Mashirikiano ya
Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makaazi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) yanatarajiwa kuibua
kasi ya kiutendaji katika sekta ya
ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili wananchi waweze kuzimudu.
Akizungumza Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi (SMZ) Dkt. Mngereza Mzee Miraji
katika kikao cha mashirikiano ya kiutendaji kilichofanyika mwisho wa wiki
iliyopita katika ukumbi wa Wizara
hiyo Maisara Unguja, alisema kupitia
vikao vya mashirikiano baina sekta mbili
hizo vitasaidia katika kuibua kasi ya utendaji hasa katika sekta ya ujenzi wa
nyumba za bei nafuu zenye kukidhi mahitaji ya wananchi wenye kipato tofauti.
Alisema kwamba
kunamafanikio yameanza kuonekana kupitia vikao hivyo ikwemo kukamilika rasimu
mbili ya makubaliano (MOU) zimekamilika kiutendaji ambapo zitarajiwa kusainiwa
katika kikao kijao cha ngazi ya mawaziri wa pande zote mbili wa wizara ya Ardhi
ya SMZ na SMT.
Dkt Mngereza alifafanua
kwamba ‘MOU’ zilizokamilika ikiwemo
ya Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ‘MOU’ inahusu Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makaazi Zanzibar na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makaazi (SMT) ambapo kuna mambo mengi ya ushirikiano wamekubaliana ikiwemo
ngazi ya kitalaamu, kubadilishana uzoefu pamoja na mafunzo kwa watendaji wa
taasisi mbili hizo.
Pia alisema wizara ya
Ardhi ya SMT imepiga hatua zaidi kiutendaji ambapo wanamfumo unayojulikana kwa
jina la Intergreted Land Information System unasaidia kutatua changamoto ya
urasimu pamoja na kuboresha huduma hivyo wizara yake kupitia Idara ya Kamisheni
ya ardhi imeanza maandalizi ya kuwa na
mfumo huyo na wamefika katika hatua nzuri.
Sambamba na hayo Dkt
Mngereza alisema wamekubaliana wawe na mashirikiano ya tafiti katika sekta ya
ardhi na makaazi ya bei nafuu lakini katika kuanzia hilo watakuwa na kamati ya
pamoja (Joint committee) ambayo imeshaingizwa katika mazungumzo ya yanayoendelea
baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na taasisi ya Shelterafrique.
Alifahamisha kwamba
taasisi ya Shelterafrique inautaratibu
wa kutoa mikopo ya bei nafuu kwa nchi wanachama zaidi ya nchi 30 na mwaka huu
wanatarajia kutakua na mkutano pamoja na
maonesho ya teknolojia ya ujenzi wa maakazi ya bei nafuu.
Aidha Dkt Mngereza
alisema wizara yake inakabiliwa na changamoto ya wataalamu wa upimaji ardhi
ndani ya maji (Hydrographic Survey) hivyo wamekubaliana na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ardhi SMZ watakuwa na mpango mkakati wa kuwajengea uwezo watendaji wao ambapo kila wizara italazimika
kuingiza katika bajeti yake.
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi (SMT) Dkt. Allan H.
Kijazi alisema watahakikisha wanaweka misingi imara kwa watanzania wote
kumiliki nyumba za bei nafuu na kuendeleza matumizi ya ardhi bila ya kuangalia
tofauti yoyote.
Alieleza kwamba
matarajio ya kikao hicho ni kuwa na mifumo ya pamoja ya uboreshwaji wa utoaji
huduma kwa viwango vinavyofanana baina ya Taasisi mbili hizo kwa lengo la
kukidhi mahitaji ya Taifa.
Kwa upande wa Mkurugenzi
Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar(ZHC)Mwanaisha Ali Saidi kupitia kikao hicho aliwaahidi wananchi
wategemee mabadiliko katika sekta ya maakaazi nakusemba kwamba Shirika lake limejipanga kimkakati katika
kuhakikisha linatoa huduma ya nyumba bora na salama kwa bei nafuu.
Naye Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Kyando Mchechu alisema Shirika
hilo kwa sasa limejikita zaidi kwenye miradi
ya ujenzi ambapo ndio kipamumbele chake kujenga nyumba katika jiji la
Dar es salaam, Dodoma na maeneo ya miji na nyumba hizo ni za ghoroma na bei
nafuu.
Kwa upande wa
watendaji waliyoshiriki kikao hicho wamezipongeza Serikali zote mbili(SMZ na
SMT) kwa kuagiza kuweko na mashirikiano
ya kiutendaji katika Taasisi ambazo zinalingana kimajukumu na hazimo katika
orodha ya sekta ziliyomo katika Muungano.
Mwisho
Comments
Post a Comment