NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
SIFUNI
Ali Haji ni Katibu Mkuu na ni kiongozi wa mwanzo, anaefanya kazi na mtandao wa
asasi za kiraia katika kisiwa cha Pemba, akiwa wa kwanza mwanamke.
Anasema mtandao huo unaojulikana kwa jina la PACSO, ni
Umoja wa Jumuiya zisizo za kiserikali uliyoanzishwa mwaka 2005.
Katika safari ya uongozi wake, anaendelea kuzisimamia
jumuiya na wanachama waliokuwa Pemba ikiwemo Pegao, Juwauza, na Tamwa.
Sifuni anaendelea kuvunja vikwazo vyake, katika
Jumuiya hiyo kwa zaidi ya miaka sita, akilenga macho yake katika mkoa wa kusini
na kaskazini mwa mji wa Pemba.
Kutokana na juhudi zake na moyo wa kujituma, amekuwa
akilenga uwezo wa kusimamia maendeleo endelevu kwa jamii ya kisiwa hicho.
‘’Nafasi hii haikuja tu, baada ya juhudi zangu
nilizokuwa nikizifanya katika uwanachama wangu, ndipo nilipopigiwa kura kwa
asilimia zote kushika nafasi ya katibu, anafafanua.
Zaidi ya mwaka mmoja taasisi hiyo, haikuwa na mafaniko
yoyote baada ya kusimamiwa na wanaume, ndipo ilipofika mwak 2006 Sifuni
alipojitolea na kuisimamia.
Katika kujinyakulia nafasi ya ukatibu, ni mwanamke wa
kwanza aliyejiamini, asiyekubali kukatishwa tamaa na amekuwa na jukumu kubwa la
kuratibu na kuunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs,.
Sifuni ni mwanamke anayeaminika katika kisiwa hicho,
katika kujenga uwezo, kutoa mafunzo na kuongeza ujuzi kwa wanachama na asasi zilizomo
kuwa na ufanisi.
Kupitia
uongozi wake, ameweza kuunganisha ushirikiano wa maendeleo kwa jamii katika
kufanya mikutano, ndani yake akiwalenga wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Haijawahi kutokea kutokana na mchango wake, amekuwa
akikuza misingi ya utawala bora na ustawi wa wananchi wote wa Pemba.
Ni mwananmke anayesimamia utekelezaji, utamaduni na
uwajibikaji, pamoja na kusaidia utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi.
Amekuwa akiwajibika kwa kusaidia mipango ya Serikali, kuunga
mkono juhudi katika kuboresha uchumi wa wananchi, kupitia malengo ya kitaifa na
Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs.
Ingawa hapo awali alianza kufanya kazi katika jumuiya
ya kuhifadhi mazingira mwaka 1996 na alikuwa mwanamke wa kwanza akihamasisha
jamii juu ya matumizi mabaya ya kasa.
Na aliweza kuihamasisha jamii, kutokana na athari za
utumiaji wa kasa na utoaji wa elimu kwa wananchi, hususan kwa ukanda wa pwani.
Baada ya uhamasishaji huo, aliunda vikundi vya
wajasiriamali vya mboga mboga, akiwa kiongozi na alikuwa na nafasi ya katibu
kwa kuwasaidia wanawake wenzake.
‘’Katika vikundi vya wajasiriamali niliweza kufanya
maendeleo mazuri, kwa kuvisimamia juu ya upandaji wa miti na mazao ya mboga
mboga,’’anaelezea.
Vikundi hivyo alivionesha njia na amevihamasisha na
aliwataka wanawake wasikae nyuma katika kujiinua kiuchumi.
Mbali na kupitia nafasi hizo, kumbe Sifuni alianza uongozi
tangu akiwa skuli ya msingi vitongoji wilaya ya Chake chake, akisimamia
wanafunzi wenzake.
Wakati anasoma skuli hiyo, alikuwa kiongozi wa darasa
na alipenda sana, kujishughulisha na kuuchanganyika na wanafunzi wenzake.
Alipopewa shughuli, alikuwa akizitekeleza na
kuzisimamia vizuri na walimkubali juu ya utendaji wake.
Mwaka 1990 aliajiriwa kuwa mtumishi wa umma, huku akijihusisha
na asasi na jumuiya, akiendeleza vikundi vya wajasiriamali bila muingiliano wa
ajira na uongozi wake.
Kutokana na uwezo alionao juu ya uongzo wake,
haikuathiri majukumu aliyokuwa akiyafanya hata akiwa nyumbani kwake.
Ingawa aliwahi kugombania nafasi ya uwakilishi katika
jimbo la Ole, mwaka 2020 ila hakubahatika na alionesha uthubutu.
Nafasi hiyo ilimpa matumaini na aliweza kuchuana na
mwanamme ila hakuonesha kushindwa baada ya kupata kura moja.
Kutokana na harakati Sifuni anatamani kuwa kiongozi,
maana sifa za mwananmke kiongozi ni kusikiliza ushauri na maoni na wala siyo kutetereka
wala kuburuzwa.
Kwa sasa Sifuni ni Katibu wa umoja wa jumuiya zisizo
za kiserikali Pemba na anajivunia kuwa yeye ni mwanamke wa mwanzo katika jumuiya
hiyo.
Mafanikio makubwa ameyapata katika uongozi wake
kupitia asasi hiyo, ameweza kuingiza
fedha zisizopungua zaidi ya shilingi milioni 700 kwa wastani wa miradi
10 kwa sasa.
WATU
WA KARIBU
Mkrugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Asasi za Kirai PACSO
Mohamed Najim anasema, Sifuni amekuwa kiongozi mzuri, na mwenye ushirikiano na
jamii anaependa kujitoa na kujitolea kwa kufanikisha harakati za maendeleo.
