Skip to main content

KUMBE MKAMANDUME ALIKIMBIA VITA IRAN KUJIFICHA PEMBA?

 

 



 

NA RAHEME MOHAMED, PEMBA

 

MOHAMMED bin Abrahman umaarufu "Mkamandume"

 

Ni mshirazi kutoka katika nchi ya Iran, mfalme ambae alifika katika kisiwa cha Pemba mwishoni mwa karne ya 15, yaani miaka 600 iliyopita.

 

Alifikia mji wa Pujini, kijiji cha Kijito Kame ambapo alikuwa pamoja na mke wake na mtoto wao mmoja.

 

Mtoto ambae alijulikana kwa jina la Haroun bin Mohammed bin Abrahman, na hadi kufikia sasa jina halisi la mke ambae alifikanae kutoka Iran halijafahamika.

 

Mfalme Mkamandume, walitoka nchi Iran kwa sababu kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuamua kuingia katika mwambao wa Afrika Mashariki, kutafuta hifadhi.

 

Walifika hapo pamoja na familia yake kwa kutumia usafiri wa majini na chombo, ambacho walitumia ilikuwa ni jahazi.

 

Huo ndio usafiri mashuhuri ulioukitumika katika enzi hizo, kwani hakukuwa na mwingine zaidi ya jahazi.

 

Walifikia katika mji wa Pujini, kijiji cha Kijito Kame ambapo alikaa hapo kwa mashirikiano na wenyeji alipwakitia na kumpa makaazi.

 




Alishirikiana nao katika mambo mbali mbali ikiwemo misiba na harusi, muda wote alipoishi katika mji huo.

 

Kutokana na hadhi yake aliyokuwa nayo, hakupaswa kuishi katika jamii na kuamua kujenga kasri lake, katika eneo ambalo linajulikana maarufu kwa 'Mkama Ndume'.

 

Mfalme Mkama Ndume, alikuwa na uthubutu wa uongozi aliongoza katika kisiwa cha Pemba, wakati huo huo aliongoza katika mji wa Mombasa Kenya.

 

Mfalme huyo, katika kipindi chake cha uongozi kisiwani Pemba aliongoza katika diwani tano.

 

Moja ya diwani hizo ni Pujini ambapo yeye mwenyewe ilikuwa ndipo alipoeka makaazi yake makuu na ndio, pakajulikana kwa jina la Mkama Ndume.

 

Nyingine ni Wapokomo ipatikana kaskazini Mashariki mwa Pemba, hapa palijulikana kuwa ni Micheweni.

 

Watu ambao asiliyao inasadikika kuwa ni jamii ya watu ambao walitoka nchini Kenya.

 

Diwani nyingine ni Chwaka-Tumbe hii inapatikana maeneo ya kaskazini maeneo ya Tumbe hadi Wingwi wilaya ya Micheweni.

 

Nyingine ni diwani ya utenzi ambayo ilijulikana kwa maeneo ya Ziwani, Ole na Meli 5 na Pandani.

 

Diwani nyingine ni Kambaluu ambayo kwa sasa inaitwa rasi Mkumbuu diwani hii inapatikana maeneo ya Mkumbuu, Ndagoni na Wesha.

 

Ukoma ni diwani nyingine, inayopatikana maeneo ya kusini Mkoani, katika maeneo ya Fufuni, Mtambile na Chanjamjawiri.

 

SABABU YA KUITWA 'MKAMA NDUME' 

Mohammed bin Abrahman alijulikana kwa jina la Mkama Ndume, kutokana na kuwa, wakati wa utawala wake, alitunga sheria kwa wanajamii wa Pujini.

 

Sheria ambazo ziliwabama wanawake watu wazima wanapofanya makosa, kuchukuwa mawe kwa miguu kutoka Vitongoji hadi katika Ngome yake.

 


Mawe ambayo yalikuwa yakitumiwa kwa kuendeleza ujenzi wa majengo yaliyojengea wakati huo.

 

Kwa wanaume watuwazima ambao walifanya makosa, wakati huo walikamatwa uume wao na kukamuliwa kama Ng'ombe anavyo kamuliwa maziwa.

 

Hapo ndipo palipopatika jina la 'Mkama Ndume' yaani ‘mkamua waume’.

 

Mfalme Mkama Ndume alikuwa na wake wawili, ambao walikuwa wanaishi katika nyumba moja.

 

Nyumba hiyo iligawiwa sehemu mbili, ambazo hawakuwahi kuonana muda wote walioishi hapo.

 

Katika ngome wa mfalme Mkama Ndume, mulikuwa na kisima, kilichopachikwa jina la kisima wivu.

 

Kisima hicho kimo ndani ya ngome ya Mfalme Mkama Ndume, ambacho kilikuwa kikitumiwa na wake zake hao.

 

Kiliitwa kisima cha wivu, kwa sababu walitumia wake hao wawili, ambao waliolewa na mume mmoja  kwa usiri bila ya kuonana.

 

Mfalme Mkama Ndume alihofia iwapo itatokea kukutana kisimani na kujuwana kuwa ni wake wenza, inawezekana kutokea madhara kwao.

 

Aliamua kuwatenga na kutokujuwana au kukutana katika hali yoyote ile, katika maisha.

 

Wakichota maji katika kisima hicho kwa njia tofauti bila ya kuonana.

 


Upande mmoja wa kisima hicho, kulikuwa na ngazi ambayo mke mmoja, alikuwa anashuka na kuchota maji kwa kutumia kata.

 

Upande mwingine kulikuwa na roda, ambayo ilifungwa na ndoo, ndio ambayo akitumia katika kujipatia maji.

