NA FATMA HAMAD, PEMBA
WAKILI
wa serikali Juma Mussa Juma, ameiomba Mahkama ya mkoa ‘B’ Wete, kulighairisha shauri
la ulawiti la kijana mwenye ulemavu wa akili, linalomkabili Nuhu Kombo Nuhu,
hadi hapo atakapofanyiwa uchunguuzi, baada ya wiki iliyopita kujifanya kiziwa
mahakamani hapo.
Awali mtuhumiwa huyo, aliwashangaaza watendaji wa mahkama
na wengine waliokuwepo mahkamani, hapo baada ya ghafla kuonekana kiziwi na
kushindwa kujibu maswali, hali iliyopelekea Mahakama kuagizwa kufanyiwa
uchunguuzi.
Hivyo Mwakili huyo
wa serikali, ameleza mahkamani hapo, kwamba tarehe iliyopita upande wao uliomba
mahakama kumpeleka Hospital mtuhumiwa
huyo, na mahkama kukubaliana na hilo.
‘’Nilitarajia leo Mheshimiwa hakimu, awepo mtaalamu
mwenye majibu ya mtuhumiwa, maana wiki iliyopita alikuwa hawezi kuzungumza
‘bubu’ na agizo lako likawa ni kufikishwa hospitali kwa uchunguuzi,’’alihoji
Wakili huyo.
Hata hivyo Wakili huyo, alioneshwa kushangaazwa kwake
hadi kufikia tarehe ya shauri hilo, agizo la mahkama kuwa, halijatekelezwa,
jambo ambalo aliomba kughairishwa hadi hapo atakapofanyiwa uchunguzi.
‘’Kwa vile agizo tulilolitoa la mtuhumiwa
huyu kupelekwa Hospitali kwa ajili
ya kupata uchunguzi
wa kitaalamu haukufanyika, tunaomba kuigharisha mpaka litakapotekelezwa,’’alidai.
Hakimu wa mahakama hiyo Ali Abdull-rahman Ali
hakupinga hoja hiyo
iliyotolewa na Mwendesha mashtaka
na kuamua kuighairisha hadi Mei 9, mwaka huu.
‘’Kwa hatua hiyo na ukumbusho huo, inabidi leo mtuhumiwa
arudi tena rumande, na hapa utawasili tena mahkamani Mei, 9 tukiamini itakuwa
umeshafanyiwa vipimo,’’alisema Hakim.
Awali ilidaiwa mahkamani hapo kuwa, mtuhumiwa huyo
alitenda kosa hilo Disema 12, mwaka jana, majira ya saa 1:30 asubuhi, Kijichame wilaya ya Micheweni
mkoa wa Kaskazi Pemba.
Ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 116 [1] cha sheria
nambari 6 ya mwaka 2018
sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment