani Pemba.
Akisoma taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiano
na Uchukuzi Dk. Habiba Hassan Omar anasema,
Serikali imekuwa ikichukua juhudi kubwa, kuimarisha huduma za usafiri
wa anga na nchi kavu.
Akitaja kuwa lengo ni lile lile la kukuza uchumi wa nchi na kuwandolea
usumbufu wananchi na wageni wanaofika Zanzibar.
Dk. Habiba anasema, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege
wa Pemba. umeanza rasmi Novemba 2024 na unatarajiwa kuchukua muda wa miezi 36, mpaka
kumalizika kwake.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Saada Mkuya anaeleza katika miradi
ya kimkakati aliyodhamiria Dk. Mwinyi ni uwanja wa ndege wa kimataifa kisiwani
Pemba.
‘’Fursa hizi ndizo zinzoongeza uchumi wa nchi na watu binafsi, hivyo
ni faraja kwetu, kuona maeneleo yanazidi kupanuka kisiwani Pemba,’’ anaeleza.
Mkandarasi wa ujenzi wa Uwanja huo ni Kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES
kutoka nchini Hispania na Msimamizi wa ujenzi ni Kampuni ya DAR AL HANDASAH
CONSULTANTS kutoka Lebanon, ambapo ujenzi huo unatarajiwa kugharimu jumla ya
EURO milioni 170.
Ujenzi wa Uwanja huo utahusisha jengo jipya la abiria, lenye uwezo wa
kuhudumia abiria wasiopungua 300,000 kwa mwaka, ikiwemo abiria wa ndani
(Domestic) na abiria wa kimataifa (International) pamoja na ujenzi wa njia ya
kuruka na kutua ndege (Runway), yenye urefu wa mita 2.510 na upana wa mita 45
utakaokuwa na uwezo wa kutua ndege zote za aina ya Code 4C.
Kwa upande wa utekelezaji wa mradi wa barabara ya Mkoani – Chake
Chake yenye urefu wa kilomita 43.5, inayojengwa na Kampuni ya PROPAV
INFRASTRUCTURES ya Hispania, ikisimamiwa na kampuni ya DAR AL HANDASAH
CONSULTANTS, ambayo inatarajiwa kuchukua muda wa miezi 36, hadi kumalizika
kwake.
Ujenzi wa barabara ya Mkoani- Chake Chake utagharimu zaidi ya EURO
milioni 93, itakayohusisha njia za watembea kwa miguu, taa za barabarani,
(streetlights) pamoja na alama za usalama wa barabarani.
Aambapo itakapokamilika itawarahisishia wananchi kuzifikia huduma
mbali mbali za kijamii na kiuchumi kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya PROPAV INFRASTRUCTURES Cristiano Becker anasema,
wanatambua kuwa, uwanja wa ndege ni mlango mkuu na daraja la kuiuganisha Pemba
na dunia.
Hivyo ameahidi kuwa wataujenga uwanja huo kwa viwango na ubora
unaokubalika kimataifa, ili mfano kwa maeneo mingine.
Mkurugenzi huyo anasema, serikali imeiamini kampuni ya PROPAV
INFRASTRUCTURES na kuipa mkataba wa kuujenga uwanja huo, hivyo itajenga uwanja
wa ndege wenye hadhi na sifa zote.
Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Mkoani- Chake Chake Christiano
anafafanua kuwa, ahadi yake ni kujenga barabara hiyo kwa uaminifu mkubwa, na
yenye viwango vinavyoendana na mustakbali wa Pemba.
Anaeleza, ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege wa Pemba, pamoja na
barabara ya Mkoani- Chake Chake utatoa ajira zaidi ya 1,000 kwa wakaazi wa
Pemba, wananchi kutoa fursa ya kufanya biashara ndogo ndogo, pamoja na mafunzo ya
ujuzi kwa vijana watakaopata fursa ya kufanya kazi na kampuni yake.
Kwa upande wao wananchi walifurahi sana kuona uzinduzi huo na kusema,
sasa unaenda kuifungua Pemba kiuchumi kwa vitendo.
Wanasema, Dk. Mwinyi amekuwa akifanya juhudi mbali mbali kuhakikisha
wananchi wa Pemba wanaimarika kiuchumi na ndio maana amekuwa akiwaletea mambo
mengi ya kimaendeleo, hivyo anahitaji pongezi.
Asha Hassan Juma, mwenye uleavu wa Wawi, anasema furaha zao ni kuona
miundombinu kwa ajili yao imezingatiwa katika ujenzi huo.
Ali Haji Kombo wa Madungu, ansema sasa anaionba Pemba iko karibu kukuza
pato na uchumi wake, maama milango ya bandari, barabara na uwaja wa ndege
umeshapanuliwa kimataifa.
MWISHO.
Comments
Post a Comment