Skip to main content

MAKABURI YA MAZRUI NA HADITHI INAYOTIA HURUMA PEMBA, MABAKI YAISHI KWA MIAKA 300 SASA

  

 NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@

MAKABURI ya Mazrui, ni sehemu ya kihistoria inayopatikana  Chwaka, shehia ya Tumbe mashariki wilaya ya Micheweni Kaskazini Pemba.

Ni sehemu moja wapo ya kivutio cha kihistoria, hutembelewa na wageni wa ndani na nje ya nchi, ili kulinda urithi na utamaduni unaopatikana humo.

Makaburi ya mazrui ni eneo la tatu la sehemu ya kihistoria, katika eneo hilo na lenye mabaki  ya utawala wa Mazrui waliohamia katika karne ya 18.

Ni miongoni mwa mabaki yaliyopo hapo ni hayo makaburi yaliyokuwepo sehemu hiyo.

Tukisema makaburi ni sehemu maalum ,iliyotengwa kwa ajili ya kuzikwa kiumbe kilichokufa na kuhifadhiwa, kwa safari yake ya milele.

MAZRUI KUHAMA KWAO KUINGIA PEMBA

Mohamed Yussuf Khamis, ni Afisa Mambo ya Kale anasema  Wamazrui kwa jina jengine wanaitwa (Waarabu), wa kabila la kimazrui, wanatokana na asili ya taifa la Oman.

Anasema, walihama kwao na kuja katika upwa wa Afrika Mashariki kwa lengo la kufanya biashara na kutawala.

Kabla ya kuhama Oman, kulikuwa na sababu ya kuingia vitani na kabila la Albusait.

Albusait ni kabila ambalo, lililikuja kutawala Zanzibar nzima, ukoo huo ulijulikana kwa jina la Said Saiyd bin Sultan kwa wakati huo.

Makabila ya mazrui na Albusait, walipigana vita huko nchini kwao Oman, kabla ya kuhamia katika ukanda huu wa pwani.

Kutokana na Said bin Sultani, alitawala hapa Zanzibar na wamazrui, waliamua kupigana vita na Said bin Sultani huko Oman.

Inasemekana vita hivyo, vilipiganishwa na Muengereza kwa sababu ya matakwa yake ya kiutawala, rasilimali na biashara.

Vita hivyo viliendelea mpaka pale Albusaiti, akashinda na kupata madaraka nchini Omani.

Baada ya kushindwa kwa vita hivyo, lilitoka tamko kuwa Mazrui aondoke aende Afrika Mashafriki.

Hapa sasa Mazrui, walitawala ukanda wa Afrika Mashariki  katika miji mikubwa katika karne ya 18 na kuenea maeneo ya Zanzibar, Kilwa, Mombasa na Pemba.

Kutokana na Mazrui kuenea ukanda huo, ndipo walipoingia katika kijiji cha Chwaka Tumbe na kuanza maisha yao mapya.

KWA NINI PAKAITWA MAKABURI YA MAZRUI

Kuhusiana na makaburi ya Mazrui, kielelezo cha kuwa baada ya kufa katika eneo, walilohamia hapo Chwaka Tumbe, walichagua eneo maalum kwa ajili ya kuzikana baada ya kufa.

 Hata kama ilikuwa ni eneo lilotengwa na makaburi yao yalikuwa, maalum yaani siyo ya kawaida kutokana famila ya  kiutawala katika sehemu hiyo.

‘’Makaburi hayo unaweza kutofautisha kutokana na hadhi ya makaburi yalivyojengwa, ikiwa la kiutawala, mtoto au mwanamke na mwanamme,’ anasimulia.



Ingwa kwa sasa makaburi hayo, hayakujulikana ni mangapi ila walizikwa kwa heshima na makaburi yalijengwa ili kutofautisha kaburi, moja na jingine.

Makaburi yalitofautishwa kutokana na hadhi ya mtu aliyekufa, ikawa kila mtu anazikwa kwa kujengewa kaburi kutokana na hadhi, na utawala wake.

