MKUU wa mkoa wa kusini
Pemba Mattar Zahor Massoud, amesema kada ya sheria itaendelea kuwa eneo muhimu
katika jamii.
Alisema, kwa kulitambua hilo Serikali, iliamua kutunga sheria mahusisi ya
msaada wa kisheria nambari 13 ya mwaka 2018, na kuanzishwa Idara ya Katiba na Masada
wa Kisheria, ili kuwafia wananchi kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria.
Alisema idara hiyo imekua ikifanya kazi kubwa katika masuala
mbali mbali ya msada wa kisheria Zanzibar, ili kuona wananchi wasio na uwezo
wanapata haki zao za kisheria.
Mkuu huyo aliyasema
hayo Mei 12, mwaka 2022 wakati akiyafungua mafunzo ya kwanza ya siku 15 kwa
wasaidizi wa sheria 15 wa majimbo yote kisiwani, yanayoendelea Gombani Chake
chake.
Alisema kada ya
wasaidizi wa sheria, inasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafahamisha wananchi hususani wa ngazi za
chini katika jamii, juu ya haki zao za kisheria na namna ya kufuatilia.
“Mafunzo haya ni
muhimu kwenu washiriki, ili mukitoka hapa muweze kwenda kutekeleza majukumu
yenu kwa uweledi na malengo yaliokusudiwa, hizi sheria mutakazofundishwa
mukazifanyie kazi,”alisema.
Kwa upande wa rushwa
alisema matukio mengi yanafanywa katika jamii, wanaoathirika ni wananchi hivyo
wasaidizi wa sheria wanapaswa kwenda kuwafahamisha juu ya suala hilo.
Mkuu huyo aliipongeza
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, skuli ya sheria ya Zanzibar
kwani kuwepo kwa skuli hiyo ni faraja kwenye kada ya sheria nchini.
Kwa upande wake Afisa
Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais katiba sheria utumishi na Utawala bora
Pemba, Halima Khamis Ali, alisema Idara, inajukumu la kusimamia masuala ya
kisheria, hivyo wasaidizi hao wamechaguliwa kwa mahitaji ya jamii husika.
Mapema Mkurugenzi wa
Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanizbar Hanifa Ramadhan Said,
aliishukuru shirika la ‘LSF’ kwa kuendela kuwaunga mkono katika masuala mbali
mbali ya kisheria.
Alisema mchakato wa
kuwapata wasaidizi hao, ulikuwa mkubwa Unguja maombi yalikua zaidi ya 400 kwa
Unguja na wanaohitajika ni wasaidizi 32, ambapo kwa Pemba maombi yalikuwa zaidi
ya 200 wasaidizi wanaohitajika ni 18, hivyo wasaidizi hao wanapaswa kuthamini
nafasi waliopatiwa.
Aidha alisema licha ya
kupatikana kwa wasaidizi 32 Unguja na Pemba 18, lakini bado kunahitajika
wasaidizi wa sheria wengi ili kufikia shehia zote za Zanzibar.
“Kwa sasa tuna shehia
888 ila wasaidizi wa sheria tulionao ni 205 Zanzibar nzima, tuna shehia 141
hazina wasaidizi wa kisheria Unguja 106 na Pemba 35,” alisema.
Naibu Mkuu wa skuli sheria
Zanzibar kitengo cha taaluma Msemo Mavare, aliwataka wasaidizi hao wa sheria
kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo, ili jamii iweze kunufaika juu ya
uwepo wao.
Akitoa neno la
shukurani Mwanasheria kutoka Idara ya Katiba na msaada wa kisheria Zanzibar Ali
Haji, alisema mafunzo hayo ni muhimu sana, kwani jamii iliyokubwa inachangamoto
nyingi juu ya masuala ya kisheria.
Mada kadhaa
zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na dhana ya wasaidizi wa sheria, katiba, sheria,
sheria ya ushahidi, uashauri nasihi, sheria ya mtoto pamoja na miiko ya
wasaidizi wa sheria.
MWISHO
Comments
Post a Comment