Skip to main content

UMEWAHI KUHADITHIWA KUHUSU CHAKULA AINA YA MWATA, WANAUME WAPIGANA FOLENI SUPU YAKE

 



NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

“NIWEKEE kisongo pawa 2000, supu weka nyingi na pili pili kwa mbali na kiungwa”, lugha za kuagizia supu ya Mwata.

Sio lugha ngeni kwa wafanya biashara na watu wanaouza supu hiyo ya Mwata hususan katika maeneo ya Kangani na vitongoji vyake.

Wenyewe hutumia jina la “kisongopawa”kama umaarufu lakini jina halisi ni Mwata, ndilo watu wengi kutoka maeneo mbali mbali hufahamu kwa haraka.

Na jina la kisongopawa si rasmi na si lenye kufahamika isipokua kwa wenyeji wa maeneo ya Kangani na jirani ambako  ndio mwata huvuliwa na kuliwa .

Mwata ni  aina  ya viumbe vipatikanavyo pwani, ambacho hutumiwa kwa ajili ya chakula au kitoweo kama ilivyo viumbe vingi vya baharini, ingawa umetofautiana navyo kwa kiasi kikubwa hata uvuvi wake.

Mwata kisiwani Pemba hupatikana zaidi na kuhesabiwa kama ni kitoweo adhimu katika Pwani ya Jemele iliopo shehia ya Kangani wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba.

Ingawa baadhi ya watu hueleza yapo maeneo mingine yanayopatikana Mwata, lakini watu wa maeneo hayo hawauchukulii kama ni chakula.

Badala yake hutumia kama chambo cha kuvulia samaki au viumbe wingine wa baharini, huku baadhi ya watu wakisema huo ni tofauti na ule unaovuliwa Kangani na kuliwa.

Ila kuzingatiwa kwake kama kitoweleo muhimu tena cha enzi na enzi kwa wakaazi wa Kangani kumeipa kijiji hicho na maeneo jirani ya Mjimbini na Kukuu umaarufu mkubwa.

Na hadi sasa ukitaja Kangani, Mjimbini na Kukuu kwa anaekujua au kukusikia hutanguliza swali kama mwata upo? ni sawa na kusema Pemba na karafuu.

Na umaarufu huu umekaa vichwani kwa watu miaka na miaka hadi sasa, ambapo unazingatiwa na vizazi kwa vizazi.

 HUPATIKANA KATIKA ENEO GANI?

Aina hii ya kiumbe cha baharini, hupatikana katika sehemu za pwani zenye mchanga mweupe ambapo panafikiwa na maji,  yaani sehemu ambazo  maji yanaingia na kutoka (kupwa na kujaa).

Fumu Haji ni miongoni mwa wavuvi maarufu wa Mwata anasema, viumbe hao huonekana zaidi sehemu zenye usafi wa mazingira na mchanga mwingi uliotulia.

“Kila sehemu ikiwa safi zaidi na mchanga mwingi na unaofikiwa na maji na kutoka, ndipo viumbe hawa huonekana zaidi kuliko sehemu nyingine”, anafahamisha.

Anasema si rahisi kuonekana na kila mtu pale anapofika pwani kwa lengo la kuwatafuta, kwani si watu wengi ambao wanaweza kutambua uwepo wa Mwata katika eneo fulani.

Wakati Makame Ali Makame nae ni mvuvi wa mwata anaeleza, ‘’sio kila mvuvi anaweza kuvua Mwata kwani  unaweza kuwa mvuvi wa samaki na usiweze kuvua Mwata’’.

Maana sehemu unapopatikana kunahitaji uzoefu wa hali ya juu, kwakuwa hata ishara zinazo ashiria uwepo wa kiumbe hicho zinamuhitaji mzoefu.

Anasema ishara kama kishimo ndio inayoonesha kuwepo kwa mwata katika eneo, ila pia kishimo hicho si chakueleweka kwa kila mmoja.



