HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MTANDAO
wa simu za mkononi wa Tigo-Zantel, umechangia shilingia milion 350, kwenye
mfuko wa fidia kwa ajili ya wananchi wanaopatwa na hasara ya kuanguka mkarafuu,
wakati wanapoliokoa zao hilo.
Hafla ya
kukabidhi fedha hizo, kupitia mfano wa hundi, lilifanyika leo Augost 27, 2024
ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake Pemba, kwenye hafla pia ya
kuwakabidhi zawadi wakulima bora wa karafuu, waliokubali fedha zao za malipo kupitia
Tigo pesa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi mfano huo wa hundi, Mkurugenzi wa mtandao wa simu wa
Tigo- Zantel Aziz Said Ali, alisema huo ni mwanzo kwa Tigo-Zantel, kuwachangia
wanoanguka mikarafuu.
Alieleza kuwa,
mtandao wa simu, kila siku umekuwa ukijali mno ubinaadamu na maendeleo yao, na
ndio maana, wamevutika mno kutoa shilingi milioni 350, kwa ajili ya kuutunisha
mfuko huo.
Aidha, mtandao
huo wa simu katika hafla hiyo, iliwakabidhi wakulima 25 zawadi za simu, baiskeli
na piki piki, kwa baadhi yao waliopokelea fedha za mauzo ya karafuu kwa njia ya
Tigo pesa.
‘’Hawa
wakulima 25, kati yao watatu wamekabidhiwa baiskeli mpya na wawili ambao ni
washindi wamekabidhiwa piki piki na wengine wamekabidhi simu janja,’’alifafanua.
Hata hivyo
Mkurugenzi huyo wa Tigo-Zantel, alisema watalifanyia kazi ombi la Waziri wa
Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaaban, wa kuweka zawadi ya gari
kwa washindi, kwa msimu ujao.
Mapema Waziri
huyo, alipongeza hatua ya Tigo-Zantel, moja kuwatunuku zawadi wakulima hao 25,
na kisha kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 350, kwa ajili ya mfuko
wa fidia kwa wanaoanguka mikarafuu.
''Niwaagize
wenzetu wa ‘ZSTC’ kufanya mazungumzo na Benki ya watu wa Zanzibar ‘PBZ’, nao
kuiga mfano wa Tigo-Zantel kwa kuuchangia mfuko huu,’’alieleza.
Eneo jingine,
Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kuwashawishi wakulima, kuacha kiliasfirisha
nje ya nchi, kwa njia ya magendo zao la karafuu, na badala yake wakimbilie ‘ZSTC’
kwa kuliuza.
‘’Kwa wananchi
wanaotaka kulisafirisha zao la karafuu, waje ZSTC kununua, na watapewa vibali
maalum, ambavyo kisha watakuwa huru kulisafirisha watakapo,’’alifafanua.
Hata hivyo
Waziri huyo, aliwataka wakulima hao, kuendelea kupokelea fedha zao za malipo ya
karafuu, kwa mtandao wa tigo pesa, kwani salama zaidi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ‘ZSTC’ Soud Said
Ali, alisema wameshajipanga kwa msimu huu wa mwaka 2024/2025 kuzinunua karafuu
kwa mfumo wa kisasa.
‘’Mkulima
sasa atakuwa anaona karafuu zake zinavyopimwa, atapokea idadi ya kilo, daraja
na fedha zake za kuuzia hata kabla hajatoka ndani ya kituo cha mauzo,’’alieleza.
Akiwasilisha
mfumo huo, Mkuu wa ‘TEHAMA’ kutoka ‘ZSTC’ Najma Nuhu, alisema hatua ambazo
mkulima atazipitia kabla ya kupokea malipo yake ni tano, katika mfumo huo wa
kisasa.
‘’Kwanza ni
usajili, ambao utathibitishwa na cheti, kupewa daraja la karafuu zake, hatua ya
tatu ni kuchungwa, upimaji na hatua ya tano ni kupokea malipo kupitia ujumbe
mfupi wa simu yake,’’alifafanua.
Hata hivyo,
alisema mchakato huo wote, kwa muuzaji mmoja wa karafuu, hautarajiwi kumaliza dakika
moja, kuanzia usajili hadi kupokea ujumbe wa malipo yake.
Badhi ya
wanufaika wa zawadi hizo, akiwemo Hamad Khalid Hamad, aliyeshinda piki piki,
alisema amefurahishwa na mpango huo wa Tigo-Zanztel, kwani sasa ana uhakika wa
safari.
Nae Kombo
Ali Mussa, aliyepata zawadi ya baiskeli, alisema hakuamini kuwa, engewa
miongoni mwa washindi, kwani alikuwa anapokelea malipo yake kupitia tigop pesa,
bila ya kushindana na mtu.
Mwisho
Comments
Post a Comment