NA HAJI NASSOR, PEMBA
AMA kweli, ukitaka kukificha kitu,
kitie kwenye maandishi.
Wengi
wamekuwa wakiyasema hayo, wakiwa na maana kuwa, ule utamaduni wa kusoma, sasa
umeondoka.
Kumbe kwenye
maandishi kama ya sheria, kanuni na sera zilizotungwa kwa ajili ya kundi
fulani, hukosa kutekelezwa kwa waliotungiwa, kwa kutosoma.
Aliwahi
kuwapa chagamoto wananchi Mkoani Pemba, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Mashibe Ali Bakari, alipotakiwa kujibu juu ya
sheria za Zanzibar kuwa lugha ya kigeni.
‘’Sheria za
Zanzibar tunatungiwa sisi wananchi ambao lugha yetu mama ni Kiswahili, lakini
zipo kwa lugha ya kugeni, hapa si mnataka kutufunga,’’alihoji Mohamed Abass
sheha mstafu wa Kinyasini.
Jaji Mshibe
akawambia kuwa, utamaduni wa kusoma hata kwa nyaraka zilizoandikwa kwa lugha ya
kiswahili sasa haupo, na ukitaka kukificha kitu kitie kwenye nyaraka.
SHERIA NA KANUNI YA UTUMISHI WA UMMA
2014
Sasa ni
miaka 19 imeshapita, tokea serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itunge Kanuni ya
Utumishi wa Umma ya mwaka 2014.
Kanuni hiyo yenye
vifungu kadhaa, lakini vipo vifungu muhimu na adhimu, hasa kwa watumishi wa
umma wanaume kuvijua, kwa kina.
Na hap
unaweza kujifunza jambo kuwa, mwajiri maisha haoneshi haki za mwajiriwa, kama
hakufanya juhudi za maksudi yeye mwenyewe kujisomea.
Inaweza wapo
wanaume, ambao ni watumishi wa umma, wamekuwa wake zao wakijfungua na pengine
kuhadithi ofisini kwake, lakini mwajiri akakaa kimnya.
LIKIZO LA MUME WA MKE ALIYEJIFUNGUA
Ili
kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria, sambamba na kujali umuhimu wa muume,
mara mke wake anapojifungua, sheria na kanuni ya Utumishi wa umma, haikukaa
kimya.
Maana imempa
haki ya likizo muume huyo, mara tu mke wake anapojifungua, hata kama mke sio
mtumishi wa umma.
Kwa mfano
kifungu cha 62 (1) kinaeleza kuwa, mtumishi wa umma ambae mke wake amejifungua,
ataruhusika kupewa likizo kwa muda wa siku tano (5) za kazi.
MASHARTI YA LIKIZO HILO KWA MUUME
Kanuni
ikafafanua kuwa, likizo hilo litachukuliwa ndani ya siku saba, baada ya mtoto
kuzaliwa, na halitoathiri lile likizo lake analolichuma kwa miezi 12.
Ingawa,
likizo hilo la siku tano za kazi kwa mtumishi mwanamme, litatolewa kila baada
ya miaka mitatu, ambapo hapa, kwa wale wasiokuwa na uzazi wa mpango hawatoangaliwa.
Maana, wapo
wanandoa kila mwaka, mke hujifungua au kila baada ya mwaka mmoja na nusu, hivyo
kinachozingatiwa sio uzazi tu, bali ni kila miaka mitatu.
Taarifa ya
kustahili likizo hilo kwa muume huyo mtumishi wa umma, iwasilishwe kwa mkuu
wake wa kazi, iambatanishwe na kitambulisho cha kuzaliwa cha mtoto.
JE MTUMISHI MWENYE MKE ZAIDI YA MMOJA?
Kanuni ya
Utumishi wa Umma, wala haikuwasahau wanaume wenye mke zaidi mmoja, hata kama
wake zake hao sio watumishi kama alivyo yeye.
Maana,
kifungu cha 62 (2) kimebainisha kuwa, mwenye mke zaidi ya mmoja, atastahiki
kupata likizo kwa kila mke wake atakapojifungua.
Hata hivyo,
endapo atakejifungua kila mwaka ni mke huyo huyo mmoja, atastahiki likizo hilo
kila baada ya miaka mitatu, na sio kila anapojifungua mke wake.
LIKIZO LA UZAZI KWA MKE MTUMISHI WA
UMMA
Kanuni hii
ya utumishi wa Umma ya mwaka 2014, imetoa haki na masharti kwa mzazi wa kike,
ambae nae amejifungua na hilo limeanishwa kifungu cha 61 (1).
‘’Mtumishi
wa umma anapojifungua, anastahiki likizo ya miezi mitatu (siku 90 za kazi) kwa
siku za kalenda,’’inaeleza sehemu ya Kanuni hiyo.
Likizo hiyo
ya uzazi ya miezi mitatu, itatolewa mara moja, kwa kila baada ya maika miwili
na miezi tisa, kwa mtumishi mwanamke.