 

Said Omar Said, ambae ni Ofisa Muhifadhi katika eneo hilo la kihistoria Mkama Ndume, anaeleza kuwa moja miongoni mwa siku, wake wa Mfalme wakiwa katika eneo la kisimani kuchota maji vyombo vyao vilikutana.

 

Mke mkubwa akashtushwa na hili ile, na kuamua kumuhadithia mume wake kuwa ameona kata imegongana na chombo chake, wakati akichota maji.

 

Hapo ndipo Mkama Ndume alipomtuliza kwa kumfahamisha kuwa, huenda ikawa ni mzimu uliopo katika kisima hicho.

 

Mfalme Mkama Ndume, alimshauri mke wake kukwepa uwo muda aliokwenda, kwa lengo la kuuachia mzimu kutumia na kupanga muda mwingine, ili asije akamletea madhara.

 

Mke mkubwa akafahamu hivyo bila ya kujuwa siri ambayo, ilifichwa na Mkama Ndume.

 

Mtandao wa wikipedia.org unatufahamisha kuwa, kisima hicho, kilikuwa na pande mbili zilizogawiwa kwa kuekwa ukuta katikati.

 

Ukuta ambao, uliwazuwiya wake hao wawili wa Mfalme, bila ya kuonana katika mazingira hayo.

 

Upande mmoja, alikuwa anatumia mke mkubwa kwa kuchota maji kwa kutumia roda.

 

Upande mwingine alitumia mke mdogo kwa kushuka kwa ngazi na kuchota maji kwa kutumia kata.

 

Katika muda wote walioishi hapo haikutokea siku wakakutana katika hali yoyote ile.

 

Kwa mara ya kwanza walikutana wakati walipokuwa wanaondoka pamoja na mume wao.

 

Aidha historia inatueleza kuwa, kisima hicho kinatumika kwa masuala ya kiibada mbali mbali za kijadi.

 

Ibada ambazo watu hufika katika eneo hilo na kuomba maombi yao, kwa wale walio na matatizo ya kimapenzi.

 

Mara baada ya mafanikio hufika tena kwa kutoa sadaka kama ni zawadi kwao, kutokana na mafanikio waliyoyapata.

 

Zawadi hizo hutumiwa na watu wa jamii iliyozunguka katika eneo hilo.

 

NJIA WALIYOPITIA WAKATI WANAONDOKA

Historia inatueleza kuwa, kulikuwa na chumba ambacho kilikuwepo chini ya bahari, huko ndiko ambako alifikilia Mfalme Mkama Ndume yeye na wake zake.

 

Kuna sehemu ambayo walioingia na kupita chini kwa chini hadi kufika katika chumba hicho.

 

Kwa mujibu wa utafiti ambae alijulikana kwa jina la Adria Laviolete aliefika miaka ya 1987 aligundua chumba hicho.

 


Chumba ambacho kipo chini ya bahari, ambapo alikuwa kuna ngazi 14, kufika katika chumba hicho.

 

Hadi kufika sasa haikujulikana tena kuwa ni sehemu gani ambayo walielekea Mfalme Mkama Ndume, pamoja na wake zake hao.

 

Mfalme Mohammed bin Abrahman 'Mkama Ndume' alibahatika kuzaa watoto wanne, ambao wote alizaa na mke mkubwa.

 

Mtoto wake mmoja, aliitwa Haroun bin Mohammed bin Abrahman ambae alitawala katika eneo la Chwaka- Tumbe.

 

Mwingine aliitwa Mjawiri, ambae alikuwepo maeneo ya Chanja mjawiri, kama jina lilivyo maarufu kwa sasa.

 

Huyu inasemekana kuwa, mara baada ya kuondoka baba yake, aliomba kupasuka ardhi na kuingia na hakujilikana alikokwenda.

 

Mwingine alijulikana kwa jina la Mwana mtoto ambae, akiishi katika kijiji cha mwana mtoto, kilichopo hapo hapo Pujini.

 

Na mwingine hakuwahi kupatikana jina lake kutokana na kuwa alifariki akiwa hajapatiwa jina.

 

Said Omar Said kutoka eneo la hifadhi ya Mkama Ndume, anafahamisha kuwa, kiwango cha watalii ambao hufika katika ngome hiyo ni ndogo sana na hairidhishi.

 

Kwani kwa mwaka, hupata ugeni wa wanafunzi wanaokuja kujifunza wasiozidi 800 na wageni wa ndani ya nchi au wakaazi wa kisiwa hichi cha Pemba, wasiozidi 100.

 

Wkati ambapo watalii wa nje hali ikiwa imezidi kupunguza wao ni wastani wa wageni 50, jambo ambalo kwa idadi hiyo ni ndogo.

 

Said amefahamisha kuwa, iwapo jamii itapata mwamko wa kufika katika sehemu za kihistoria, kuona uhalisia wa maeneo waliyoishi watawala wa zamani.

 

Wanaweza kujijengea uelewa zaidi kuliko kutosheka na masomo wanayosoma wanapokuwa madarasani, au hadithi na wazazi nyumbani.

 

Kwa upande wake Saleh Omar Juma Mkuu wa divisheni wa Makumbusho na Mambo ya Kale Pemba anasema, taasisi mbalimbali zinazohusiana na Mambo ya utalii, kuwaelekeza watalii wanapofika Unguja kufika Pemba.

 

Anasema kuwa, watakapofika Pemba, wanaweza kusaidia kuingiza mapato ya serikali na kuongeza kuenea kwa historia ya visiwa hivi.

 

Amesema iwapo watafanya hivyo wanaweza kuwasaidia wao kwa kuongeza idadi ya wageni.

 

                  MWISHO.

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...