Skip to main content

KAMPUNI YA ‘FOREVER LIVING PRODUCTS INTERNATIONAL’ YATUA PEMBA

 

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANANCHI kisiwani Pemba, wameshauriwa kutumia virutubisho lishe, vinywaji na bidhaa kadhaa zinazozalishwa kwa mti wa Mshubiri, ili kuboresha afya zao, ikiwemo kupunguza takamwili zilizozidi.

Ushauri huo umetolewa na Msambazaji huru wa kampuni ya Forever Living Products International, Imani Lushino, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu uwepo wa wasambazaji huru wa bidhaa hizo kisiwani Pemba.

Alisema, kwa zaidi ya miaka  2000 mmea wa mshubiri umekua na manufaa mengi ndani na nje ya mwili wa binadamu na kuwa bidhaa kama mafuta na virutubisho lishe zinazolishwa kupitia mti huo zina msaada mkubwa kuboresha afya.

Alisema, kwa miaka hii na kwa aina ya vyakula watu wanavyokula bila ya kuzingatia lishe bora, kumesababisha kiwango cha magonjwa hasa yasiyoambukizwa kuzidi kuongezeka kutokana na Kinga ya mwili kupungua inapokosa lishe bora iliyosheheni virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili,

Alieleza kuwa, tayari kampuni hiyo na bidhaa zake, zimeshasambaa zaidi ya mataifa160 duniani Tanzania ikiwemo, na imekuwa na mafanikio makubwa.





Msambazaji huru huyo alifafanua kuwa, hupendelea zaidi kabla ya mtu kuanza kutumia bidhaa hizo au anataka kufanyabiashara, kupewa elimu kwanza.

‘’Kampuni yetu pamoja na umaarufu wake hasa kwenye eneo la virutubisho lishe na biashara, suala la elimu ndio ambalo linapewa kipaumbele,’’alifafanua.

Hata hivyo, alisema wapo wananchi kadhaa kisiwani Pemba, sasa wanaendesha maisha yao, baada ya kujiunga na kampuni hiyo na kusambaaza bidhaa zao.

‘’Kwa mfano hapa Chake chake eneo la Wawi, yupo mwananchi, Bi. Nunu Issa Juma ambaye alishaanza kuwa Msambazaji mwaka mmoja sasa, amejiunga na sisi na kazi yake, ni kusambaaza virutubisho lishe, mafuta, sabuni na vinywaji vinavyotokana na mti huu, na sasa anatengeneza Kipato kizuri Kwa muda wake wa ziada pamoja na kuendelea na shughuli zake zingine,’’alifafanua.


Katika hatua nyingine, alisema wanampango wa kukutana na makundi ya wanavyuo, watumishi wa umma, wanamazoezi na makundi mingine ya kijamii, ili kuitambulisha kampuni hiyo na bidhaa zake.
Wakati huo huo, akizungumza na wananchi wa shehia ya Mgogoni wilaya ya Chake chake, Msambazaji huyo wa bidhaa za kampuni ya Forever Living Products International Imani Lushino, aliwataka kujiwekea mpango mzuri wa lishe bora.



‘’Jiepusheni sana na kula mafuta kupita kiwango, sukari, vyakula vya makopo kwani huchangia ongezeko la magonjwa sugu,’’ alieleza.

Mmoja wa wananchi aliyepata elimu hiyo Raie Hamad Abdalla, alisema bidhaa hizo zinaonekana na faida nyingi, ikiwemo kupunguza takamwili zilizozidi mwilini.

‘’Inaonekana kwa aina ya vyakula tunavyokula kila siku, takamwili huwa nyingi mwilini kuliko lishe inayobakia, sasa ni vizuri  kupata virutubisho lishe na bidhaa za mshubiri Ili kuongezea lishe inayopungua,’’alisema.


Zuwena Hamad Ali, alisema kwa sasa ameanza kutumia bidhaa kama mafuta kwa ajili ya kuondoa harara na ameanza kusafika pia na virutubisho lishe kwa ajili ya kuboresha Afya ya maungio na magoti, sasa nimeanza kupata ahuweni kubwa, maana nilikuwa nimeangaika na bado magoti yanauma, virutubisho vimenisaidia kurudisha ute ute katikati ya maungio na Sasa naendelea vizuri,’’alieleza.

Kwa upande wake Mohamed Khamis alisema, ana nia ya kuwa mfanyabiashara wa bidhaa hizo, kwani watu wengi wanakabiliwa na changamoto za kiafya.

Kampuni hii ambayo imesambaa nchi zaidi ya 160 duniani ikiwemo Tanzania na nchi jirani, ina zaidi ya wasambazaji wa bidhaa zaidi milioni 10 ulimwenguni.

 
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1978 huko Scottsdale, Arizona, ni kampuni inayoongoza kwa utengenezaji na usambazaji wa bidhaa za Mshubiri duniani kote.


Mwanzilishi wa bidhaa za kampuni ya Forever Living, Rex Maughan, aliona faida ya kiafya ya mmea wa Mshubiri, na kuamua kuanzisha biashara inayojihusisha na matumizi ya mti huo.


Miongoni mwa bidhaa wanazouza ni vinywaji vya juisi ya Mshubiri, mafuta kwa ajili ya afya, vipodozi na virutubisho vya lishe kwa afya, kwasasa unaweza kupata maelekezo zaidi namna ya kupata bidhaa na virutubisho lishe kutoka kwenye Kampuni ya Forever Living Products na maelekezo kuhusu kuwa mdau wa Kampuni ya Forever  Kwa kuwasiliana na Msambazaji huru huyo Mr. Imani Lushino Kwa nambari 0719131013 ambaye kwasasa yupo kisiwani Pemba.
 Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo ni vy

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan