NA MWANDISHI WETU,
IKULU
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi,
amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023, serikali itaongeza mshahara kwa kutumia
utaratibu wa kuwapanga watumishi katika madaraja na vyeo kwa mujibu wa miundo
ya utumishi kwa kuzingatia elimu zao pamoja na uzoefu wa kazi.
Rais
Dk. Mwinyi aliyasema hayo huko katika viwanja vya Maisara kwenye hotuba yake
aliyoitoa ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi),
ambapo kwa Zanzibar sherehe hizi zimefanyika hivi jana, hii ni kufuatia kuwapa
wananchi wa Zanzibar muda wa matayarisho ya skukuu ya Idd el Fitr.
Rais
Dk. Mwinyi alisema kuwa ana imani kwamba ongezeko la mishahara litakalofanywa
litakuwa na mchango katika kuimarisha uwezo wa watumishi wa umma kujikimu
kimaisha pamoja na kuondoa kilio cha muda mrefu kwa watumishi wa umma ambapo
elimu na uzoefu wao wa kazi haukuwa ukijitokeza wazi wazi katika marekebisho ya
mshahara yaliyofanywa vipindi vilivyopita.
Hivyo,
Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga TZS
bilioni 12.7 kwa mwezi sawa na TZS bilioni 153 kwa mwaka kwa ajili ya
kugharamia utekelezaji wa zoezi hilo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Alisema
kuwa kutokana na utaratibu huo mshahara wa kima cha chini kwa mtumishi
aliyeajiriwa mwaka 2019 utapanda kutoka shilingi 300,000 hadi kufikia shilingi
347,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.6.
Aliongeza
kuwa vile vile kwa mtumishi wa elimu ya ngazi ya cheti wa masomo ya sanaa
aliyeajiriwa katika mwaka huo huo mshahara wake utapanda kutoka TZS 321,000
hadi kufikia shilingi 382,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.
Kwa
maana hiyo, Rais Dk. Miwnyi alisema kwamba kila mfanyakazi atapata nyongeza ya
mshahara kutegemea na elimu yake pamoja na muda aliofanya kazi ambapo mfano huo
ni kwa mfanyakazi mpya hivyo hata ambae hana cheti lakini amefanya kazi muda
mrefu mshahara wake utaongezeka kwa kadri ya muda aliofanyakazi.
Vile
vile, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa katika kuhakikisha kwamba wafanyakazi
wanaendelea kuwa na kipato hata wanapopata changamoto ya kupoteza ajira au
kupata ajali wakiwa kazini, serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar
(ZSSF) imeanzisha Fao la Upotevu wa Ajira na Fao la Kuumia Kazini.
Comments
Post a Comment