Skip to main content

MADEREVA WATAKAOPANDISHA NAULI KUKIONA, ABIRIA WAPEWA USHAURI HUU....

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi kisiwani Pemba, imewataka wananchi watakaodaiwa nauli mpya iwe kwenye dalala, bajaji au bodaboda kwa kisingizio cha kupanda bei ya mafuta, kuripoti katika vyombo vya sheria, kwani serikali haijatangaaza nauli mpya.

Kauli hiyo, imetolewa na Ofisa Mdhamini wa wizara hiyo, Ibrahim Saleh Juma, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia malalamiko ya wananchi, kulipishiwa nauli mpya hivi sasa.

Alisema, serikali inaelewa vyema juu ya changamoto ya kupanda kwa nishati hiyo ya mafuta duniani, ingawa bado, tamko la kupandishwa nauli halijatolewa.

Alieleza kuwa, serikali imekuwa na utaratibu wa kupokea mapendekezo ya upandishwaji wa nauli hiyo kutoka kwa madereva hao, na kisha kukaa pamoja, ili kuangalia uwezekono wa kupandisha ama laa.

Ibrahimu alieleza kuwa, hadi sasa na tokea kupanda kwa nishati hiyo, serikali haijatangaaza nauli mpya, hivyo ni marufuku kwa dereva yeyote, kupandisha nauli hiyo.

Alifafanua kuwa, ni vyema wananchi watakaokumbana na changamoto hiyo, kuchukua nambari ya chombo hicho, na kukilalamikia katika vyombo ya sheria, kwa hatua zaidi.

‘’Tunaelewa kuwa nishati ya mafuta imeshapanda bei, lakini serikali na wamiliki wa gari hizo na vyombo vyingine, hatujakaa tukakubaliana bei mpya, hivyo kwa sasa ziendelee bei za zamani,’’alifafanua.

Hivyo, amerejea wito wake kwa wananchi, kwanza wasikubali kulipishwa nauli mpya na wakitenzwa nguvu, wakimbilie kwenye vyombo vya sheria kuripoti taarifa hiyo.

Aliendelea kusisitiza kuwa, dereva atakejichukulia sheria mikononi mwake, kwa kuwaongezea nauli abiria, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Katika hatua nyingine, Ofisa Mdhamini huyo, aliwataka madereva na makondakta, kuendelea kuwatoza abiria nauli za zamani, na serikali inaendelea kulitafutia ufumbuzi jambo hilo.

‘’Ni kweli madereva wanahaki ya kulalamikia upandaji wa bei ya mafuta, lakini hawana mamlaka ya kupandisha nauli, maana hata mafuta yakishuka bei, wao hawashushi,’’alifafanua.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wenye dalala na gari za mizigo mkoa wa kusini Pemba ‘PESTA’ Hafidh Mbarka Salum, alisema tayari wameshapeleka mapendekezo ya nauli mpya serikalini.

Alisema, baada ya kuona kuna changamoto ya kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta, waliamua haraka mno, kuiarifu serikali na kuwaandikia mapendekezo yao, ili kupunguza ukali wa bei hiyo.

‘’Sasa imeshafika karibu wiki, tokea tupeleke mapendekezo hayo, ingawa siwezi kukutajia aina ya nauli tulizopendekeza, kwa mujibu wa masafa,’’alieleza.



Hata hivyo Katibu mkuu huyo wa ‘PESTA’, amesema Jumuiya yao, haitambui nauli mpya wanazotoleshwa abiria, katika gari za abiria, kwani hadi sasa, mapendekezo yao ya nauli mpya hayajajibiwa serikalini.

‘’Inaumiza na kuuma mno, kuona nishati ya mafuta na gharama nyingine zimeshapanda, lakini nauli bado zinatumika za zamani, niwaombe waendelee na ustahamilivu,’’alisisitiza.

Baadhi ya madereva wa gari za abiria, akiwemo Hassan Ali Mohamed alisema, kwa sasa wanafanyakazi hiyo, kwa hasara kubwa.

Nae Ibrahim Haji Machano, alisema kukosekana kwa nauli mpya, na nishati ya mafuta kupanda, imekuwa kama wanawachumia fedha wenye vituo vya mafuta pekee.

Kwa upande wake Issa Khatib Issa, alisema amekuwa akienda miendo miwili tu kwa siku na kulaza gari, ili kupunguza hasara.

‘’Nikibahatika siku za kuwepo kwa meli, huwa ndio safari yangu moja tu, kisha naenda kuilaza gari, maana mafuta yamepanda na nauli bado ni kongwe,’’alifafanua.

Mwananchi Asha Haji Kombo alisema, juzi alitoleshwa shilingi 1,500 badala ya shilingi 1,000 bei ya zamani, kutoka mjini Chake chake hadi Ngwachwani.

Kwa upande wake Hawa Othman Azizi, alisema alipanda dalala kutoka Mtambile hadi Mkoani, kondakta alimtolesha nauli ya shilingi 1,000 badala ya shilingi 600 ya zamani.

Imebaini kuwa, baadhi makondakta wanaofanyakazi barabara ya Mkoani- Chake chake badala ya nauli ya shilingi 1,800 ya zamani, huwakata abiria kati ya shilingi 2,000 hadi shilingi 2,500.

Ilifahamika kuwa, kwa mara ya mwisho serikali ilitangaaza nauli mpya miaka mitano iliyopita, kufuatia wakati huo, kupanda kwa nishati ya mafuta.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ‘ZURA’ April mwaka huu, ilitangaaza kupanda kwa bei ya mafuta, yakiwemo ya Petroli kutoka shilingi 2,942 kwa mwezi Machi hadi shilingi 3,500.

Mafuta mingine yaliopanda ni ya Dizeli, kutoka shilingi 2,952 hadi shilingi 3,500 huku mafuta ya taa nayo yakichupa hadi shilingi 3,500 kutoka shilingi 2,900 wakati mafuta ya ndege pekee, yakishuka bei kutoka shilingi 2,368 hadi shilingi 2,365.



Nauli za zamani ambazo hadi sasa zinaendelea kutumika kwa baadhi ya maeneo ni shilingi 1,800 Chake chake- Mkoani, shilingi 900 Chake chake- Mizingani, shilingi 1,300 Chake chake hadi Mtambile.

                        Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...