‘’Mijengo hiyo ilikuwa ikizingatia sana kiutwala na ukubwa na hadhi ya  makaburi,’’ anafafanua.

Hapo palikuwa na kielelezo ya kuwa palikuwa na watu walikufa na kuzikwa sehemu hiyo.

Saleh Omar Juma, ni mkuu wa divisheni na Uthibiti wa Mambo ya kale, anasema katika kisiwa cha Pemba, kuna urithi wa kimaumbile na urithi wa ndani.

Unaweza kusema urithi, unaoshikika na urithi usioshikika, kwa urithi unaoshikika yaani ni huu wa kimaumbile amabo unaonekana katika maeneo ya kihistoria.

Anasema katika upokeaji wa wageni, upo kiasi kwa mwaka na itaegemea na msimu wa kipindi unavyokwenda.

Aina ya watu wanaotembelea katika eneo hilo ni watafiti, watalii na wanafunzi, ila kiingilio kinatofautiana baina ya mgeni na mzawa.

‘’Katika jamii zetu za kawaida, tunazoishi muamko bado mdogo wa utembeleaji wa eneo hilo zaid kwa watu maalum,’’anafafanua.

Anasema katika makundi, wanaotembelea eneo hilo wapo na wageni kutoka nje ya nchi na kila mwaka, hutokezea watafiti kuingia sehemu hizo, kwa ajili ya utafiti hulipia ada ya eneo hilo. 



Kutona na jamii iliyopo, kwa sasa imekuwa ni sehemu ya kihistoria lilojengewa na ndani yake yamo makaburi.

Kwa sasa eneo hilo, limo katika orodha ya  maeneo ya sehemu za kihistoria yanayohifadhiwa na kutunzwa na serikali.

Kwa mtalii kiingilio ni dola tano, mtu mzima mzawa shilingi 2,000 na makundi ya wanafunzi wa sekondari, hulipia shilingi 1,000 na skuli za msingi shilingi 500 pamoja na maandalizi huingia kwa makundi kwa bei ya masikizano.

 Kumbe makaburi hayo yalikuja karne ya 18, baada ya utawala wa Haroun eneo la makaburi ya Mazrui ni kijiji ambacho kilikaliwa na wakaazi hao.


Kutokana na umuhimu wa eneo hilo, serikali imekuwa ikiyaenzi na kuyathamini maeneo hayo, hata hotuba ya bajeti ya Utalii na Mambo ya Kale katika baraza la wawakilishi ya mwaka 2025/2026, imelithibitisha hilo.

Inasema lengo la kuyaendeleza ni kukuza pato la taifa kupitia sekta ya utalii, kuwashawishi wawekezaji wa ndani na nje, kuanzisha miradi ya utalii na urithi wa kihistoria, itakayotoa tija kwa wananchi.

 Kusimamia na kuendeleza makumbusho ya kihistoria na mambo ya kale kuyalinda, kuyahifadhi na kuyatangaza maeneo ya urithi wa kihistoria yaliyopo nchini.

Wizara inayoshughulikia maeneo ya kihistoria, imekuwa ikishirikiana na taasisi za elimu ya juu, za kitaifa na kimataifa katika jitihada za kufanya tafiti kubwa za akiolojia, kwa lengo la kufahamu kwa kina historia ya sehemu husika.

Maeneo ambayo yamefanyiwa utafiti ni pamoja na eneo la kihistoria la Chwaka Tumbe, lilikoko kaskazini wa kisiwa cha Pemba.

 Wizara imekuwa ikiendelea kutekeleza programu ya kuyaimarisha na kuyaendeleza maeneo ya kihistoria, yaliyopo nchini kwa ujumla.

Katika kipindi hiki cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya nane, imefanikiwa kufanya matengenezo makubwa kwa eneo la kihistoria la Chwaka Tumbe.

Kuendelea kuyafanyia matengenezo eneo hilo ni hatua moja wapo ya kutunza na kuhifadhi historia iliyopo nchini, kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

  MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...