Skip to main content

Posts

MAENEO 148 YAATHIRIWA NA MABADILIKO TABIANCHI

  TAMWA ZNZ, Kitengo cha Habari SEREKALI ya Mapindizi ya Zanzibar imesema inaendelea na juhudi mbali mbali za kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha nchi inakua salama. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Harusi Said Suleiman alisema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa mazingira katika mkutano wa mabadiliko ya tabianchi katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdul Wakili Kikwajuni Zanzibar. Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi iliyoathirika na mabadiliko hayo katika nyanja mbali mbali ikiwemo za kiuchumi na kijamii. “Sehemu kubwa zilizoathirika katika maeneo hayo ni pamoja na kilimo, uvuvi, utalii na makaazi ya wananchi hali ambayo kwa namna moja au nyengine imesababisha kurudisha nyuma juhudi za wananchi na taifa kwa ujumla katika kukuza uchimi wa nchi,”alisema. Alisema mwaka 2012, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais ilifanya utafiti ulionyesha kuwa hali ya hewa ya Zanzibar imeathirika kutokana na mabadiliko ya Tabianchi jambo lilosababisha ...

WANANCHI VISIWA VIDOGO PEMBA, WAZIMA VIBATALI BAADA YA MIAKA 58, WAKIFIWA NA UMEME WA SOLA

NA NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NI ya miaka 58 imepita sasa, kila mmoja hawezi kuamini, mafanikio makubwa kwa wananchi wa visiwa vidogo vigodo vilivyoko wilaya ya Wete Pemba yaliofikiwa. Mwaka 2022, ndoto za wananchi wa visiwa vya Njau na Kokota, zimetimia baada ya Shirika la Umeme Zanzibar ‘ZECO’, kuzima kibatali na kuwasha umeme wa sola kwa wananchi wa visiwa hivyo. WANANCHI WENYEWE Ali Oma Khami anayeishi Kisiwa cha Njau, anasema mabadiliko makubwa wanaendelea kutokea, ikiwemo kukua kwa biashara kufuatia kuwepo kwa nishati ya umeme. ''Umeme ni moja ya nishati inachorahisisha maendeleo ya sehemu yoyote ile, ni wazi na sisi tumeanza kunufaika na mabadiliko makubwa ya Serikali kutupatia miundombinu ya umeme,” anasema. Chumu Omar Kai, kwa sasa wanapata kwa matumizi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuweka chaji, ambapo zamani walilazimika kwenda nje ya kisiwa masafa ya kilomita 30 hadi mjini Wete. Nae Nyezume Abdalla Ali anawataka wenzake kuilinda miundombinu ya hio, ili iwe...

PICHA ZA KAMBI YA MSAADA WA KISHERIA MICHEWENI

 

WANANCHI KASKAZINI PEMBA, ZITUMIENI SIKU 3 ZA KAMBI YA KISHERIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa mkoa wa kaskazini Pemba, wametakiwa kuzitumia siku tatu za kambi ya kutoa masaada wa kisheria, ili kufikisha malalamiko yao ya kisheria, na kupatiwa ufumbuzi papo hapo. Hayo yameelezwa leo Oktoba 17, 2024 na Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, katika hutuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Omar Bakari, kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, iliyozinduliwa uwanja wa Majengo Micheweni Pemba. Alisema, siku tatu hizo watakuwepo wanasheria, Jeshi la Polisi, wasaidizi wa sheria, mahakim na mawakili, ili kusikiliza changamoto za kisheria na kuzitolea ufumbuzi papo hapo. Alieleza kuwa, kuwapata wanasheria wakati mwingine huwa ni vigumu, ingawa kufuatia uzinduzi wa kampeni hiyo, wanapatikana papo hapo bila ya malipo. ‘’Niwatake wananchi wa mkoa wa kaskazini Pemba na hasa wa wilaya ya Micheweni, kufika hapa Micheweni majengo, ili kupata elimu na msaada wa kisheria tena ...

