NA HASINA KHAMIS, PEMBA @@@@
MKUU wa wilaya ya Chake Chake Pemba, Rashid
Abdalla Ali, alisema uwepo wa Azam Tv, utawezesha kuibua vipaji viliopo
kisiwani Pemba kwa vijana.
Alisema hayo wakati akifungua duka la wakala
wa Azam Tv huko, eneo la Sukita mjini Chake chake, kisiwani Pemba.
Alisema tegemeo kwa vijana wa Pemba, juu ya uwepo
wa ofisi kuu ya Azam Tv, ni kuimarisha kutangaza na kuvumbua vipaji vya wasanii,
mbali mbali ikiwemo kuonesha tamthilia zao.
Aidha mkuu wa wilaya alisema "wananchi
hawatakuwa na haja ya kusafirisha visimbuzi vyao nje ya kisiwa cha Pemba, kwa
matengenezo badala yake kutumia vyema ofisi hiyo iliyofuguliwa kwa ajili yao,"alisema.
Nae Meneja wa mauzo na usafirishaji wa bidhaa,
Adam Ndimbo, aliwahakikishia wananchi kuwa huduma zitatolewa kwa sawa nchi nzima,
pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.
Alisema changamoto zote za visimbuzi
zimetatuliwa na kuwataka kuwa na imani na wakala wa hao kwa huduma bora na
matengenezo bure.
"Wakala wa Tripl M, tumewaamini na
wanaweza hivyo ninawaomba wananchi kuwa na imani nao kwa kuboresha huduma na
upatikanaji wa bidhaa za Azam Tv Pemba,"alisisitiza.
Nae wakala mkuu wa Tripl M, Suleiman Seif Ali,
aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kununua na kutengeneza bidhaa zao bure
katika ofisi yao.
Akisoma risala ya wakala hao, aliwataka
wananchi "kutoa ushirikiano kutoka kwa Serikali, taasisi na wadau mbali
mbali na kuahidi huduma zitatolewa bila ya usumbufu wowote,"alifafanua.
Nae Mtendaji mkuu wa Azam Tv Sabrina Mohamed
Ali, alisema huo ndio mgodi wa kwanza kwa Zanzibar na 15 kwa Tanzania, ambapo
huduma zote zitapatikana Pemba.
MWISHO
|
|
Comments
Post a Comment