Anaeleza wakati ambao maji hukauka ndio wakati unaopatikana mwata na bamvua likiisha yaani maji yakijaa ni vigumu Mwata kupatikana.

                                        UVUVI WAKE

Mchakato wa uvuvi wa mwata unatofautiana kidogo na uvuvi wa viumbe kama samaki, Pweza na hata viumbe vyingine wa baharini ingawa wote kwa pamoja wanaishi katika mazingira yanayofanana.

Abass Haji Mkaazi wa Kangani anasema, nilazima mvuvi awe na ujiti maalum wenye urefu  kutoka ncha ya  kidole cha kati cha mkono hadi kwenye “mirfaki” yaani futi moja.

Anaeleza ujiti huo unaweza kuwa wa mti kama Mkoko michanga, Mbungo na miti mingine yenye ncha kali na kupinda pinda.

Anaongeza sio kila mti wenye ncha unaweza kutumika kuvulia Mwata, akitolea mfano mti wa mpenda pendapo ingawa unancha ila hauwezi kutumika kuvulia Mwata.

“Kuvua Mwata tunatumia ujiti maalumu wenye urefu wa futi moja ambao una ncha kali, na mara nyingi tunatumia miti kama Mikoko michanga, ila si kila mti unaweza kutumia” anafahamisha.

                                       MUONEKANO WA MWATA

Muonekano wa mwata baada ya kuvuliwa ni mithili ya uchango wa kuku ama bata, kwa upana kama huo kwa wale wachanga na wapevu wakiwa ni wenye kuongezeka kidogo.



Urefu wake unaweza kufikia hadi sentimita 30 kwa waliopea na sentimita 20 hadi 25 kwa ambao hawajapea vizuri.

Mwata ukivuliwa unakua ni wenye kujifumba ambapo ndani yake huonekana kuwa na mchanga mweupe wa pwani na muda mwingine hua na chango ambazo ni kidogo sana.

Mara nyingi muonekano wake huwapa mashaka walaji hasa wale wanaouona kwa mara ya kwanza, kwani huufananisha na uchango wa kuku na wengi hushindwa kuula hasa wale ambao hawauoni sana.

Mwata huwa ni warangi nyeupe kwa ule mchanga au mpevu kiasi, na rangi manjano kwa ule mpevu zaidi ambao wengi wakiuona kwa mara ya kwanza hushtuka.

Aina hii ya mwata mkubwa hupatikana kwa kuzamia na ni madrassa sana kupatikana na umepewa jina la “mwata koko”.

                                                       UPISHI WAKE

Mwata hupikwa kwa namna tofauti, kulingana na matakwa ya mlaji ambapo hutofautiana ladha kulingana na namna ya upishi.

Kuna wanaopika kwa mchemsho wa kawaida wa mwata maji na chumvi, huku wataalamu wa upishi huo wakisema ladha huwa nzuri zaidi ukipikiwa maji ya chumvi “yabaharini”.

Mara chache hutiwa pilipili, na aina hii ya mchemsho ndio ambao hupendwa na watu wengi hasa wanaojizowesha kuula.

Na wingine hupikwa mchemsho kwa kuongeza baadhi ya vifaa kama kitunguu swaumu, uzile na bizari ambapo aina hii ya mchemsho wa mwata hutumiwa na wafanyabiashara wingi, kwani ni yenye kuwavutia wateja, na hupendelewa zaidi na wazoefu wa ulaji huu.



Mwata hupikwa kwa kukaangwa, na aina hii ya upishi hupendelewa zaidi na watu ambao si wazoefu wa ulaji wa mwata.

                                            WALAJI WAKE/WATEJA WAKE

Mwata ni aina ya kitoweo ambacho hupendelewa zaidi na wakaazi wa maeneo ya karibu na bahari au ambao washawahi kuishi katika maeneo hayo.

Anasema mmoja kati ya wavuvi wa Mwata Khadija Mcha Amour wa Kangani kwa miaka ya nyuma, haukuwa na wateja wengi wala bei inayoridhisha.

