NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR
Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo Mai 07 imekaa kikao kazi na Benki ya Dunia
kwa ajili ya kupitia mipango ya utekeleza ya Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia
Tanzania- PAMOJA, unaotekelezwa na Wizara hiyo kwa Kushirikiana na Wakala wa
Uwezeshaji KIuchumi (ZEEA).
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mradi wa PAMOJA
Kinazini, Unguja. Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya
Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto Ndugu Daima Mohammed Mkalimoto amesema
kilao hicho kimeleta tija kutokana na
michango ya wadau iliyotolewa ili kuhakikisha utekelezaja wa Mradi
unawanufaisha walengwa walikusudiwa wakiwemo wanawake na watoto.
Ameeleza kwamba Mradi wa
PAMOJA unalengo la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia ZEEA, pia luwalinda na
kuwahifadhi wahanga wa matukio hayo, hivyo
Benki ya Dunia wametoa maelekezo kwaajili ya kuleta ufani.
Naye Mratibu wa Mradi wa
PAMOJA Ndugu Aisha Abbas Seif amesema kikao kazi hicho ni kikao cha pili baada
ya Wizara hiyo kuingiziwa fedha na benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa
Mradi wa PAMOJA.
Kwa Upande wa Benki ya
Dunia akizungumza Mtaalam wa Masuala ya Kijamii, kutoka Benki ya Dunia Ndugu
Tanya D'lima ameishukuru Wizara kwa ushiriki wako katika kikao hicho na amesisitiza
timu ya utekelezaji kuongeza spidi
katika kutekelezaji wa Mradi ili Kwenda samba na muda uliyoekwa kwa lengo la
kuwanufaisha walengwa.
Comments
Post a Comment