NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MWALIMU Mkuu
wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent, iliyopo Mgogoni wilaya ya Chake
chake Pemba, Mwache Juma Abdalla, amewataka wanafunzi wa darasa la kumi na
mbaili skulini hapo, kuzitumia kwa maandalizi ya hali ya juu, wiki 11 zilizobaki,
kabla ya kufanya mtihani wao wa taifa.
Alisema,
wiki hizo sio kidogo, kwa mwanafunzi kama ataweka pembeni uvivu, kudorora,
kushughulikia anasa na kujikita kwenye masomo, hivyo anaweza kufanya vizuri,
kwenye mtihani wa taifa.
Mwalimu mkuu
huyo, aliyasema hayo leo Augost 24, 2024 skulini hapo, kwenye kikao cha wazazi na wanafunzi
hao, cha kutoa matokeo ya mitihani ya majaribio ya kimkoa ‘MOCK’ yaliofanyika
hivi karibuni.
Alisema, bado
wanafunzi wanayonafasi ya kujiandaa na mitihani hayo, kwani waalimu wameshamaliza
mtaala waliopangiwa, na sasa ni kazi wanafunzi wenyewe.
Alieleza kuwa,
waalimu wamekuwa wakitumia jitihada binafsi ili kuhakikisha wanamaliza mitaala
mapema, na sasa ni kazi ya wanafunzi kuangalia mitihani iliyopita.
‘’Tumebakiwa
na wiki 11 kabla ya kukutana na mitihani ya taifa, sasa wanafunzi muongeze bidii,
waalimu wapo kwa ajili yenu na wengine hata majumbani hawarudi kwa wakati,’’alieleza.
Akizungumzia
kuhusu mitahani hayo ya majaribio, alisema skuli hiyo imekuwa na dara la tatu (c),
ingawa matokeo hawakuridhika nayo kwa kiasi fulani.
‘’Matokeo ya
‘MOCK’ yameshatoka, lakini kiujumla sisi waalimu yametuhuzinisha, maana jitahada
za waalimu ni kubwa, ingawa wanafunzi wanaoneka kuwa wavivu,’’alifafanua.
Hata hivyo Mwalimu
huyo mkuu, alisema matokeo hayo sio mabaya sana, maana hakuna mwanafunzi aliyepata
kiwango cha alama sifuri wala daraja la nne.
Mapema Mwenyekiti
wa bodi ya wazazi ya skulini hapo Dk. Said Mohamed, alisema bado wazazi wanayonafasi
ya kukaa na watoto wao, na kujua ni chanzo cha mtoto wake kufeli.
‘’Mzazi
anayonafasi kubwa mno, kuhakikisha mtoto wake anaongeza juhudi na kisha anakuwa
na matokeo mazuri kwenye mitihani ya taifa,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine Mwenyekiti huyo, alipongeza juhudi za waalimu skulini hapo, ambazo
zimesaidia skuli hiyo kuendelea kujiwekea historia, ya kutokuwa na daraja la
nne.
Mwalimu
Khamis Mohamed, alisema kasoro anayoiona kwa wanafunzi hao, ni kutoelewa wajibu
wao, hasa kwa yale madarasa yenye mitihani.
‘’Wanafunzi
sio wabaya kiakili, ila changamoto iliyopo wapo wasiofahamu wajibu wao, na hili
linahitaji nguvu pia za wazazi na walezi, maana mwalimi pekee, mwanafunzi hatofanikiwa,’’alishauri.
Mzazi Khamis
Ali Juma, aliwashauri waalimu skulini hapo, kuweka mkazo wa ufahamu ya lugha ya
kiengereza, kwani ndio msingi wa masomo kadhaa.
Asha Saleh
Juma, alielezea kusikitishwa kwake na ufaulu mdogo wa somo la hesabati, na
kuwataka wanafunzi kuacha woga, kwani somo hilo ni rahisi.
Mzazi
Mohamed Juma, aliwataka wanafunzi kuongeza bidii, kwani kila kitu kinawezekana
kufanikiwa, ikiwa mfanyaji atajielewa.
Wanafunzi 81
waliofanya mitihani ya majaribio ya ‘MOCK’ skulini hapo, waliopata daraja la
kwanza ni wanane, daraja la pili 22, daraja la tatu 36, daraja la nne 15 na
hakukua na mwanafunzi aliyepata daraja la mwisho.
Kati ya masomo
11, ambayo wanafunzi hao 81, waliyapasi kwa wingi ni masomo ya kiswahili walipasi
wote 81, somo la uraia wanafunzi 79, dini ya kiislamu 79, Jiongrafia 78,
english 72, chemia 65.
Kwa mitihani
kama hayo ya mwaka 2023, wanafunzi wote walikuwa 53, ambapo hakukua na
aliyefeli, na hakukua na mwanafunzi aliyepata daraja la nne.
Ambapo kwa
mitihani ya taifa, kati ya wanafunzi hao, sita walipata daraja la kwanza, ambao
ndio walioungana na wenzao juzi kula chakula cha pamoja na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Mwisho
Comments
Post a Comment