NA JAFFAR ABDALLA, PEMBA
MASHEHA Kisiwani Pemba, wamehimizwa
kuendeleza juhudi za kuwahamasisha wananchi, kujitokeza kuchanja chanjo ya kujikinga
dhidi ya ugonjwa wa Uviko19, ili kujiepusha na maambukizi ya maradhi hayo.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkuu wa Kitengo cha elimu ya Afya Zanzibar, Bakar Hamad Magarawa, wakati
akifungua mafunzo ya siku moja, yaliyowashirikisha masheha na watendaji wa Wizara
ya Afya, mkutano uliofanyika Samail Chahe chake Kisiwani Pemba.
Alisema, bado
zipo baadhi ya shehia idadi ya wananchi wanaojitokeza kupata chanjo
hiyo ni ndogo, hivyo ipo haja kwa masheha, kuwaelimisha wananchi wao
kuchukua tahadhari kwa kupata chanjo hiyo.
Aidha Bakari amewatoa
hofu wananchi kuwa, chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote, ambayo
yananaweza kuathiri afya zao, wanapopatiwa chanjo hiyo na kuacha dhana yakuwa
chanjo hizo zinamadhara.
‘’Nawasihi masheha
muendelee kuhamasisha wananchi wenu kuchanja chanjo hii, kwani kuna baadhi ya
shehia idadi ya walio chanja iko chini, kulingana na takwimu zinavyo onesha,”alisema
Magalawa.
Kwa upande wao baadhi
ya wananchi, waliitaka wizara ya Afya kuhakikisha, wanawamalizia dozi kwa wale
wananchi ambao wameshachanja, chanjo ya kwanza.
Walisema wananchi
walio wengi walipata chanjo mmoja, ambapo walitakiwa kupata dozi ya pili ya
chanjo hiyo, ili kuwa na uhakika wa kujikinga na ugonjwa wa uviko 19.
Nao Baadhi ya Masheha
katika mkutano huo wameiyomba Wizara ya Afya, kuwapatia vitambulisho kwa wale
wananchi ambao walishamaliza dozi ya chanjo hiyo.
Hata hivyo Masheha hao
walisema wanaotoa chanjo wanapaswa kuzingatia suala la wakati, kwani huwa
wanakusanya watu kwaajili ya zoezi hilo, lakini badae watu hao huondoka
kutokana na watoa huduma hiyo kuchelewa kufika.
Mwisho.
Comments
Post a Comment