Skip to main content

KATIBU MKUU ABEIDA AWAPA USIA NZITO WATOTO WA KIKE WENYE ULEMAVU




 Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah amewataka Watoto wakike wenye ulemavu kutoona hali hiyo kwamba ni kikwazo cha kutosoma  na kukatisha  ndoto zao za Maisha.

Akizungumza katika uzinduzi wa vyoo rafiki vya Watoto wa kike wenye ulemavu uliyofanyika leo katika skuli ya Sekondari ya Jangwani Dar Es Salaam, hafla hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, amesema anaelewa changamoto zinazowakabili wasichana hao lakini hawatakiwi kukataa tamaa katika kutafuta elimu ili wawe viongozi wa baadae.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinazungumza masuala ya watu wenye ulemavu kwenye vyombo vya maamuzi ili kuhakikisha watu wenye ulemavu hawajaachwa nyuma.

Amesema Tanzania ni nchi moja wapo  ambayo inatekeleza mingozo mbali mbali inazungumzia  masuala ya watu wenye ulemavu ikiwemo UN Covection on the right of People with disability pia kunasheria  ya Tanzania Bara ya mwaka 2010 na kwa upande wa Zanzibar kuna sheria namba  9 ya mwaka 2006 ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka jana, sheria zote hizo zinazungumzia wajibu wa utambuzi wa haki kwa watu wenye ulemavu, usawa na kutokubaguliwa, kukuza uelewa, n.k.

Aidha Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa walimu wote katika skuli mbali mbali kuweka vyoo rafiki kwa Watoto wenye ulemavu, na sio vyoo tuu hata njia ili mazingira nayo yawe rafiki na kuwa na amani.




Naye Mkurugezi  wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, Sofia Mbeyela amesema ujenzi wa mradi wa vyoo rafiki kwa Watoto wa kike wenye ulemavu umeanza Julai mwaka jana na umegharibu milioni 20,000 kwa ujenzi wa vyoo vine na chumba kimoja kwaajili ya walengwa hao kubadili nguo wakati wakiwa katika siku zao za hedhi.

Aidha amewashukuru wadau wote waliyojitokeza kwa hali na mali katika kuchangia ujenzi huo  kwani hapo awali skuli hiyo ilikuwa na vyoo rafiki vitatu huku wanafunzi wakiwa 110, hali ambayo ilionesha hatari kwa Maisha yao.

Alieleza kwamba mradi huo utaendelea kwa skuli zote hivyo amewaomba wananchi, viongozi, mashirika/taasisi za umma na Serikali kuendelea kuchangia ili kuwaondolea Watoto wenye ulemavu changamoto hiyo.

Kwa upande wa wanafunzi wenye ulemavu, akizungumza Zulfa Swaleh mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Skuli ya Jangwani amesema amefarajika na ujenzi wa vyoo hivyo lakini pia amewaomba wananchi kujitokeza kuwasaidia madaftari na vitavu kwani wengi wao ni Watoto wa familia zenye kipato cha chini.

 


Mkurugezi  wa Taasisi ya Maisha ya Amani kwa watu wenye ulemavu, Sofia Mbeyela  na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Abeida Rashid Abdallah ni watu mweney ulemavu hivyo wanaelewa changamoto zinazowakabili Watoto wenye ulemavu na wataendelea kupambana ili kuhakikisha watu wenye ulemavu hawajaachwa nyuma kama sheria na miongozo ilivyoelekeza.

 

Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch