Skip to main content

Posts

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

UWANDANI CHAKE CHAKE WAKUMBUSHWA KUTOZITIA MKONO KESI ZA JINAI

    NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kujitenga mbali na sulhu za kesi za jiani, ikiwemo za udhalilishaji, kwani kufanya hivyo, ni kuyapalilia matukio hayo. Hayo yameelezwa leo Juni 25, 2024 na Mkuu wa Divisheni ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar ofisi ya Pemba, Bakar Ali Omar, kwenye hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi Haji Nassor, kwenye mkutano wa wazi, kwa wananchi waliomo ndani ya mpango wa kanusuru kaya maskini, ikiwa ni sehemu ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar. Alisema, bado wapo baadhi ya wazazi, wamekuwa wakizikalia mkekani kesi hizo, kwa kuzifanyia sulhu, jambo ambalo kisheria ni kosa na kuongeza kichocheo kwa watendaji. ‘’Niwasihi sana wananchi wa Uwandani, tukiwa ndani ya wiki ya msaada wa kisheria, jambo hilo mliepuke na ikitokezea mkimbile mbele ya vyombo vya sheria,’’alieleza. Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi hao, kuwatumia wasai...

UHALIFU MFIKIWA CHAKE CHAKE BADO KITENDAWILI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Mfikiwa wilaya ya Chake chake, wamesema kupooza kwa ulinzi shirikishi katika shehia yao, kumesababisha kurudi upya vitendo vya kihalifu, ikiwemo wizi wa mifugo. Walisema, kwa sasa wapo wafugaji wanaolazimika kulala na mifugo yao majumbani kama vile Ng’ombe kutokana na kuhofia wizi ulioshamiri shehiani hapo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, Juni 22, 2024  walisema, kwa sasa hali ya vitendo vya kihalifu imeibuka upya, kufuatia ulinzi shirikishi kutoonekana. Walieleza kuwa, kwa sasa ndani ya shehia yao hakuna ndizi, muhogo, fenesi, chungwa wala mifugo ya kuku, Ng’ombe na Mbuzi wanaonawiri kwa wizi ulivyokithiri. Mmoja kati ya wananchi hao Mohamed Khamis Ali, alieleza kuwa, kwa miaka zaidi ya sita sasa, hakuna tena ulinzi shirikishi ambao uliondoa vitendo vya uhalifu. ‘’Sasa hakuna mkulima wala mfugaji anaefaidika na mazao yake, kutokana na wizi uliokithiri ambao ni watu kutoka ndani ya shehia yet...

WAMBAA, CHUMBAGENI KUANZISHA MFUKO WA UCHINJAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAUMINI wa dini ya kiislamu shehi za Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamekutana na kukubaliana kuanzisha mfuko maalum wa uchinjaji, kila ifikapo mfunguo tatu, kwa ajili ya sadaka kwa wasiokua na uwezo. Kwenye kikao hicho, kilichofanyika skuli ya Wambaa, waumini hao walisema, imeonekana kuna kundi kubwa kubwa la waumini wenzao, wamekuwa kikosa kitoweleo kwa siku za sikukuu, jambo ambalo sio sahihi. Akizungumza Mwenyekiti wa muda wa mfuko huo Ali Abdi Mohamed, jana Juni 22, 2024  alisema wamekusudia kuwa mfuko huo uwasaidie, wale ambao uwezo wao uko chini. Alieleza kuwa, mpango huo wa uchinjaji kila ifikapo mfunguo tatu, kwa hatua za awali utahusisha kila watu saba, kutakiwa kumiliki Ng’ombe mmoja na kumuwasilisha kwa kamati, kwa ajili ya uchinjaji. Mwenyekiti huyo alisema, kisha baada ya kukamilisha taratibu za uchinjaji, kutagawiwa mafungu matatu, kama sheria ya dini ya kiislamu ilivyoelekeza, ambapo fungu moja hutolewa...

