Skip to main content

TAMWA-ZNZ YATAKA MABADILIKO YA HARAKA SHERIA MPYA YA HABARI

  





 


Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ


Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ) kimesema kuna haja ya taasisi husika za mabadiliko ya sheria kuweka kipaumbele kufanyiwa marekebisho yanayoendana na matakwa ya wadau katika sheria za habari Zanzibar ili zitoe mazingira ya uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yao.

 

Mkurugenzi wa Chama hicho Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa akizungumza na wandishi wa habari katika mkutano wa kuwasilisha ripoti ya sheria za habari Zanzibar zilizofanyiwa mapitio na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na Shirika la INTERNEWS Tanzania ambazo zinakinza uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kujieleza vyombo vya habari alisema uhuru wa habari ni nguzo muhimu katika maendeleo ya taifa.


Alisema uhuru wa habari ni nguzo muhimu inayoweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ukuzaji wa maendeleo kwenye Nchi hivyo inapotokea sheria ya tasnia hiyo kubana ni sawa na kuchelewesha maendeleo ambayo yanahitajika na kila mtu.

 

Alieleza, “lazima tufahamu kwamba uhuru wa habari kwenye Nchi yoyote ni nguzo muhimu inayoweza kusaidia maendeleo  na ndio maana enzi za uhai wake Nelson Mandela alipigania uhuru wa habari katika muda wake wote hususani vyombo binafsi (Private media).’’

 

Akitolea mfano changamoto za sheria hiyo alisema ni pamoja na Sheria namba nane, (27) (i) ya Wakala wa Habari Magazeti na Vitabu ambacho kinaeleza afisa yoyote wa Jeshi la Polisi anaweza kuzuia au kukamata gazeti lolote lile lisichapishwe iwapo atashuku linakwenda kinyume jambo ambalo linakwenda kinyume na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza.


 “Tuna kila sababu ya kuona kwamba Sheria zetu, Sera na matendo yaendane na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa habari ili iweze kuleta maslahi kwa makundi yote,” alieleza Dkt. Mzuri Issa.

 

Aliongeza “tumepitia sheria kumi za habari na katika kufanya mapitio hayo tunasukumwa zaidi na mambo matatu. kama Zanzibar na Tanzania tunapaswa kwendana na mikataba ya kimataifa.”

 

Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo akifafanua zaidi alionesha kusikitishwa kwake na mamlaka mengine ya sheria ambayo inampa uwezo waziri wa habari kufungia chombo chochote cha habari iwapo ataona inakwenda kinyume na matakwa yake.

 

Alieleza kuwa hatua ya kufungia chombo ni jambo kubwa amabalo lisingepaswa kufanywa na waziri badala yake lilipaswa kufanywa na mamlaka nyingine ikiwemo Mahkama.

 

Mapema akiwasilisha ripoti ya mapitio ya sharia za habari, Shifaa Said alisema licha ya juhudi kubwa kuchukuliwa na wadau wa habari kutoa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria mbalimbali lakini bado utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.

 

“Sisi kama wadau tumeshatoa mapendekezo yetu ya kuhitaji mabadiliko ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya tume ya utangazaji ya Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997 na tunaendelea kufanya ushawishi ili tuweze kupata sharia bora zitakazotoa nafasi kwa wandishi na vyombo vya habari kutekeleza majukumu yake kwa uhuru,” ’Shifaa Said Hassan, mdau wa habari.

 

Hivyo aliwataka wandishi wa habari kuendelea kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sharia kwa kuandika mapungufu yaliyopo katika sharia hizo ili ziweze kufanyiwa marekebisho kwa haraka.


Alieleza, “sisi wandishi wa habari tuipigie chapuo sheria za habari zilizofanyiwa mapitio ambazo zinakinza uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa kufanya ushawishi kupitia vyombo vya habari ili hizi sheria ambazo tunahisi zinatatiza uhuru wa habaroi ziweze kufanyiwa marekebisho.”



 

Akichangia ripoti hiyo mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar, Jabiri Idrissa alisema waandishi wa habari Zanzibar wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufanya kazi iwapo siku sheria zilizopo zitafanyiwa kazi ipasavyo.

 

Akitolea mfano kupitia Sheria ya Kinga na Madaraka ya Baraza la Wawakilishi no. 4 ya 2017, Spika anaweza kumuita raia yoyote wa Zanzibar kuhojiwa kwenye kamati za Baraza hilo iwapo ataona amefanya  kosa ambalo limekinzana na sheria za Baraza, huku sheria hiyo ikimzuia alieitwa kwenda na wakili wake wakati wa kuhojiwa. Tunaona kuwa kufanya hivyo ni kumyima haki muhimu ya mtu kujitetea pamoja na kuwa jambo la kuitwa na kuhojiwa lilipaswa kufanywa na Mahkama na sio taasisi nyengine yoyote ile.

 

Nae Khadija Rashid kutoka Redio Jamii Mkoani Pemba alisema kuna haja ya kuongezwa  uhamaishaji zaidi kwa wanahabri juu ya ushawishi wa mabadiliko ya sharia hizo ili kuweka mazingira salama kwa tasnia hiyo.

 

Alisema, “kinachosikitisha zaidi ni kuona idadi kubwa ya  wananchi hawajui sheria zinazowahusu wao wenyewe na kuongezea kuna haja kazi kubwa zaidi kuendelea kufanyika.

 

Nae Rerema Sleiman Nassor alisema wakati wa uchaguzi wanahabari wengi hukutana na mazingira  mgumu licha ya kufanya kazi zao kwa misingi yote ya sheria za tume.

 

Alisema, “mazingira niliokutana nayo sitaweza kusahau maisha yangu yote nilitolewa kituo cha kupigia kura kama sikua na kazi maalumu ya kukusanya habari kwa maslahi ya umma’’alisema.

 

Mkutano huu wa kuwasilisha ripoti ya sheria za habari Zanzibar unakuja kufuatia kufanyika kwa mapitio ya sheria mbalimbali za habari ambayo yamefanywa na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na Shirika la INTERNEWS Tanzania pamoja na wadau wengine wa habari Tanzania.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...