Anaeleza mwata ulichukuliwa kama ni kitoweleo cha waliokosa pesa au waliokosa samaki na kuufanya kuwa ni chaguo lao la mwisho.

Anaeleza mwata haukua na thamani kama ilivyo sasa, na haukua na wateja wa uhakika wala soko la uhakika na walikua wanavua kama bahati nasibu, na mvuvi hakuwa anapata mteja akaridhika.

Anafahamisha walikuwa wakiuza kwa kupitisha mitaani ambapo mwata ulipangwa siniani na kupewa watoto kuutembeza na muda mwingi huenda nao masafa marefu bila kupata wateja.

“Kwa miaka ya nyuma mwata haukuwa na wateja wengi  wala bei inayoridhisha, na haukuwa na  wateja wa uhakika wala soko la uhakika tulikuwa tunavua kama bahati nasibu, na  mara nyingi tulikua tuna kula wenyewe”, anaeleza.

Khadija anasema mbali na kukosa wateja pia thamani yake ilikua ndogo sana, kwani fungu lenye Mwata 10 hadi 15 lilikuwa likiuzwa kwa shillingi 500 bei ambayo haikuendana  na juhudi za mvuvi.

Time Kebu Ali, pia ni mvuvi wa mwata anasema wateja wao wengine maarufu ni wafanyabiashara, anasema kutokana na umaarufu wa mwata siku hizi pia kuna kundi la wafanyabiasha ambao hununua mbichi na kupika supu na kuuza.

Anaeleza hili pia limeongeza thamani kwa wavuvi kwani limefanya mwata kuwa wa thamani na wenye kumfaidisha mvuvi, kwani kwa sasa fungu la jumla ya mwata 6 au 8 huuzwa kwa shilling 1000, bei yenye manufaa kwa mvuvi.

Anafafanua pamoja na kuongezeka thamani Mwata haupatikani kwa wingi kama ulivyokua zamani, hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayopelekea kujaa kwa maji chumvi katika sehemu zinazotegemewa kutoka maji ili mwata uishi.

Ali Mohamed Makame ni mfanyabiashara wa supu ya mwata ambayo imempa jina la umaarufu (kisongo pawa) anaeleza, wateja wake wengi hukimbilia supu ya mwata kuliko aina nyengine ya supu.

Anafahamisha ingawa kiingilio ni shillingi 500 ila wapo watu wanakunywa hata ya 5000 kitako kimoja kutokana na upenzi walionao kwa supu hiyo.

Bikombo Khamis ni muuza supu ya mwata anafafanua, wanaume ndio huvutiwa zaidi na supu ya Mwata kuliko wanawake na wateja wake, wengi ni watu wazima kuliko vijana.

“Supu ya mwata ni supu inayopendwa zaidi kuliko aina nyingine ya supu kwa hizi nnazouza mimi, na wateja wangu wengi ni wanaume kuliko wanawake”, anaeleza.

                                                       FAIDA ZA KIAFYA

Kama ilivyo kwa vitoweo vya baharini kuwa na umuhimu mkubwa kwa ujenzi wa afya ya binaadamu mwata pia una umuhimu mkubwa kiafya.

Mwata unamadini ya Iodini na Amaino asidi yanayotengeneza homoni za kudhibiti uvimbe katika mwili.

Huzalisha kabohaidreti inayosaidia kuimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mwata  pia huimarisha afya ya mifupa.

Mmoja ya wakaazi wa Kangani Jamila Khatibu Faki anasema, wao hula mwata kama sio kitoweo rasmi, bali ni kama kiburudisho au nyongeza tu, kama ilivyo kachumbari kwa baadhi ya watu.

Nae Far-hat Mohamed wa Kangani anasema, umaarufu wa mwata ni  miongoni mwa vitu wanavyojivunia, kwani umebeba utambulisho wao katika  maeneo mbali mbali, kama ilivyo vyakula vyingine.

                                                                 MWISHO.

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...