NA MARYAM
NASSOR, PEMBA@@@@ KAMATI zilizomo kwenye shehia zimetakiwa
kushuka kwa wananchi na kuibua matatizo
yanayowakabili ili kuyapatia ufumbuzi unaofaa.
Kauli hiyo, imetolewa na Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia inayoshughulika
na Mazingira, Utetezi wa Kijinsia Pemba (PEGAO)
Hafidh Abdi Said katika mafunzo ya kuwapatia uwezo wajumbe wa Kamati hizo
kutoka wilaya nne kisiwani Pemba.
Alisema, iwapo kamati hizo zilizoundwa zitashuka chini kwenye jamii kutafuta matatizo
yanayowakabili wananchi na kushirikiana na viongozi kuzitatua, shida nyingi
zitapungua.
‘’Kamati hizi zinatakiwa kuwa karibu na wananchi ili kuibua changamoto
zinazoikumba jamii na kuzifikisha kwa viongozi husika kupatiwa ufumbuzi,’’
alisema.
Aidha alisema kuwa, Serikali haiwezi kujua yote yanayoikumba jamii,
hivyo watakapoyaibua na kuyapeleka kwa viongozi yatafanyiwa kazi kwa haraka.
Nae, muwezeshaji katika mafunzo hayo Habibu Ali Khamis alisema, mpango
wa kuchochea maendeleo katika jamii ni suala la wote, hivyo wanatakiwa kuwa
tayari na kujitolea ili kuwasaidia wananchi.
Alisema, Kamati hizo zinatakiwa kutafuta chanzo cha tatizo na kufanya
upembuzi wa kina na kupata mbinu haraka za kutafuta suluhisho.
Alieleza kuwa, jamii inakumbwa na shida nyingi ikiwemo utoro wa
wanafunzi mashuleni, pamoja na janga la udhalilishaji.
Aidha alisema, Kamati hizo zinatakiwa kukubalika ndani ya jamii ili iwe
rahisi kwao kupata ushirikiano unaohitajika.
Mmoja wa wajumbe hao alisema, jamii bado haiko tayari kushirikiana
katika malezi, hivyo ni ngumu kufanikisha yote kwa haraka.
Aliwataka wananchi kushirikiana pamoja na Kamati za shehia, ili
kufanikisha malengo yao wanayojiwekea.
MWISHO.
Comments
Post a Comment