Na Nafda Hindi, Zanzibar @@@@
Uwepo wa mradi wa VIUNGO, mbogamboga na matunda Zanzibar umesaidia wananchi kujikita katika sekta ya kilimo hali iliyoleta mapinduzi ya kiuchumi
katika familia zao.
Hayo yamebainishwa na wanufaika wa mradi huo mara baada ya
kutembelewa na Kikosi Kazi cha ufundi kwa Taasisi zinazotekeleza mradi huo
kwa lengo la kugunduwa Mafanikio pamoja na changamoto zinazowakabili wakulima
na kuzitafutia ufumbuzi.
Wamesena kuna mafanikio waliyoyapata kupitia kilimo ikiwemo
kuimarisha Afya za familia kwa lishe bora kwa kula mboga mboga na kuongeza
kipato kupitia mfumo wa biashara.
Ali Shauri ni katibu wa uhirika wa kilimo hai kiitwacho
TUMAINI LA KIJANI uliopo Chuini Zanzibar, amesema wao wanatengeneza bustani za
nyumbani ambazo zinajumuisha mbogamgoga pamoja na mimea ya dawa lengo likiwa
kukibadilisha kijiji kuwa cha kijani na
wananchi kurudi katika uasili wa kutumia dawa za mitishamba jambo linalotoweka
kwa vizazi vijavyo.
Amesema sababu
zilizowapelekea kujiingiza katika kilimo hicho ni kuona jamii inakuwa na afya
bora kwa kutumia vyakula wanavyovizalisha wenyewe kupitia kilimo hicho sambamba
na kupunguza matumizi ya fedha.
“Sababu ambazo zimetufanya kuingia katika kilimo hichi ni
kuzingatia suala ziama la afya bora kwa jamii kwa kutumia chakula
walichokizalisha wenyewe ambacho ni salama ukizingatia kimezalishwa kwa kutumia
teknolojia ya kilimo hai” amesema Ali Shauri
Amesema jamii ya kijiji hicho imeanza kuelewa dhamira ya
kilimo hai katika kupunguza matumizi ya fedha na sasa wameondoa dhana ya kuliba
bustani za maua na kuanza kulima bustani za mbogamboga.
“kabla hatujaanza mradi huu kulikuwa kuna watu wameweka
bustani za maua lakini baada ya kuuelezea mradi huu katika kijiji chetu wenyi wamepunguza maua na kuanza kulima
kilimo cha mbogamboga” Ameongezea
Akiyataja moja ya mafanikio waliyoyapata kupitia kilimo
hicho amesema kwa sasa kumekuwa na uhakika ya upatikanaji wa chukula kwenye
familia zinazojishughulisha na kilimo hicho.
“Familia zimeanza kuhakikisha upatikanaji wa chakula chao
pamoja na kupunguza gharama za matumizi ya mbogamboga” Aliendelea kufafanua
Kwa upande wake Bi. Aviwe Ali Songoro ambaye
anajishughulisha na kilimo cha Vanila, Migomba, Pensheni na viungo vingine
amesema awali alikuwa akijishughulisha na kilimo cha pilipili lakini mwanga
kwake ulianza kung’aa baada ya kunufaika na mradi wa Viungo mboga na Matunda
chini ya programu ya Agri-Connect.
“Nilianza kulima pilipili lakini baada ya kukutana na
maafisa wa mradi wa VIUNGO, mbogamboga na matunda wakanipatia mafunzo nilianza
kujibadilisha na kuingia kwenye mazao mengine” Amesema Bi. Aviwe
Amesema alianza na ukulima wa vanila akiwa na mashina 200,
uwezeshi wa mradio huo kwa kumpatia mbegu kwa sasa ana mashina 1,000 na tayar
yameshaanza kutoa maua huku kwa upande wa migomba kwasasa anamiliki mashina
2,800.
“Nilianza na mashina 200 ya vanila ila mradi umeniwezesha na
kwa sasa nina mashima 1,000 ambayo tayari imeshatoa Maua” Aliongezea
Amesema amekuwa na mafanikio makubwa kupitia shughuli zake
hizo za kilimo ambapo zinamsaidia kuendeshea maisha yake ikiwemo suala zima la
mahitaji yake ya msingi pamoja na kuwasomesha watoto wake.
“Kwsasa nina uhakika wa mahitaji yangu na hivi sasa
nawasomesha watoto wangu mmoja akiwa yupo Chuo Kikuu na namlipia kila kitu”
Alisisitiza
Kama inavyofahamika kila penye mafanikio hapakosi changamoto
ndio ilivyo pia kwa Bi. Aviwe ambapo yeye amesema uhaba wa maji wa kumwagilia
mazao yake imekuwa ndioo kikwazo kikubwa kwake.
Akizungumza kwa niaba ya
Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji Mali Asili na Mifugo Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Pemba Muhandisi, Idriss Hassan
Abdulla amepongeza juhudi zinazofanywa kwa pamoja na watekelezaji wa mradi wa
viungo Zanzibar na ameahidi kuwa Wizara itaendelea kutoa mashirikiano ya kina
ili kuona lengo la kuwawezesha wananchi kwenye kilimo linafikiwa.
“Tumeona umuhimu wa sisi Wizara kuwa na ushirikiano na
washirika hawa wa miradi na tumejiridhisha kuwa ni kazi nzuri ambayo inalenga
kutoa ajira pamoja na kuimarisha lishe bora kwa wananchi” Alisema Afisa huyo
Nae Meneja Mkuu wa Mradi wa VIUNGO, Simon Makobe amesema
wamefurahishwa kuona yale ambayo walikuwa wakiwafundisha wakulima hao wamekuwa
wakiyazingatia na kuyafanyia kazi hali iliyoleta mabadiliko kutoka walipokuwa
na walipo sasa.
“Tumefurahishwa kuona wakulima wameanza kuwa na mabadiliko
kwenye utekelezaji wao mafanikio yameanza kuonekana hasa kwa akina mama”
Amesema Simon Makobe
Vicent Akulumbuka kutoka timu wa washauri mradi wa VIUNGO Wizara ya Kilimo Tanzania Bara kutoka Dodoma
amesema katika mradi huo wako katika hatua ya kujitathmini na kuangalia
maendeleo ya mradi na changamoto zinazowkabili wakulima ili kuzipatia ufumbuzi.
“Tumeona wakulima wanajisaidia wenyewe kupata masoko lakini
ikitokea kuna changamoto ya masoko sisi ndio kazi yetu kutatua changamoto
hiyo” Amesem Akulumbuka
Ziara hiyo imejumuisha
Ushirika wa kilimo cha bustani
(TUMAINI LA KIJANI) kilichopo Chuini, Wilaya ya Magharibi “A”, Mkulima
wa zao la Vanila Kizimbani na Kiwanda cha Uchakataji na Usindikaji wa Viungo
unaozalisha kiungo cha majani ya chai
(ZANZIBAR ORGANIC PROCESSOR) kilichopo Amani viwanda vidogo vidogo Mkoa wa
Mjini Magharibi.
Mradi hua wa Viugmgo unaotekelezwa kwa pamoja na TAMWA, People Developmend Forum (PDF) na Community
Forest in Pemba (CFP) unadhaminiwa na Jumuiya ya Umija wa Ulaya.
Comments
Post a Comment