NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MRATIBU Idara ya mashirikiano ya sekta ya umma na binafsi Said Salum Mohamed , amewataka waandishi wa habari kutumia vyema kalamu zao katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mashirikiano baina ya serikali na sekta binafsi, katika uwekezaji wa masuala ya kijamii na kiuchumi ili wananchi kupata huduma bora zinazosimamiwa na sekta hiyo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungimza na wadau wa habari katika mafunzo yakuwajengea uwezo kuhusiana na mashiashirikiano baina ya sekta za umma na binafsi yaliyofanyika ukumbi wa wakala uwezeshaji wananchi kiuchumi Gombani Chakechake Pemba.
Alisema kuwa sekta za umma na binafsi imekuwa na mipango ya kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi ili wananchi wapate huduma hizo zenye kuleta maendeleo.
"Hizi taarifa ziwafikie jamii na wawekezaji katika kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa kuyafikia malengo ya serikali ili wananchi wapate maendeleo,"alifafanua.
Alifafanua kuwa uwekezaji wa umma na binafsi Public Private Partnership(PPP) ni mfumo wa uwekezaji unaohusisha taasisi binafsi kwa kushirikiana na serikali pande zote mbili.
Alisema kuwa majukumu yanayofanywa na taasis hiyo ni kusimamia mikataba ya miradi yote inayoingia kati ya serikali na muekezaji binafsi na alisema kati ya miradi ya uwekezaji kwa mifumo wa Ppp ni bandari, majengo ya serikali,barabara, elimu na viwanda ili kutekelezwa kwa wakati na muda maalumu uliopangwa.
"Majukumu makubwa ya sekta binafsi na umma ni makubaliano ya mkataba wa serikali na sekta binafsi na ufadhili kwa uendeshaji kwa muda maalumu ili kutekeleza miradi hiyo,"alifafanua.
Msimamizi wa sekta binafsi na umma Machano Mmanga Mgeni alisema kuwa,faida kubwa ya Ppp ni kuboresha utoaji wa huduma kwa kuleta ufanisi katika huduma za umma.
Alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisadia ukuaji wa uchumi kwa kuchangia ajira na kuleta maendeleo ya miundombinu na huduma bora.
"Taasisi hii ipewe nafasi ya kufanya kazi kisheria ili kutekeleza miradi ya uwekezaji na jamii ipate huduma bora kwa wakati,"alifafanua.
Alisema kuwa pindipo itakapopewa nafasi sekta hiyo itasaidia upatikanaji wa teknolojia inayoendana na wakati pamoja na kuimarisha ufanisi kwa watendaji.
Akizungumza kwa niaba ya waandishi wenzake Zuwena Shaaban alisema kuwa mafunzo hayo yameweza kuwasaidia kujua mashirikiano yanayofanywa na sekta binafsi na umma kwa serikali kupitia wawekezaji na miradi wanayotekeleza taasisi hiyo.
Alisema kuwa kutoka na mafunzo hayo watakwenda kutumia vyema kalamu zao ili kuitambulisha jamii juu ya maendeleo yanayotekelezwa na sekta hiyo.
"Tuwapongeze sekta hii kwa mafunzo waliyotupatia kwa kutuweza kujua mashirikiano baina ya sekta za umma na binafsi kuputia serikali kuu wa wawekezaji na tunaomba yawe endelelvu ili kuelewa zaid,"alifafanua.
MWISHO.
Comments
Post a Comment