NA KHAULAT SULEIMAN, SUZA@@@@
WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mudrik Ramadhani Soraga amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhamiria kukifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi, hasa katika sekta ya Utalii, ili kutangaza fursa zilizopo kisiwani humo.
Alieleza hayo katika hafla ya ufunguzi wa Tamasha la mswahili wa Kipemba lililo fanyika jana Augost 24, 2024 katika uwanja wa kisiwa cha Kojani Wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema serikali imeandaa mikakati ya kuwaboreshea wananchi huduma za kijami kwa lengo la kuendelea kutangaza mila na silka, Utamaduni katika kisiwa cha Pemba.
Aidha amesema katika kukifungua kisiwa cha Pemba, Kojani tayari ipo katika uboreshwaji wa kutengezewa darasa la kujifunza kwa vitendo ili Kojani kua kitovu cha Utalii zaidi.
"Zaidi ya asilimia 30 zinategemea sekta ya Utaliii, lazima kuweka matamasha, ili kuendelea kuitangaza Zanzibar katika sekta ya Utalii na kuvutia wageni mbali mbali,''alisesema waziri huyo.
Alifahamisha kuwa, serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Utaliii itaendelea kuweka matamasha katika sehemu mbali mbali kisiwani Pemba, ili kutunza rasilimali zilizopo kisiwani hapa.
kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, alisema katika kuunga mkono juhudi za Serikali na Rais wa Zanzibar katika kuzitekeleza ahadi alizoziweka ya kuifungua Pemba kiuchumi, Wizara ya Utalii imejidhatiti kuongeza Utaliii kwa kasi zaidi kisiwani humo.
Amempongeza waziri na Wizara yake, kwa juhudi wanazozichukuwa kuhakikisha kisiwa cha Pemba kinafunguka kiutalii.
Mapema Mbunge wa jimbo la Kojani Hamadi Hassan Chande ambaye pia ni naibu waziri wa Fedha Tanzania Bara, aliwataka wananchi wa jimbo la Kojani, kuendelea kuzilinda mila, silka na tamaduni zao, ili uwe upekee na kulinda madili.
"Watu wa Kojani mueendelee kuwa wakirimu wa wageni na kulinda asili, ili kuvutia wageni mbali mbali ambao wanafika kisiwani hapa,''alieleza.
Naye mkuu wa Wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakar ameiyomba jamii kuendelea kuilinda na kuhifadhi mila na silka za wazanzibar kwani ni kutofanya hivyo kutapoteza Utamaduni wao
" Kwa sasa Utamaduni haupo na ile asili hasa ya kipemba ama Mzanzibar kutokana na kufuata mila za kigeni, ambazo zinauwa kizazi chetu hivyo kila mmoja ana jukumu la kulinda mila zenu,''alieleza
Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Zuhura Mgeni Othman, alieleza kua Wizara inahakikisha kuendeleza matamasha mbali mbali, ili kuikumbusha jamii pamoja na kukitangaza kisiwa cha Pemba kwa lengo la kukuza Utalii Zanzibar
Comments
Post a Comment