Skip to main content

Posts

AFANDI KHALFAN ATIMIZA AHADI KWA WAVUVI

      NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WAVUVI wa bandari ya Tanda Tumbi Shehia ya Mjanaza Wilaya ya Micheweni Pemba, wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya Hali ya Hewa, ili kuweza kujikinga na matatizo yanayoweza kutokea wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi.   Hayo yalielezwa na Mkaguzi wa Polisi ambae pia ni Polisi shehia ya shehia ya Mjanaza Khalfan Ali Ussi, wakati akikabidhi simu kwa wavuvi hao, ikiwa ni ahadi iliyoitoa kwao hivi karibuni.   Alisema, kwa vile wao ni wavuvu anamatumaini makubwa kuwa,   simu hizo lengo lake ni kuwasaidia katika shughuli zao hizo, pindi wanapopatwa na majanga mbali mbali.   Alifahamisha kuwa, lengo la kutoa simu hizo ni kutokana na maafa mbali mbali, ambayo yanawapata wavuvi wakiwa katika shughuli zao, na kukosa chombo cha mawasiliano.   "Leo (jana), nimekuja kwa ajili ya kutimiza ahadi yangu, niliyoiweka kwenu kuwapatia simu ambayo itaweza kuwasaidia, pindi mnapotokezea ka...

BARAZA LA WATOTO WAWI, LAKERWA ADHABU NYEPESI KWA WABAKAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ BARAZA la watoto la shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, limesema bado hawaridhishwi na hukumu nyepesi zinatolewa mahakamani, kwa washtakiwa wanaowabaka watoto na wanawake. Walisema, bado hukumu zinazotolewa na mahakma maalum za kupambana na udhalilishaji, zinawafaidisha wabakaji, jambo ambalo, linatishia kuendelea kwa matendo hayo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema, Baraza la Wawakilishi mwaka 2018, lilipitisha sheria kali kwa watakaotiwa hatiani kwa udhalilishaji, ingawa bado mahakimu hawaitumii ipasavyo. Walisema, wamesomeshwa kuwa, mahkama ikimtia hatiani mshitakiwa kwa makosa ya ukatili na udhalilishaji, adhabu yake ni kuanzia kifungo kisichopungua miaka 30 au maisha, ingawa hakuna aliyetekelezewa adhabu hiyo. Mjumbe wa baraza hilo Aisha Mohamed Juma, aliema anashangaa kuona washtakiwa wanafungwa miaka kati ya 10 au 15 tu, jambo ambalo anashindwa kuwaelewa mahakimu. Alieleza kuwa, hajaona wapi mahak...

WATOTO WA KIKE BADO SANA USHIRIKI KWENYE SOKA

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@   BADO kuna ushiriki mdogo kwenye michezo kwa watoto wa kike, Kisiwani Pemba na sababu moja inayopelekea watoto wa kike kuwa nyuma katika sekta hiyo na hasa mpira wa miguu.   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Julai, 9, 2024, kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema bado wanawake ushiriki wao ni mdogo, katika michezo ya aina mbali mbali, hasa soka   ambapo jitihada zinahitajika kuhakikisha nao wanashiriki.   Muhisin Omar Haji, Wawi Chake chake, alisema watoto wa kike huishia maskulini kushiriki michezo na wanapomaliza hawajiendelezi na wala hakuna mtu wala taasisi ya kuviendeleza vipaji hivyo.   Alisema wapo watoto wa kike wanakuwa wazuri kimichezo, kama mpira wa miguu, kikapu, mpira wa Pete na mengine, lakini cha kuumiza ni kuwa baada ya kumaliza skuli hawajiendelezi.   Asha Said Haji miaka 17, na Mwanaisha Haju Soud miaka 16 wote wakaazi wa Machomane, walisema kutokana na changamot...

