NA RAHIMA MOHAMED
TUME ya Utangazaji Zanzibar imesitisha leseni za utangazaji kwa muda wa miezi sita kwa vituo vitatu vya redio na kuvifungia vituo viwili vya televisheni kwa muda usiojulikana baada ya kukiuka masharti yaliyowekwa na tume hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Kikwajuni mjini Zanzibar, Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Suleiman Abdulla Salim, alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kugundua ukiukwaji wa leseni ya utangazaji kwa vituo hivyo.
Alieleza kuwa tume inafuatilia kwa ukaribu kabisa vituo vyote vya utangazaji na haitosita kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaotoa huduma ya utangazaji bila ya kuwa na leseni inayotambulika kisheria.
Akivitaja vituo vilivyofungiwa kwa muda wa miezi sita ni redia ya Bomba fm ambayo imekwenda kinyume na masharti yaliyowekwa kwa kurusha matangazo tofauti baina ya Zanzibar na Dar essaalam, Assalam FM pamoja na AM 24 FM ambazo zimebadili muundo wa hisa ya kampuni bila ya kuridhiwa na tume hiyo na kuacha kurusha matangazo vituo hivyo eneo la Unguja na Dar essalam.
(chanzo Zanzibar Leo)
Comments
Post a Comment