NA KHAULAT SULEIMAN, SUZA@@@@ WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mudrik Ramadhani Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhamiria kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi, hasa katika sekta ya Utalii, ili kutangaza fursa zilizopo kisiwani humo. Alieleza hayo katika hafla ya ufunguzi wa Tamasha la mswahili wa Kipemba lililo fanyika jana Augost 24, 2024 katika uwanja wa kisiwa cha Kojani Wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema serikali imeandaa mikakati ya kuwaboreshea wananchi huduma za kijami kwa lengo la kuendelea kutangaza mila na silka, Utamaduni katika kisiwa cha Pemba. Aidha amesema katika kukifungua kisiwa cha Pemba, Kojani tayari ipo katika uboreshwaji wa kutengezewa darasa la kujifunza kwa vitendo ili Kojani kua kitovu cha Utalii zaidi. "Zaidi ya asilimia 30 zinategemea sekta ya Utaliii, lazima kuweka matamasha, ili kuendelea kuitangaza Zanzibar katika sekta ya Utalii na kuvutia wageni mbali mbali,''alisesema waziri huyo. ...