‘’Amekuwa na mawasiliano mbalimbali ndani na nje ya
nchi ili kuhakikisha jamii, inanufaika katika kupata maendeleo kupitia asasi
hii ya kiraia,’’anafafanua.
Suleiman Hamad Salim ni mume wa Sifuni anasema,
amekuwa na ushirikiano mkubwa na wanajamii wa kisiwa cha Pemba, katika kuhamasisha
maendeleo na utatuzi wa changamoto zinazowakumba.
Kaimu Mratibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake
TAMWA- Pemba Amina Ahmed anasema, amekuwa akimjua kwa kuzijengea uwezo jumuiya
hiyo na wanachama, katika kufikia malengo yao ya kikatiba.
Amekuwa kiongozi mzuri, katika kuimarisha uwezo wa
kiutendaji na amekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za jamii.
Ali Abdalla Bakari ni mwanajamii wa Chake chake anasema,
amekuwa akimjua Sifuni, kwa ucheshi na ni mchapakazi mwenye moyo wa kujituma na
kuwa tayari katika majukumu yake.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya uhifadhi na utunzaji wa
mazingira Vitongojo VECA Ali Abdalla Juma anasema, kiongozi huyo ni mwenye
uzalendo na moyo wa kujitolea.
Fatma Suleiman Hamadi ni mtoto wa Sifuni anasema, hata
yeye amerithi uongozi kutoka kwa mama yake kwani amepata mafunzo kupitia asasi
hiyo huku akiwa kiiongozi kwenye jumuiya yake.
Sifuni ni mzaliwa wa shehia ya Vitongoji wilaya ya
Chake chake mwaka 1968 na ni mama mwenye familia ya watoto sita aliyesoma skuli
ya Vitongoji tangu elimu ya msingi hadi sekondari.
Mwaka 2022 Sifuni alistaafu utumishi wa umma na
amejikita katika asasi hiyo, kuwa kiongozi mwenye busara na matumaini ya watu
wa Pemba.
Wanaharakati
na kiongozi wa dini wanalipi
Afisa Program wa chama
cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar TAMWA Khairat Ali anasema,
amewajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika habari zinazozingatia
haki za wanawake katika uongozi, demokrasia na zinazochangia maendeleo ya
jamii.
‘’Tupo hapa kuwafundisha
masuala ya takwimu kwa sababu tunataka kuona jitihada zenu katika kushughulikia
masuala ya wanawake na uongozi zimefika wapi, zinaleta mafanikio kwa kiwango
gani na jamii imezipokea kwa namna gani,’’anafafanua.
Sophia Ngalapi ni mkuu wa
mawasiliano chama cha waandishi wa habari wanawake Zanzibar TAMWA anasema, ni
vyema waandishi wa habari kuwaibua wanawake ambao wana uwezo wa kuongoza kwenye
jamii ili kusaidia kuchapuza maendeleo.
Anasema kuwa wapo
viongozi wanawake, wanawajibika ipasavyo katika majukumu yao na kuibadilisha
jamii kwa kutatua changamoto zilizopo ili kufikisha maendeleo kwa haraka.
Mratibu kutoka Ofisi ya Mufti Shehe Said Ahmed Mohamed
anasema, katika dini ya kiislamu nimeweka wazi nafasi ya mwanamke katika
uongozi, kwani amekuwa mtu bora katika kusimamia na uislamu hauna shaka.
Yohana Ali Mfundo ambae ni Mchungaji kutoka Kanisa la
Mkusanyiko wa Mungu Tanzania (TAG) lililopo Ngerengere Chake chake anasema,
dini yao haijabagua mwanamke asiwe kiongozi, isipokuwa aendeshe kwa kufuata
taratibu na sheria zinavyoelekeza.
MIKATABA
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotolewa na
azimio Oktoba 31 mwaka 2000, limesema kuongezeka ushiriki wa wanawake katika
ngazi za maamuzi, inazidisha semokrasia ya nchi, uchumi, amani na utulivu.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 21(1)
kinaeleza kila Mzanzibar anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu, katika
kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke.
Mkataba wa Kikanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika,
uliotiwa saini mwaka 2008, kupitia Ibara ya nambari 13 kinaeleza kuwekwa mikakati
madhubuti ya kuwawezesha wanawake.
Taarifa ya wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Waze
na Watoto Zanzibar ya mwaka 2024/2025 imebainisha kuwa, tafiti zinaonesha kuwa
nchi zinazozingatia usawa wa kijinsia zimeweza kuimarika kiuchumi kwa kasi kuliko nchi ambazo hazizingatii.
Mkataba wa Kimataifa wa
Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake mwaka 1979 katika kifungu cha
5.2.1 umefafanua kuwa, kuondosha ubaguzi dhidi wanawake na kuhakikisha kuwa
wanafaidika na haki sawa za kiuchumi kijamii, kisiasa na kiraia.
Mkataba wa Wanawake Barani Afrika wa mwaka
2003 na umepitishwa na wakuu na Serikali za Afrika huko Maputo, katika kifungu
5.2.2 unalinda haki za wanawake juu ya aina yoyote ya ubaguzi.
Sera ya Maendeleo ya
Wanawake na jinsia ya mwaka 2000 ya Taifa katika kifungu cha 5.2.3 kinaeleza
kuwa inatoa mwelekeo, mikakati na shughuli mbali mbali za uongozi na maendeleo inazingatia
usawa wa kijinsia.
Na katika Malengo ya
Maendeleo Endelelevu lililoanza mwaka 2015 mpaka 2030 kuhusu lengo 16 limezungumzia
kujaza jamii zenye amani na zilizojumuishi kwa maendeleo endelevu na kuwezesha
upatikanaji wa haki kwa wote.
MWISHO.




Comments
Post a Comment