NA KHAULAT SULEIMAN, SUZA@@@@
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, amesema kua Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, inajukumu la kuhakikisha wanalinda mila, silka na asili ya Zanzibar, kwa kuona kua ni fursa kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Ameeleza hayo kwenye Tamasha la Utamaduni wa mswahili wa kipemba, jana August 25, 2024 lililofanyika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema wakati umefika sasa kwa Wizara hiyo, kwa kuweka taratibu mbali mbali ambazo zitaihamasisha jamii, kuendeleza kulinda na kuuenzi utamaduni wa Zanzibar.
"Wizara mnatakiwa kua wabunifu, ili kuendelea kuongeza watalii na pato katika nchi, mnatakiwa kutoa elimu katika jamii, kwamba utalii sio wa kutembea uchi, kwani ni fursa ambayo inasaidia kuleta maendeleo yenye kulinda heshima na utamaduni,''alisema.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mudrik Ramadhani Soraga, amempongeza Afisa Mdhamin Zuhura Mgeni Othman kwa kuona ipo haja ya kuandaa matamasha ambayo yatasaidia kuikumbusha jamiii kuendeleza mila na tamaduni zao.
"Dhamira ya matamasha haya, ni kufungua fursa za uwekezaji na utalii, ambazo zitapatikana kisiwani Pemba, tumejionea jinsi utajiri uliopo hapa, katika kuenzi utamaduni, kisiwa cha Kojani wamejitahidi sana bado ule msukumo namna gani, utakua wa kivutio na kua fursa katika jamiii,''alieleza.
"Ni tamasha la kwanza hili, lakini limeakisi yale kuliyoyatarajiwa kuyafikisha katika jamiii, kua ipo haja ya kuenzi utamaduni wetu, kwani ni wa kipekee ambao tunao na kuendelea kuwa nao.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib amesema jamii, ipo haja ya kuunga mkono juhudi za serikali, katika kuikumbusha jamiii juu ya kuenzi mila, silka, asili ya watu wa Pemba, kwa kuandaa matamasha mbali mbali.
"Tumeona kwa sasa, jamii ilivyo na mporomoko wa madili, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu anathamini utamaduni wake, ili kuwa wa upekee, kujivunia juuu ya utamaduni huo.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Rahimu Mohamed Bhaloo, alieleza kua serrkali kwa sasa imekua kwa kasi kikubwa, katika sekta ya utalii, kwa kuona zaidi ya wageni 600,000 wanaitembelea Zanzibar.
"Tunaona jitihada mbali mbali katika sekta ya utalii, zinachukuliwa ili kuhamasisha wageni na wenyeji kujionea utalii wetu wa Zanzibar, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuunga mkono, jitihada hizo ili tuweze kupata maendeleo katika nchi yetu.
Afisa Mdhamin Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Zuhura Mgeni Othaman, amewashukuru viongozi mbali mbali na wananchi, katika kumuunga mkono kwa kuandaa matamasha, ambayo yataikumbusha jamiii, pamoja na kuwavutia wageni kufika katika kisiwa cha Pemba.
Aidha ameyahidi kuyafanyia kazi yote ambayo wameagizwa na serikali, ili kuhakikisha sekta ya utalii, inazidi kuleta maendeleo na mchango mkubwa, katika kuingiza na kukuza pato la nchi.
Tamasha hilo la mswahili wa kipemba, lilianza kwa matembezi yake kwa shughuli kadhaa, ikiwemo gari za ng'ombe na mitindo mbali mbali ambayo yanalengo la kuenzi utamaduni wa kipemba.
mwisho
Comments
Post a Comment