Kama ilivyo
kwa mtumishi mwanamme ambae mke wake amejifungua, nae pia kwa mtumishi wa umma
mwanamke, likizo lake hilo, halitoathiri lile likizo lake la kawaida.
Kanuni
ikafafanua kuwa, pindi mtumishi huyo wa kike atajifungua kabla ya kutimiza muda
uliotajwa (miaka miwili na miezi tisa), atastahiki kupata mapunziko ya wiki
sita tu.
Lakuzingatia
hapa, taarifa za kujifungua kwake, inaweza kutolewa na yeye mwenyewe, au mtu
wake wa karibu mfano muume na ziende kwa Katibu mkuu au mkuu wa tasisi.
Kanuni
ikaenda mbali zaidi, na kueleza kuwa ikiwa mtumishi huyo, amejifungua mapacha,
kipindi cha likizo kitaongezwa mpaka kufikia siku 100 za kazi.
Kubwa zaidi,
ikiwa mimba hiyo imeharibika, au kufa kwa mtoto, mtumishi huyo atapewa likizo
ya wiki sita, tokea tarehe ya kujifungua au kuharibika kwa ujauzito huo.
Kanuni
ikisema kuwa, iwapo likizo lake ilikatishwa kwa sababu ya kufa kwa mtoto wake
mchanga, akipata ujauzito kabla ya kutimiza miaka miwili na miezi tisa, kuanzia
tarehe ya kujifungua au kuharibika mimba.
Basi Kanuni
hiyo ya Utumishi wa umma, imeweka wazi kuwa, mtumishi huyo atastahiki likizo ya
miezi mitatu kwa siku za kazi.
JE HAKI YA MTOTO KUNYONYA IKOJE KWA
MAMA MTUMISHI WA UMMA?
Mtumishi
huyo atapewa saa moja kila siku, kwa ajili ya kunyonyesha mtoto wake kwa
kipindi cha miaka miwili mfululizo.
Lakini
Kanuni imemtaka mtumishi huyo kuchagua, aidha kuitumia nafasi hiyo asubuhi
kabla ya kuja kazini au mchana saa moja, kabla ya muda wa kawaida ya kuondoka
kazini, yaani saa 9:30.
JE WATUMISHI WA UMMA WANAUME
WANAYAJUA HAYA?
Omar Hassan
Khalid wa wizara ya elimu, anasema mke wake ameshajifungua watoto saba akiwa
kazini, lakini hakumbuki hata siku moja, kupewa mapumziko hayo.
Mohamed Jafu
Said mstaafu wizara ya Mawasiliano, anasema licha ya kuwahi kuwa na wake wanne,
wakati akiwa mtumishi wa umma, ingawa haki hiyo hakuwahi kuipata.
‘’Inawezekana
mimi kama mtumishi wa kawaida hili jambo sikuwa nalijua, lakini je ofisa
utumishi wangu kama anajua, mbona sikuwahi kuaelezwa,’’anahoji.
Hassan Ali
Hassan ambe ni mfanyakazi wizara ya Afya anasema, aliwahi kupewa mwaka 2016,
baada ya kusikia kwenye redio, juu ya uwepo wa haki hiyo, na kuidai.
‘’Kuanzia
hapo, niliwahi kuomba tena mwaka 2020, na wakati huo wake zangu wawili
walijifungua kwa wakati mmoja, lakini niliambiwa nisubiri, na sikupewa
tena,’’anasema.
Ingaa Hidaya
Hassnuu Omar na Asha Mbarouk Omra watumishi wa wizara ya Elimu, wanasema haki
ya mapumziko baada ya kujifungua huipata,,
WIZARA YA KATIBA, SHERIA, UTUMSHI NA
UTAWALA BORA
Afisa sheria
wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Pemba Bakari Omar Ali, anasema
wamekuwa wakieleza maafisa utumishi, ili wawelimisha watumishi wao.
‘’Wakati
mwengine tasisi za umma wanatuita na kuwasomesha watumishi wao, juu ya sheria
na kanuni za utumishi, na hili suala la mapunziko ya siku tano za kazi
tunaligusa,’’anasema.
Anaona wapo
baadhi ya watumishi wanaume wamekuwa wakizitumia siku hizo, ingawa wengine
ijapokuwa wanajua lakini hawaziombi.
NINI KIFANYIKE?
Mtumishi
Issa Haji Khamis na mwenzake Khaija Hija Othman, wamependekezwa elimu zaidi
hasa ya kuifahamu kanuni ya utumishi wa umma, izidi kutolewa.
Afisa
Mdhamini wizara ya Katiba na sheria Pemba Halima Ali Khamis, amesema lazima
watumishi wajiongezea kwa kuzisoma sheria wanazozifanyia kazi.
Aliyekuwa
ofisa Utumishi wizara ya Habari Mohamed Juma, anasema ni jukumu la mtumishi,
kujua kanuni zinazogusa haki na wajibu wake.
Mwisho
Comments
Post a Comment