NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
MWENYEKITI
wa Umoja wa Wanawake Tanzania ‘UWT’ taifa Mery Pius Chatanda, amesema aina ya
Mbunge wa viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, katika kuwakomboa
wanawake kiuchumi, ndio mfano unaofaa kuigwa, na wabunge wengine Tanzania.
Alisema,
Mbunge huyo ameendelea kutekeleza kwa vitendo maagizo ya UWT taifa, ya
kuwakomboa wanawake kiuchumi, kufuatia kukabidhi mashine ya kuzalisha mikate na
tosi na fedha taslim, kwa wanawake wa mkoa wake, yenye thamani ya shilingi million
10.5
Mwenyekiti
huyo wa UWT taifa, aliyasema hayo leo Oktoba 25, 2023, Micheweni mara baada ya kukabidhi mashine
hiyo, kuweke jiwe la msingi ofisi ya ushoni wa nguo na kukabidhi shilingi milioni
1, zilizotolewa na Mbunge huyo.
Alieleza kuwa,
anaamini kupitia uwekezaji wa Mbunge huyo, wanawake wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba,
watapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, kupitia njia ya kujiinua kiuchumi.
Alifahamisha
kuwa, wakati umefika kwa wabunge wengine wa mikoa ya Tanzania, kufuata nyao za
utekelezaji wa Ilani, kama alivyofanywa Mbunge wa viti maalum, mkoa wa
kaskazini Pemba.
‘’Kwa hakika
Mbunge wetu huyu wa mkoa wa kaskazini Pemba Asya Sharif Omar, ametekeleza kwa
vitendo, dhana ya kuwakomboa wanawake kiuchumi, kwani uwekezaji aliyoufanya,
umenifurahisha mno,’’alieleza.
Aidha Mwenyekiti
huyo wa UWT taifa Mery Pius Chatanda, alisema, Mbunge Asiya Sharif, ni aina ya
wabunge wachache Tanzania, wanaotekeleza kwa vitendo, yale waliowaahidi
wananchi.
Katika hatua
nyingine, amwataka wanawake wa CCM mkoani humo, kuzienzi mashine hizo na ziende
moja kwa moja, kuwanufaisha na kupunguza ukali wa umaskini wa kipato.
Alieleza kuwa,
hataki kusikia, misuguano, malumbano na ugomvi kupitia uwekezaji huo mkubwa, na
badala yake wafanyake kazi, kwa ushirikiano.
Wakati huo
huo Mwenyekiti huyo wa UWT taifa, amemtaka Mbunge huyo, kuendelea na kasi yake
hiyo, kwani bado wanawake waliowengi, wanakabiliwa na hali ngumu ya kipato.
‘’Mbunge wetu
Asya Sharif, endelea kuwakomboa wanawake kiuchumi, ili ile dhana ya wanawake
jeshi kubwa, izae matunda kwa kujiongezea kipato,’’alieleza.
Akizungumza kabla
ya kukabidhi mashine hizo, Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba, Asya
Sharif Omar, alisema, ameamua kuyafanya hayo, ili wanawake wanachama wa UWT wainuke
kiuchumi.
Alieleza kuwa,
kwa vile aliaminiwa kwa kushika nafasi hiyo, hana budi, kurejesha imani ya
kweli kwa wananchi, kwa njia ya kuwaekeza miradi mikubwa na yenye tija kwao.
Alifahamisha
kuwa, UWT daima imekuwa ikiwahimiza wao wabunge mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi,
kurudi kwa wananchi, katika kufikishia miradi mikubwa.
‘’Mheshimiwa
Mwenyekiti, huu sio mwanzo, nimeshachangia na kutoa vifaa mbali mbali vya
ujenzi, katika ofisi na matawi yetu ya UWT na CCM, kama njia ya kurejesha imani,
kwa wananchi,’’alifafanua.
Hata hivyo,
Mbunge huyo alisema amechangia shilingi milioni 1, kwa ajili ya uunganishaji
huduma ya umeme na ununuzi wa mafeni, kwenye kituo cha ushoni cha UWT kilichopo
Micheweni.
Mapema Mbunge
huyo, aliwataka wanafunzi wanawake wa skuli ya sekondari ya Chasasa Wete, kusoma
kwa bidi, ili kufikia malengo waliojiwekea.
Akizungumza na
wanafunzi hao, mara baada ya kukabidhi mchele paketi tano, taula za kike boksi
10, soda boksi 10 na sukari paketi moja vyenye thamani ya shilingi million 1.3,
alisema kila mmoja, kwa vile amejiwekea malengo, hana budi kuyafikia.
Hata hivyo, amewataka wanafunzi hao, kuendelea kujilinda na kutoa taarifa, wanapoona viashiria vya udhalilishaji dhidi yao, kutoka kwa mtu yeyote.
Kwa upande
wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Riziki
Pemba Juma amempongeza Mbunge huyo, kwa uamuzi wake, wa kuwasaidia chakula wanafunzi
hao.
Alisema,
alichokifanya ni njia moja wapo ya kuwaweka mazingira mazuri wanafunzi hao,
kwani suala la chakula na taula za kike, ni mambo muhimu kwao.
‘’Hizi taula
zikikosekana, mwanafunzi wa kike huanza kujiskia aibu na wakati mwingine,
anaweza kukatisha masomo japo kipindi kimoja au zaidi,’’alieleza.
Mwisho
Comments
Post a Comment