Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makaazi Zanzibar imesema kumekua na uvamizi pamoja na uuzaji
holela wa maeneo ya ardhi ya akiba kitendo ambacho kinachangia ongezeko la
migogoro ya ardhi Zanzibar.
Kauli hiyo imetolewa
jana na waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali
alipokutana na Masheha wa Wilaya ya Kusini Unguja, kikao maalum kilichofanyika
ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo alisema
kumekua na uvamizi na uuzaji holela wa maeneo ya ardhi ya akiba
yaliyotengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Waziri Rahma alisema
Wizara yake itahakikisha inaweka mikakati imara ya udhibiti wa uuzaji ardhi
kiholela hasa katika maeneo ya ardhi ya akiba yaliyotengwa na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Aidha alieleza kwamba
Wilaya ya Kusini Unguja inaongoza kwa uvamizi na uuzaji wa ardhi kiholela hasa katika maeneo ya fukwe za
bahari yiliyopo wazi hivyo kutokana
uwezo wa wizara yake kupewa dhamana ya usimamizi wa ardhi kwa mujibu wa tangazo
la kisheria Nam 137 ya Mwaka 2020 itahakikisha inayadhibiti maeneo hayo.
“ Wilaya ya kusini
Unguja inaongoza kwa uvamizi na uuzaji
wa maeneo kiholela hasa maeneo ya fukwe na yaliyo wazi hivyo kwa vile Wizara yangu ndio iliyopewa
dhamana ya usimamizi wa ardhi kwa mujibu wa sheria nitahakikisha ninayadhibiti
maeneo hayo na atakaebainikia kwenda kinyume hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake” Alisema waziri huyo.
Hivyo Waziri huyo amewataka masheha hao kuunga mkono
juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika usimamizi wa
masuala ya ardhi pamoja na kufanya kazi zao ipasavyo kwa kutojihusiha na
vitendo vya uuzaji wa ardhi bila kufuata sheria zilizowekwa.
Naye Naibu Katibu
Mkuu wa wizara hiyo Mzee Ali Haji alitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya ardhi kwa
wageni ambapo alisema kwa mujibu wa Sheria ya ardhi Nam.12 ya mwaka 1992
imekataza kuuziwa ardhi mgeni yeyote bali atatakiwa kukodishwa kwa ajili ya
uwekezaji na sio vyenginevyo.
Kwa upande Mkurugenzi
Mipango Miji na Vijiji Kutoka Kamisheni ya Ardhi Muchi Juma Ameir alisema
tayari Kamisheni ya Ardhi
imeyaainisha maeneo yote yenye
ardhi ya akiba yaliyoko katika Mkoa wa Kusini Unguja yakiwemo Paje, Muungoni,na
Muyuni kwa lengo la kuyapanga na kuyapima kwa kuyawekea alama na kuyadhibiti ili yasiweze kuvamiwa kwa uuzaji
wa viwanja kiholea .
Kwa upande wa mashe
Shehia ya paje Mohammed Rajabu Makame alisema kuwa kwa kiasi kikubwa wanasheria ndio wanaohusika
na masuala ya ukiukwaji wa sheria kwa kufanya vitendo hivyo na hata wao
kuwakosesha ufanisi mzuri wa kiutendaji hasa katika kazi zao za usheha.
Mapema Mkuu wa Wilaya
ya Kusini Rajab Mkasaba alimkaribisha waziri huyo na kuwataka masheha kuwa
mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa jamii juu ya umiliki wa ardhi katika
shehiya zao.
Kikao hicho
kimefanyika kwa lengo la kujadili na kuweka mipango mikakati ya usimamizi madhubutu ambao utasaidia
kuondoa changamoto ya uuzaji wa ardhi kiholela
pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi nchini.
Mwisho
Comments
Post a Comment