NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
ALIYEKUWA
Mratibu wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’
Mohamed Hassan Abdalla, amechaguliwa kwa kura za ndio, kushika nafasi ya
Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo, iliyokuwa wazi.
Mahamed
Hassan, ambae hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo mdogo na wa dharura,
alijizolea kura 15 kati ya kura zote 17 zizopigwa na wanachama wa CHAPO.
Akitoa matokeo
hayo leo Augost 31, 2024, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya 'CHAPO' Hafidh Abdi Said,
alisema wapiga kura wote, walitarajiwa wewe 23, ingawa hadi muda wa kupiga kura
unafika kulikuwa na wajumbe 17 pekee.
Alieleza kuwa,
kwa mujibu wa katiba ya CHAPO, imeanisha idadi ya wajumbe wote, ni kufikia nusu,
ili kufanya uamuzi iwe wa uchaguzi ama kupitisha ajenda.
‘’Idadi ya
wanachama hai 17, kati ya 23 haijakikua katiba ya 'CHAPO' na ndio maana, tumefanya
zoezi la uchaguzi na mshindi ambae ni Mohamed Hassan Aballa, kwa nafasi ya
Mkurugenzi ameshinda,’’alifafanua.
Katika hatua
nyingine, Makamu huyo Mwenyemiti wa kamati ya uchaguzi, alisema kati ya wapiga
kura wote 17, kwa bahati nzuri hakuna hata kura moja, iliyoharibika.
‘’Kabla ya kumtangaaza
mshindi wetu, niwapongeze wanaCHAPO kwa kuendesha zoezi la upigaji kura, bila ya
kuwepo hata kura moja iliyoharibiki,’’alieleza.
Mapema kabla
ya kuanza kwa uchaguzi huo, Makamu huyo Mwenyekiti, aliwataka wapiga kura na
utulivu wa hali ya juu, ili kulikamilisha zoezi hilo, kwa amani.
Akizungumza
mara baada ya kupatikana kwa Mkurugenzi huyo mpya, Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ‘CHAPO’
Zuwena Hamad Ali, alimtaka Mkurugenzi huyo, kuondoa mipasuko ndani ya Jumuiya.
‘’Sasa uchaguzi
umekwisha, hakuna haja tena ya mipasuko, makundi na kilichombele yako, ni
kuwaunganisha wanajumuiya, ili kazi iendelee,’’alieleza.
Aidha Mjumbe
huyo wa bodi, alisema hawatofurahishwa kusikia wapo wasaidizi wa sheria ni wa
wavivu, hawapendi ushirikiano kwani, mwisho wake ni kuidhoofisha CHAPO.
‘’Tujitahidi
sana, kwani malalamiko sio silaha ya kufikia mwafaka, bali watu wafanye kazi,
kisha changamoto ndio njia ya kuelekea mafanikio,’’alieleza.
Kwa upande
wake Mkurugenzi fedha wa ‘CHAPO’ Riziki Hamad Ali, alisisitiza haja kwa
wanachama hao, kupita kila wakati ofisini hapo, na sio kwa ajili ya mikutano
pekee.
Mwanachama
wa ‘CHAPO’ Mashavu Juma Mabrouk, alisema njia ya kufikia malengo yao, ni
kushrikiana na uongozi mzima wa CHAPO, kwa kila hatua.
Nae Ali
Salim, alisema kilichopo mbele ya wanachama wa CHAPO kwa sasa, ni kuongeza
juhudi za kazi, ili wananchi wasione tofauti, kati ya alipokuwepo Mkurugenzi aliyepita na
sasa.
Msaidizi wa
sheria Khadija Said Khalfan, alimtaka Mkurugenzi huyo mpya, kuwaunganisha watu
wote, ili iwe rahisi kufanikisha mipango na mikakati yao.
Comments
Post a Comment