NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@
WANANCHI wa
shehia ya Uwandani wilaya ya Chake chake Pemba, wamekumbushwa kujitenga mbali na
sulhu za kesi za jiani, ikiwemo za udhalilishaji, kwani kufanya hivyo, ni kuyapalilia
matukio hayo.
Hayo
yameelezwa leo Juni 25, 2024 na Mkuu wa Divisheni ya Katiba na Msaada wa Kisheria
Zanzibar ofisi ya Pemba, Bakar Ali Omar, kwenye hutuba iliyosomwa kwa niaba
yake na Msaidizi wa sheria wa Jimbo la Wawi Haji Nassor, kwenye mkutano wa
wazi, kwa wananchi waliomo ndani ya mpango wa kanusuru kaya maskini, ikiwa ni
sehemu ya wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar.
Alisema,
bado wapo baadhi ya wazazi, wamekuwa wakizikalia mkekani kesi hizo, kwa kuzifanyia
sulhu, jambo ambalo kisheria ni kosa na kuongeza kichocheo kwa watendaji.
‘’Niwasihi
sana wananchi wa Uwandani, tukiwa ndani ya wiki ya msaada wa kisheria, jambo
hilo mliepuke na ikitokezea mkimbile mbele ya vyombo vya sheria,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, aliwataka wananchi hao, kuwatumia wasaidizi wa sheria waliomo ndani
ya shehia yao, pale wanapokuwa na changamoto za kisheria.
Aidha aliwaeleza
wananchi hao kuwa, moja ya jukumu la msingi kwa wasaidizi hao wa sheria, ni
kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria kwa wananchi maskini bila ya malipo.
Hata hivyo,
aliipongeza taasisi ya LFS, kwa kuendelea kufanyakazi na Idara ya Katiba na
Msaada wa kisheria, kupitia mradi wa upatikanaji haki.
Akizungumza kwenye
mkutano huo, Sheha wa Uwandani wilayani humo, Ali Mussa Hamad alisema wazo la Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria pamoja na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria
wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ kufika shehiani humo, ni jema.
Alieleza kuwa,
anajua zipo shehia 32 wilayani humo, hivyo wamethamini shehia ya Uwandani
kuteuliwa na kupewa elimu ya kisheria.
Mapema Mwakilishi
wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania TASAF shehiani humo Khamis Seif Faki,
alisema wazo la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuuleta mfuko huo,
umewakomboa walio wengi.
Aidha aliwakumbusha
walengwa hao, kuendelea kujiwekea akiba kupitia vikundi mbali mbali vya
ushirika, ili wakati watakapotoka ndani ya mpango huo, wasiwe tegemezi kwa
familia zao.
Baadhi ya
wananchi wa Uwandani akiwemo Khadija Abdalla Khamis, aliipongeza Idara ya
Katiba na Msaada wa Kisheria pamoja na ‘CHAPO’ kuwafikishia elimu ya kisheria.
Kwa upande
wake Saada Ali Khamis, alisema moja ya changamoto ndani ya ‘TASAF’ ni kuchelewa
kwa malipo yao na wakati mwingine. kupungua kwa ruzuku.
Mwananchi Kombo
Ali Abdalla ‘Mbunge’ aliwakumbusha wasaidizi wa sheria, kuendelea kuwasaidia
wanawake wanaodhulumiwa mirathi, ardhi na migogoro ya ndoa.
Nae Anithun
Ali Abdalla, alisema changamoto anayoiona ni wanawake walio wengi, wamekuwa na
uwelewa hafifu wa sheria za nchi, na kusababisha kukosa haki zao.
Shehia ya Uwandani
wilaya ya Chake chake, inao wakaazi 3,767 waliomo vijiji vya Gongoni, Pande,
Mibungoni, Mkwajuni, Kwa joto, Kimbuni, Mperani na Mkaani ambapo kati yao 378
wamo katika mpango wa kupewa ruzuku na TASAF.
Wiki ya
msaada wa kisheria Zanzibar ilizinduliwa Juni 24, 2024 na Waziri wa Nchi Afisi,
Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleiman.
Ambapo shughuli
nyingine zinazoendelea kwa Pemba, ni mikutano ya shehia za Micheweni na
Uwandani kwa kuzungumza na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini na
kongamano la wanafunzi wanaosomea uwalimu SUZA Mchanga mdogo.
Hii ni wiki
ya tano wa Msaada wa Kisheria Zanzibar, ambapo ujumbe wa mwaka huu ni ‘tumia
teknologia kurahisisha upatikanaji wa haki' na mgeni rasmi wa kilele hicho
anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Mwisho
Comments
Post a Comment