FIDEL CASTRO, WANANCHI WAPIGA MARUFUKU UZURURAJI HOLELA ENEO LA SKULI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro, wananchi kijijini hapo, pamoja na uongozi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, umekubaliana kupiga marufuku kuanzia sasa, kutoingia kwa mtu yeyote bila ya kazi ya halali, ndani ya eneo la skuli, ili kuepusha athari ambazo zimeanza kujitokeza. Wakizungumza kwenye kikao cha pamoja, kilichofanyika skulini hapo, walisema tayari athari kama za wizi wa vifaa vya wanafunzi, umeanza kujitokeza, hivyo wamekubaliana kuanzia sasa kupiga marufuku, uingiaji kiholela. Mwalimu mkuu wa skuli hiyo Seif Hamad, alisema ameridhishwa na uamuzi uliofikiwa na pande mbili hizo, kwani wamekuwa na hofu kubwa ya kutokezea vitendo vya udhalilishaji hapo baadae. Alieleza kuwa, uamuzi huo unaweza kusaidia sana kuondosha uingiaji holela ndani ya skuli hiyo, ambao kwa kiasi kikubwa, ulikuwa unaanza kutishia hata mali za skuli. ‘’Mimi nimeridhishwa na uamuzi ambao umefikiwa kati yetu, wazazi na uongozi wa shehia, kwamba sasa t...

DK. MWINYI AKIFUNGUA KISIWA CHA PEMBA KIUCHUMI, KIWANDA CHA MAJI CHA KWANZA HICHI HAPA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@   “Waswahili wanasema… ‘Pemba Peremba, ukienda na joho utarudi na kilemba’,.   Wengine wakasema kuwa, “waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba”. Haya ni baadhi ya misemo na misimu, ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba hupenda kuyatumia, kulingana na wakati na kwenye kitu kinachohimiza maendeleo. Karne zimepita, tangu misemo hiyo kutumika, licha ya kuendelea kutumiwa vijijini, kulingana na mazingira au kitu kilichopo. Katika miaka iliyopita, kulikuwa na baadhi ya watu waliweza kudiriki kusema kuwa, hakuna uwezekano wa Pemba, kuwa ya viwanda, licha ya maeneo huru ya uwekezaji kutengwa kwa miaka zaidi ya 20. Sasa ni miaka minne ya uongozi wa Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi, wananchi wa kisiwa cha Pemba wameanza kujivunia maajabu ya kimaendeleo. Tayari miradi ya kimkakati imeanza kuonekana ndani ya Kisiwa cha Pemba, kwa mabadiliko makubwa ya maendeleo, ndani ya kisiwa hicho. Ilikua ni Julai 27 mwaka 2022, jua tayari linaelelekea kuzama, Rais D...

'WEPO' YAZINDUA MRADI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILLISHAJI

  SALIM HAMAD, PEMBA@@@@ HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zuwena Mohamed Abdul-kadir amewataka wadau wa mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji, kuongeza kasi katika mapambano hayo, ili kuwakinga watoto wasiharibiwe, ambao ndio kundi kubwa linalokabiliwa na shida hizo. Kauli hiyo ya Hakim wa Mkoa, imetolewa kwaniaba yake na Hakimu wa Mahkama ya Mwanzo Wete Adam Abdalla Faki wakati akizungumza na Wadau wa Mambano ya Udhalilishaji, katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa uwezeshaji wa Kisheria na upatikanaji wa haki unaofadhiliwa na UNDP uliofanyika Baraza la Mji Wete. Alisema  katika kumaliza shidha hizo, wadau kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kusimama imara na kutoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo visiendelee. ‘’Bado vitendo hivi vinaendelea kujitokeza pamoja na juhudi zote zinazochukulia lakini tunatakiwa kuwa wamoja na mashiriano kupiga vita vitendo hivyo,’’alisema . Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka Jumuia ya wasaidizi wa sheria Wete...

'CONNECTING CONTINENT' YAWAONESHA NJIA WAZAZI KUONGEZA UFAULU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent iliyopo Mgogoni wilaya ya Chake chake, umesema kama wazazi na walezi wataongeza ushirikiano, kati yao na waalimu, uwezekano wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa kidato cha nne upo. Mwalimu mkuu skulini hapo, Mwache Juma Abdalla, alisema waalimu wanaosomesha skuli hiyo, wamekuwa na moyo mmoja wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne, hasa kwa mitihani ya taifa. Alisema, hilo linaweza kuwa rahisi mno, ikiwa kuanzia sasa   wazazi na walezi, watajenga msingi madhubuti ya ushirikiano kati yao na waalimu, skulini hapo. Alieleza kuwa, wapo wazazi na walezi, hawapiti skulini hapo jambo ambalo linalowapa ukakasi waalimu na kuhisi wameachiwa majukumu peke yao ya ulezi. Mwalimu mkuu huyo, aliyasema hayo Julai 6, 20204 kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka huu, cha kuwasilisha matokeo ya muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Alifahamis...