NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya wazalishaji karafuu Zanzibar, 'ZACPO' Abuubakar Mohamed Ali, amewataka wakulima wa zao la mikarafuu, kuungana kwa pamoja katika jumuiya hiyo, ili kulitanua zao kuu la karafuu.
Aliyasema hayo Augost 25 ,2024 wakati alipokua na wakulima na wanachama wao, wa mikoa miwili ya Pemba, katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi, wilaya ya Chake chake, Pemba, kwenye mkutano wa kukumbushana majukumu.
Alieleza kua, wakulima wote kisiwani Pemba ni vyema katika kushirikiana na ZACPO, ili kua kitu kimoja na kuweza kutengeza sauti ya pamoja, amabayo itaweza kusikika kwa kila upande, ili wananchi wahamasike zaidi katika upandaji wa mikarafu na kuiepusha kutoweka.
Aidha Katibu huyo Mtendaji, alisema jumuiya hiyo imeundwa kwa lengo ni kuanzisha mfuko, ambao utaweza kuwasaidia wale wote wanaoshughulika na ukulima wa zao la karafuu, wakiwemo wanaolima, wakodishwaji, wakodishaji pamoja na wale ambao wanasaidia kwanamna moja ama nyingine,
Hata hivyo alisema kua jumuiya, imekabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, ukosefu wa jengo la ofisi yao ambalo lingesaidia kufanyakazi zao kwa ufanisi.
''Tunakuwa tunahama na kuhamia kile eneo, kutokana na ukosefu wa jengo letu maalum la kuendeshea shughuli za jumuiya ambayo kwa kiasi kikubwa, inasaidia kukuza na kulinda zao la taifa,''alieleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti na sera kutoka ZAPCO Sharif Maalim Hamad, aliwataka wakulima kuzichangamkia fursa pale zinapotokezea, ili kuliendeleza zao hilo.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la karafuu, walisema kuwa wapo tayari kushirikiana na ZAPCO hatua kwa hatua, ili kuhakikisha zao hilo halitoweki moja kwa moja kisiwani.
Jumuiya ya wazalishaji karafuu Zanzibar ZAPCO, ambayo ilianzishwa mwaka 2002, ambayo kwa sasa inaowanachama 5,600 moja ya jukumu lake ni kuishauri serikali, katika kulikuza na kuliendeleza zao la karafu kwa maslahi ya wananchi na taifa.
MWISHO
Comments
Post a Comment