NA WAANDISHI WETU, PEMBA@@@@
WANACHAMA wa Chama cha
Mapinduzi CCM, 270 wakiwemo wanawake 71 na wanaume 199, wamejitokeza kuomba nafasi
za Ubunge na Uwakilishi katika majimbo 18 kisiwani Pemba.
Kati hao 270, walioomba
nafasi ya Ubunge wote walikuwa ni 147, kati ya hao wanawake ni 40 na wanaume 107,
huku kwa nafasi ya Uwakilishi wote waliomba ni 123, wakiwemo wanawake 31 na
wanaume 92.
Waandishi wa shirika la
Magazeti ya serikali ambao walifika ofisi za CCM za wilaya za Micheweni, Wete,
Mkoani na Chake chake, walibaini kuwa, wilaya ambayo wanawake walijitokeza kwa
wingi ni wilaya za Micheweni na Mkoani ziliokuwa na watia nia idadi sawa ya 19
kwa nafasi ya Ubunge na Uwakilishi kila wilaya.
Wilaya iliyoshika nafasi ya tatu
kwa wanawake wa CCM kujitokeza kwa wingi ni wilaya za Wete, iliyoibua wanawake 17,
huku wilaya ya Chake chake ikishika nafasi nne kwa watia nia 16.
Aidha wilaya ambayo wanawake
waliojitokeza kwa wingi kwa nafasi ya Ubunge ni wilaya ya Micheweni, lililoibua
wanatia 11, ambapo hapo wapo wanaume ni 17, kutoka katika majimbo tofauti.
Kwa upande wa wilaya hiyo, watia
nia wote kwa nafasi ya uwakilishi ni 25, ambapo wanawake ni wanane, huku wanaume
wakiwa 17.
Wilaya ya Mkoani, yenyewe
kwa watia nia ya ubunge ni 41, kati yao wanawake ni tisa na wanaume 32, samba mba
na idadi ya 31, wakiwemo wanawake 10 na wanaume 21.
Kwa upande wa wilaya ya
Chake chake, wapo watia nia 51, kwa nafasi ya ubunge wanawake wakiwa 12 na wanaume
39, huku kwa uwakilishi wakiwa 23 wanawake wanne na wanaume 19.
Kwa mujibu wa taarifa,
wilaya ya Wete ilikuwa na watia nia 44 kwa nafasi ya uwakilishi, wanawake
wakiwa tisa na wanaume 35, huku kwa ubunge wakiwa 27, ambapo wanawake ni wanane
na wanaume 19.
Katibu wa CCM wilya ya Wete
Rished Omar Khalfan aliwataka watia nia wote kuwa watulivu katika kipindi hichi,
cha kusubiri mamuzi ya ngazi ya juu ya chama.
“Watia nia endeleeni kuwa watulivu
ili taratibu za chama zifanyike na kuwarejesha wagombea watatu ambao hao watajinadi
na kisha kupigiwa kura na wajumbe,”alisema.
Naye katibu wa CCM mkoa wa kusini
Pemba Kajoro Vyohoroka aliwataka, watia nia kuto jipitisha pitisha kwa wajumbe,
kwani wakati wa kufanya hivyo kwa sasa bao.
Zoezi la uchukuwaji wa fomu kwa
watia nia kwa nafasi wa CCM mbali mbali, lilianza Juni 28 na kumalizika Julai 2
mwaka huu nchi nzima.
MWISHO.
Comments
Post a Comment