MKUTANO WA KWANZA MABADILIKO TABIANCHI-TAMWA ZANZIBAR YASEMA NENO

  TAMWA ZNZ , Kitengo cha habari Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Taasisi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (ZACCA) na Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, imeandaa mkutano wa kwanza wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika   Zanzibar, oktoba 20 hadi 22 katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TAMWA Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, Mwenyekiti wa kamati ya Jukwaa la mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.(ZANCCC) Mahfudh Shaban Haji, amesema lengo la mkutano huo ni kujenga uwezo, uelewa na hamasa kwa asasi za kiraia, wanajamii na Idara za Serikali kufahamu dhana nzima ya mabadilikoya tabianchi na uhimili wake.   Aidha Shaaban ameeleza kuwa mkutano huo utazungumzia mada mbali mbali za kimataifa na kitaifa ikiwemo mkakati wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2014, sera, uwajibikaji na dira ya maendeleo 2050 ambayo ...

ANNA ATAJA FAIDA LUKUKI ZA ELIMU KWA MTOTO WA KIKE

  NAIBU Waziri wa Maendeleo wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Anna Athanas Paul amesema iwapo mtoto wa kike atasoma kwa bidii ataweza kuviepuka viashiria vya unyanyasaji ambavyo ndio vikwazo vikubwa vinavyowafanya kutokufikia malengo yao. Ameeleza jayo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike huko katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kampas ya Maruhubi Unguja. Amesema   watoto wa kike wakisoma kwa bidii itasaidia kutimiza malengo yao ya baadae hali ambayo itasaidia kujiepisha na vitendo viovu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia. “Iwapo mtoto wa kike atasoma kwa bidii ataweza kuviepuka viashiria vya unyanyasaji ambavyo ndio vikwazo vikubwa vinavyowafanya kutokufikia malengo yao ” Amesema Waziri huyo. Naibu Waziri huyo amefahamisha kuwa kwa mujibu takwimu kutoka Afisi ya Mtakwimu Mkuu mwaka 2023 matukio 1954 ya ukatili na udhalilishaji yaliripotiwa kati ya matukio hayo wasichana walikuwa 1263 sawa na aslimia 77.1 hiyo inaonesha bado watoto wa k...

VOSHOKA WA UBAKAJI PEMBA KIKAANGONI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAMTANDAO wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji kisiwani Pemba, wamelaani kitendo cha watu wazima, kukimbilia kwa watoto wachanga, kuwadhalilishaji, kwani husababisha athari zaidi kwao. Walisema, miongoni mwa athari hizo ni kuwasababisha kukosa kizazi, kuwatishia masomo, athari za kisaikolojia jambo ambalo linatajwa kuzima ndoto zao za maisha. Wakizungumza kwenye kikao cha kuwasilisha ripoti za kazi zao, kilichofanyika ofisi ya TAMWA Pemba, walisema, sasa vitendo hivyo wadhalilishaji wameelekeza nguvu zaidi kwa watoto wadogo. Walieleza kuwa, zipo kesi kadhaa zinazowahusu watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi 10, wakifanyiwa udhalilishaji na wanaume wenye umri kuanzia miaka 40 hadi 50. Mwanamtandao kutoka wilaya ya Mkoani Haji Shoka Khamis, alisema sasa wabakaji wameelekeza nguvu kwa watoto wadogo, jambo linalokuwa gumu wanapofika mahakamani. ‘’Wadhalilishaji sasa wamehamia kwa watoto wadogo, na kisha huwapa lugha za vitisho...

TAMWA- ZANZIBAR YAKOSA USINGIZI HADI SHERIA MPYA YA HABARI IPATIKANE

      NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ‘’BILA ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi’’. ‘’Tena pia mtu huyo ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati, na raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio ya nchini na duniani kote, ambayo ni muhimi kwa maisha yake’’. Ndivyo Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inavyoelekeza kifungu cha 18, juu ya upatikanaji na utoaji wa habari kwa raia, tena bila ya kujali mipaka ya nchi. Mwanasheria wa kujitegemea Khalfan Amour Mohamed, anasema suala la kupata habari, au kutoa ni haki ya kikatiba, ambayo inatofautiana na haki nyingine. ‘’Ukitaka kuzigawa haki hizi, basi zipo haki za kikatiba na haki nyingine zilizotengenezewa sheria yake mbali mbali, mfano haki ya elimu,’’anafafanua. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajali wananchi wake, haikuishia tu ndani ya Kati...