ZANZIBAR
Wizara ya Elimu imeombwa kuhamasisha na kutoa elimu ya
kilimo cha mboga mboga mashuleni kwa lengo la kuboresha lishe bora kwa
wanafunzi.
Wakizungumza katika kaikao cha pamoja huko hoteli ya SEA
CLIFF Mangapwani kilichowashirikisha
watendaji Sitini na tano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichajadili mafanikio na changamoto
zinazoikabili sekta ya kilimo hasa cha mboga mboga, VIUNGO na matunda na
kutafuta ufumbuzi ili kuleta tija kwa jamii.
Wamesema Wizara ya Elimu ya Zanzibar na Tanzania Bara
washirikiane kwa pamoja kuongeza nguvu kutoa elimu kwa wanafunzi wa kulima
kilimo cha bustani mashuleni kwa lengo la kuimarisha Afya zao kwa kupata lishe
bora na kwa ajili ya maisha yao ya
baadae.
Mapema Mratibu wa mradi wa Agriconnect Zanzibar Omar
Abuubakar Muhammed amesema ipo haja kwa jamii kuhamasishwa juu ya ulaji wa
lishe bora hususan kina baba ambao wanaongooza kupeleka majumbani kwao vyakula
visivyozongatia lishe bora na hatarishi kwa Afya za walaji .
“Tunahamasisha vijana na wanawake kuhusu lishe bora na tumewasahau wanaume ambao wao ndio wapelekaji wakuu wa vyakula visivyokuwa na lishe bora majumbani kwao kama vile chips na vyakula vyengine vya mafuta,” Abuubakar Mohammed, alisema.
Nae Magret Natai Afisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo Dodoma
amesema jambo muhimu katika mradi wa Agriconnect ni kujenga uelewa kwa jamii kuzingatia
ulaji wa chakula unaofaa na lishe bora hasa kwa wanafunzi kwa kuzingatia wao ni
wazazi wa baadae hivyo itarahisisha kupeleka elimu majumbani.
“Wizara ya elimu iweke mipango mikakati ya kuhakikisha shule
zote zina maji ili wajifunze kilimo cha bustani ya mboga mboga na kuwa rahisi
kwao kumwagilia mazao yao,” Magret alisema.
Aidha Mratibu wa masuala ya lishe Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknologia Tanzania Bara Grace Shileringo amesema Wizara ya Elimu imejipamga
kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula chenye virutubisho kwa kuanzisha bustani
za mboga mboga mashuleni.
“Mradi huu wa VIUNGO umefanya kazi nzuri shuleni hasa maeneo
ya school garden kwenye kutoa elimu na kuanzisha club za lishe shuleni, Wizara
tunasisitiza wanafunzi wapate chakula chenye lishe bora na hakiwezi kuletwa na
wazazi isipokuwa kupitia school garden,” Grace alisema.
Afisa Lishe kutoka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Tanzania Bara (TAMISEMI) Asiyatu M’bwambwa amesema kazi kubwa ya Wizara
hiyo ni kutekeleza miongozo na Sera mbali mbali kutoka Wizara husika ili
kuhamasisha na kuzijengea uwezo kamati tekelezaji.
“Sisi kazi yetu kubwa kama Wizara ni kuhamasisha na
kuzijengea uwezo kamati za chini ziweze kuhamasisha upatikanaji wa chakula kwa
kupitia mbinu mbali mbali kama bustani za mashuleni na ufugaji wa wanyama
wadogo wadogo ili wapate chakula bora na kina faida kwao sio kushiba tu hata
kuwafanya wawe imara,” Asiyatu alisema.
Kupitia mradi wa VIUNGO tayari shule kumi na tano kutoka
Zanzibar na mia moja kutoka Tanzania Bara zimepatiwa elimu ya kuelimisha
wanafunzi kulima kilimo cha mboga mboga mashuleni.
Mradi hua wa Viugmgo unaotekelezwa kwa pamoja
na TAMWA, People Developmend Forum (PDF)
na Community Forest in Pemba (CFP) unadhaminiwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.
Comments
Post a Comment