Skip to main content

HISTORIA PANGO LA KIJIJI MAKANGALE, INASISIMUA, INATISHA

 



NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@

PANGO la kijij, linalopatikana shehia ya Makangale, kaskazini  mwa Pemba.

Ni mojawapo ya kivutio cha kihistoria vyenye hadithi ya kipekee.

Umaarufu wa pango hili, ulianza mwaka 2009 baada ya Profesa Felix Chami wa Chuo Kikuu cha Dar- es Salaam, kugundua mabaki ya kihistoria, ikiwemo mifupa ya wanyama, shanga, mkaa, na vigae vinavyoashiria uwepo wa makazi ya binadamu katika vipindi tofauti vya kihistoria kwenye pango hilo.

Kwa mujibu wa historia, pango hili lilitumiwa na wapiganaji wa vita ya kwanza ya dunia 1914 hadi mwaka 1918.

Na baadae vita ya pili ya dunia yam waka 1939 hadi mwaka 1945, kama maficho yao na pia sehemu ya kuficha silaha.

Leo hii, pango la kijiji Makangale limekuwa kivutio kikubwa cha watalii, wanaotembelea hasa hoteli za kaskazini Pemba, hufika kushuhudia uzuri na historia ya pango hilo, lenye milango miwili wa kuingilia na wa kutokea.
Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Pemba imeboresha njia za kuingia pangoni humo, ili kurahisisha wageni wanapokaribishwa.

Maana wageni hao huwa, wanavutiwa na sauti za popo wadogo ambao ni wanyama wa kudumu wa katika pango hilo.

 Yussuf Haji Khatib ni Afisa Muhifadhi wa Mambo ya Kale Pemba, anasema eneo la kihistoria la pango la kijiji ni sehemu muhimu ya kihistoria, hapa kisiwani Pemba.

Umuhimu wake umekuja zaidi, baada ya Proffesa Felix Chami kutoka chuo kikuu cha Dar-es- Saalam kufanya utafiti mwaka 2009 wa kiaklojia.



Utafiti huo aliufanya kwa kuchimba chini (systemically) na baada ya kufanya utafiti huo, alipata mabaki mbali mbali.

Kama vile vigae vya zamani vya vyungu, majagi ya kutilia maji vya udongo na kigae.

Mabaki hayo ya udongo na kigae, yaliyokutikana chini  yalitengenezwa nje na ndani ya nchi  na paliashiria kuwa eneo hilo palikuwa na makaazi ya watu na shughuli zao.

Kwa mujibu wa vigae watu hao, walifanya biashara  na watu wa nje na walikuwa wana mawasiliano baina yao kutokana na vigae hivyo, vilionesha kuwa vinatoka mataifa kama China, Iran, India.

Vigae hivyo vilitoa tafsiri pana, kutokana uhalisia wake, katika eneo hilo, palipatikana na mbegu za mimea ya mitama.

Katika utafiti huo, hata kama palikuwa na maakazi ya watu kutokana na mbegu hizo shughuli za kilimo kwa jamii ya watu wa hapo, zilikuwepo tangu enzi za chuma.

Enzi za chuma hapo Afrika, kuanzia miaka 200 kabla ukiristo mpaka miaka 1000 common error.



Mwaka 2012, alifanya utafiti tasisi ya max plan na ikarejea tena mwaka 2016, na akapata mabaki kama aliyoyapata Chami na mingine  kama vile mifupa ya panya wakubwa.

Inafahamika kiwa, hao ndio waliopata mabaki mingi zaidi na waliamini kuwa, kisiwa cha Pemba huenda ndIo kisiwa cha minosia kilichotajwa katik kitabu cha zamani  cha wagiriki yaani (periplus).

Minosia ni kisiwa kinachoishi mamba, ambao hawazuru  kaskazini mwa pango la kijiji, kulikuwa na mji wa kale unaoitwa Msuka mjini.

Pamoja na hilo, waliamini kuwa kuna mawasiliano ya watu, katika kuhifadhi na kulitumia shughuli mbali mbali.

Na ilisemekana kuwa, katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia, watu walilitumia lile pango kwa kujifichia.

 Sababu ya kujifichia, kuliokotwa mzinga wa wajerumani uliotumiwa na vikosi vya kiengereza, kati ya kisiwa cha Njau na huba wa Mkiya wa ng’ombe.



Anasema kinadharia pango hilo, ni makaazi ya wanyama na wadudu wa asili kama kaa, ambao ni kivutio kwa wageni na popo wadogo wadogo wingi, wanaoishi pango hilo.

Popo hao huwa hawajifichi hata wanapoona watu na pango hilo, likabakia kuwa ni la saili na lenye mandhari mazuri kwa watalii.

Kwa sasa mabaki yaliyofanyiwa utafiti yamehifadhiwa na hifadhi na Idara ya Mambo ya Kale Pemba, kwa ajili ya kumbukumbu na kivutio kwa wengine.

Kumbe ukiingia katika Pango hilo, utapokelewa na sauti nzuri za popo wadogo, ambao ni miongoni mwa wanyama wanaoishi katika pango hilo.

 

Afisa anasema, hata magego ya meno ya mwanadamu yalipatikana na hata hivyo yalipimwa na kufanyiwa uchunguzi magego hayo.

Inafahamika kuwa, yaligundulikana kuwa makaazi ya watu yalianza miaka ya 5,000 iliyopita.

 

Kwa sasa pango hilo hufanyiwa marekebisho, ila likabakia na uhalisia wake ulele na marekebisho hayo ni pamoja na  ngazi za kupandia.

 

 

 Na pembezoni mwa pango hilo, pamewekwa huduma za kibinaadamu, hasa kwa waleo wanaotembelea, wakiwemo wanafunzi

 

 Saleh Omar Juma ni mkuu wa divisheni na Uthibiti wa Mambo ya Kale, anasema katika upokeaji wa wageni upo kiasi kwa mwaka na itaegemea na msimu wa kipindi unavyokwenda.

 Kwa sasa eneo hilo limo, katika orodha ya  maeneo ya sehemu za kihistoria yanayohifadhiwa na kutunzwa.

Hata kama ni kivutio, kumbe kumetofautiana baina ya mtalii kiingilio ni dola tano, mtu mzima mzawa shilingi  2000.

Na makundi ya wanafunzi wa sekondari hulipia shilingi 1,000 na skuli za msingi ni shilingi 500 pamoja na maandalizi huingia kwa makundi kwa bei ya mapatano.

  

    MWISHO. 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...