NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
UONGOZI wa Umoja wa
wanawake wa CCM ‘UWT’ mkoa wa kusini Pemba, umesema ziara iliyofanywa hivi
karibuni na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo taifa Zainab Khamis Shomari, imekuwa
ni darsa tosha, kuelekea ushindi wa CCM hapo mwakani.
Hayo yameelezwa na
Mwenyekiti wa umoja huo mkoani humo, Zuwena Khamis Abdalla, alipokuwa
akizungumza hivi karibuni, kufuatia kumalizika kwa ziara ya Makamu Mwenyekiti huyo,
mkoani mwake.
Alisema ujio wake,
umewaamsha na kuendeleza mbele umoja huo na chama kwa ujumla, kwani ametoa maagizo
ambayo kama yakifanyiwa kazi, CCM itaendelea kuweka historia ya ushindi katika
kila uchaguzi.
Alieleza kuwa, moja
ambalo wanalikumbuka ni kuwataka viongozi wa UWT mkoa, wilaya na hadi shina
kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama wa CCM.
Alifahamisha kuwa, hilo
ni jambo la msingi ndani ya UWT, na hivyo ni lazima viongozo wote hadi ngazi ya
mkoa, kulitekeleza kwa vitendo agizo la Makamu Mwenyekiti huyo.
‘’Ni kweli ziara ya Mheshimiwa
Zainab, imetuachia darsa na ukumbusho kwetu sisi viongozi wa ‘UWT’ na hata wanachama
wa kawaida, na moja hili la kuongeza idadi na wanachama wapya,’’alisema.
Aidha Mwenyekiti huyo
wa ‘UWT’ Mkoa wa kusini Pemba, alisema agizo jingine ni kuhakikisha, wanaUWT na
wanaCCM kwa ujumla, wanaendelea kuwa waalimu wa kuvielimisha vyama vingine, juu
ya maendeleo yaliopo.
‘’Alituambia, sisi UWT
na jumuia nyingine ndani ya chama, tusiwe tunapiga kelele ovyo, na badala yake
tuwaonesha wale wingine maendeleo yaliofanywa na Dk. Mwinyi na Mama Samia,’’alisisitiza.
Katika hatua nyingine
Mwenyekiti huyo wa UWT mkoa wa kusini Pemba, Zuwena Khamis Abdalla, alisema
watalifanyia kazi, agizo alilolitoa kuwataka ambao hawajajikusanya kwenye vikundi
vya ushirika, kufanya hivyo.
‘’Alisema hadharani
kuwa, sasa ule mkwamo kwa baadhi ya vyama ya ushirika hasa eneo la mashrti katika
upatikanaji mikopo, wameshazungumza na serikali, hivyo ni jukumu la wananchi
kujikusanya na kujisajili, ili kuiomba mikopo hiyo,’’alisema.
Nae Katibu wa UWT
mkoani humo Asila Ali Salim, alisema ziara hiyo sio tu kupokea maagizo hayo na
kuyafanyia kazi, bali imesaidia uhai wa ‘UWT’ na chama kwa ujumla.
‘Unajua tunapokuwa na
viongozi wanaotutembelea kwenye maeneo yetu ya kazi kama hivi, kuanzia sisi
viongozi na wanachama, huhamasika zaidi kutekeleza majukumu yetu, kwa hili
tunampongeza Makamu Mwenyekiti,’’alieleza.
Aidha alieleza kuwa,
jambo jingine ambalo limewapa moyo, ni pale alipozungumza na wajasiriamali,
katika ukumbi wa Manispaa ya jiji la Chake chake, na kuwapa moyo zaidi.
‘’Unajua Mwakamu
Mwenyekiti wetu wa UWT, ziara yake ilikuwa ya kisayansi zaidi, maana pamoja na
kuzungumza na wanaUWT, lakini alitembelea pia soko la Machomane na kuacha
maagizo,’’alifafanua.
Akiwa katika mkoa wa
kusini Pemba, Makamu huyo Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM Tanzania ‘UWT’
Zainab Khamis Shomar, alipata nafasi pia ya kukabidhi piki piki mbili, kwa
ajili ya ofisi za UWT za wilaya ya Chake chake na Mkoani.
Wakati huo huo Makamu
Mwenyekiti huyo, alivieleza vyama vyingine vya siasa kuwa, daima CCM, itaendelea
kuhubiri amani na utulivu, maana ndio mwalimu wa vyama vingine nchini.
Alisema, CCM baada ya kuwahudumia wananchi
wote wa Tanzania bila ya ubagauzi, msingi wake mwingine mkuu ni kuhubiri umoja,
mshikamano, amani na utulivu kwa nia ya kuwaunganisha watu wote.
Aidha aliwataka
viongozi wa UWT, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa kuendelea kuhubiri jambo
hilo, kwani ndio msingi mkuu kwa chama hicho, tokea kuasisi kwake.
‘’Sisi UWT na jumuia
nyingine za chama, tumekuwa tukihimiza kila siku, kuwa ajenda yetu ya kwanza
iwe ni kuhubiri amani na utulivu, kisha kuleta maendeleo kwa kila
mtu,’’alifafanua.
Aidha Makamu Mwenyekiti
huyo wa UWT taifa Zainab Khamis Shomar, aliwapongeza rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na Dk. Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar, kwa
kuchapuza miradi ya maendeleo.
Alieleza kuwa, tayari
Dk. Mwinyi kwa upande wa Zanzibar ameshavuuka lengo la utekelezaji wa Ilani ya
CCM ya mwaka 2020/2025, katika miradi kadhaa, aliyowaahidi wananchi wakati
akiomba ridhaa.
‘’Kwa mfano, aliahidi
ujenzi wa vyumba 1,500 vya madarasa, wakati wa kampeni ingawa ndani ya miaka
yake mitatu ya utawala ameshajenga vyumba 2,273 hapa ameshavuuka lengo kwa
asilimia 150,’’alifafanua.
Mwisho
Comments
Post a Comment