PACSO, YAJENGA DARAJA KWA WAANDISHI, WANAASASI PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari na wana asasi za kiraia Pemba, wametakiwa kufanyakazi kama mwili mmoja, ili wanapofuatilia kero za wananchi, iwe kazi rahisi kuzipatia ufumbuzi.   Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mwemvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamed Najim Omar, wakati akiufungua mkutano wa siku moja, kwa waandishi hao wa habari na wanaasasi za kiraia Pemba, mkutano uliofanyika leo Juni 21, 2024 ukumbi wa Maktba Chake chake.   Alisema, waandishi wa habari na wanaasasi za kiraia, imegundulika wote wanawatetea wananchi wanaokabiliwa na changamoto, mfano ya ukosefu wa barabara, hivyo ni vyema wakashirikiana katika hilo.   Katika hatua nyingine Najim, alisema ushirikiano kati ya pande mbili hizo, unaweza hata kubadilisha sera na sheria, ambazo zinaonekana kupitwa na wakati, katika uendeshaji wa shughuli zao.   Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ‘PACSO’ Sifuni Ali Haji, alisema anategemea baada ya kumalizika kwa mradi huo, ku...

WANAOJIFUNGULIA MAJUMBANI WAZUNGURUKWA NA MAJANGA LUKUKI, KIFO KUPOTEZA DAMU VIMO

  NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ ‘MIMBA yangu ya nne manusura niiage dunia’. Asha Said mama wa watoto wanne ambae sio jina lake halisi anasema, mimba yake ya pili alijifungulia nyumbani, na alipata tatizo la kutokwa na damu nyingi, na kupelekea hadi kupoteza fahamu. ‘’Baada tu ya kujifungua sikujifahamu tena, mpaka nilikuja kuzinduka nimewekewa chupa ya maji hospitali ya Micheweni,’’anaeleza. Mume wa mama huyo ambae hakupenda jina lake lichapishwe, anasema baada ya kuona hali ya mke wake imeshakuwa mbaya, ndipo usiku huo, alipokodi gari na kumpeleka Hospitali. Hivyo alipatwa na huzuni, hali ambayo ilipelekea kupoteza gharama kubwa ya matibabu, kwa ajili ya kuokoa maisha ya mke wake, pamoja na mtoto.   ‘’Nilipata funzo na sasa nikimuona tu uchungu umeanza namuwahisha hospitali haraka, kwani huko akipata matatizo anaweza akawahiwa mapema na watalamu wa afya,’’anaeleza.   Maryam Said mkaazi wa Chake chake ambae anaishi na virusi vya ukimwi kwa muda wa miaka 18, alim...

USHIRIKA 'JAMBO NIA' MFIKIWA KUVUNA 'MAHELA' KWA UVUNAJI ASALI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAUSHIRIKA wa ‘jambo nia’ wa kijiji cha Fuuweni shehia ya Mfikiwa wilaya ya Chake chake, wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki, wamesema wanategemea, kujiingizia wastani wa shilingi milioni 1.6, ikiwa mizinga yao 13, itazalisha chupa 65 za asali. Walisema, fedha hizo wanategemeza kuzipata, miezi minne ijayo kutoka sasa, kupitia mzinga yao 13 walioitega mwaka jana. Walieleza kuwa, fedha hizo zitatokana na kuuza chupa 65, wastani wa shilingi 25,000 hadi 30,000 kwa chupa moja, yenye ujazo wa lita moja. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema waliamua kuanzisha kilimo cha nyuki, kwa malengo kadhaa, ikiwemo kujipatia kipato na kuhifadhi mazingira. Walieleza kuwa, kupitia mizinga hiyo 13, kama hakutavuna upepo mkali ukiambatana na mvua, wanategemea kila mzingia, kuvuna chupa tano, na kujipatia chupa 65 kwa mizinga yote. Mwenyekiti wa ushirika huo Hassein Khamis Salum, alisema wazo hilo, lilikuja kuanzia mwaka 2022, baada...