Skip to main content

MWENGE WABISHA HODI CHAKE CHAKE, UKITOKEA MKOANI

 


 

NA MWANDISHI WETU, PEMBA

MKUU wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, ameuhakikishia, uongozi wa mbio za mwenge kitaifa wa mwaka 2025, kwamba watayafanyia kazi maagizo, maelekezo na ushauri waliutoa, hasa suala la kutunza amani na utulivu, kuelekea uchaguzi mkuu.

 

Mkuu huyo wa wilaya aliysema hayo jana, eneo la skuli ya Ngwachani wilayani humo, kwenye hafla ya kumkabidhi mwenge huo, mwenzake wa wilaya ya Chake chake Mgeni Khatib Yahya.

 

Alisema ujumbe wa mwenge kiujumla, umekuja kuwazindua wananchi wa wilaya yake, juu ya umuhimu wa kutunza amani, kwa maslahi mapana ya taifa na watu wake.

 


Alieleza kuwa, wakati mwenge huo unakimbizwa wilayani mwake na kukutana na wananchi, ulisisitiza utunzaji wa amani, na hasa kuelekea mwezi Oktoba mwaka huu, kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi.

 

Dk. Hamad alifahamisha kuwa, jingine ambalo mwenge huo wa uhuru chini ya kiongozi wake Ismail Ali Ussi, ulisisitiza, ni kupiga vita dawa za kulevya nchini.

 

‘’Na hili suala la kupiga vita dawa za kulevya, na sisi wilayani tunaliunga mkono, maana vijana wamekuwa wakiathirika siku hadi siku na kupoteza nguvu kazi ya taifa letu,’’alifafanua.

 

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa wilaya ya Mkoani, aliwapongeza wakimbizwa hao, kwa umoja na mshikamano waliouonesha, katika kipindi chote ndani ya wilaya hiyo.

 

Akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Chake chake mwenge huo na wakimbiza mwenge wake, alimtaka kuutunza, kuenzi, ili nae kuukabidhi wilaya nyingine ukiwa salama.

 

Akisoma taarifa ya mwenge huo kwa wilaya ya Mkoani, Katib tawala wa wilaya hiyo, Miza Hassan Faki, alisema miradi sita ilitembelewa na mwenge huo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15.8.

 


Alieleza kuwa, awali walifanikiwa kukusanya michango yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 52.1, ambapo kati ya fedha hizo, shilingi milioni 13.5 zilitumika kwa usafiri na shilingi milioni 23 kwa ajili ya kuchangia miradi ya mwenge.

 

Mapema, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2025, Ismail Ali Ussi, aliwakumbusha wananchi wa wilaya Mkoani, kuwachagua viongozi wenye hamu ya maendeleo.

 

‘’Naelewa kuwa, mwishoni mwa mwaka huu, Tanzania itaingia kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi, niwaombe mkawachague viongozi, wanaowajali,’’alisema.

 


Aidha, kiongozi huyo wa mbio za mwenge, alisifu usihirikiano aliouona kwa watendaji wa wilaya ya Mkoani, jambo lililompa faraja.

 

Mara baada ya kuupokea mwenge huo, Mkuu wa wilaya ya Chake chake Mgeni Khatib Yahya, aliwahakikisha watembeza mwenge hao, kuwa watakuwa salama na afya njema.

 

Alieleza kuwa, wilaya imeshajipanga kuutembeza mwenge huo kwa umbali wa kilomita 53.5, katika miradi minne, yenye thamani ya zaidi ya shilingi biloni 19.

 


Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Chake chake, waliahidi kuunga mkono mwenge huo, ili kuhakikisha unafungua miradi na kuiwekea mawe ya msingi iliyokusudiwa.

 

Khadija Omar Hassan wa Madungu na mwenzake Aisha Hassan Kassim wa Chanjaani, walisema ujio wa chombo hicho, ni kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja.

 

‘’Mwenge hauna chama wala dini, na haipendezi kuutenga, maana lengo lake ni kuchochea maendeleo kwa wananchi wote,’’walifafanua.

 


Mwenge huo wa uhuru ukiwa wilaya ya Chake chake, utayatembelea miradi minne, ukiwemo ujenzi wa hospital Chonga, mradi wa vijana Wesha, hospital ya huduma za wazazi Gombani na kufanyika mkesha wake Madungu, ambapo asubuhi utaaelekea mko wa kaskazini Pemba.

                   Mwisho     

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...