TAMWA ZNZ, Kitengo cha Habari
SEREKALI ya Mapindizi ya Zanzibar imesema inaendelea na
juhudi mbali mbali za kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi ili
kuhakikisha nchi inakua salama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Harusi Said
Suleiman alisema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa mazingira katika
mkutano wa mabadiliko ya tabianchi katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdul Wakili
Kikwajuni Zanzibar.
Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi iliyoathirika na
mabadiliko hayo katika nyanja mbali mbali ikiwemo za kiuchumi na kijamii.
“Sehemu kubwa zilizoathirika katika maeneo hayo ni pamoja na
kilimo, uvuvi, utalii na makaazi ya wananchi hali ambayo kwa namna moja au
nyengine imesababisha kurudisha nyuma juhudi za wananchi na taifa kwa ujumla
katika kukuza uchimi wa nchi,”alisema.
Alisema mwaka 2012, Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
ilifanya utafiti ulionyesha kuwa hali ya hewa ya Zanzibar imeathirika kutokana
na mabadiliko ya Tabianchi jambo lilosababisha kupanda kwa joto na mvua kubwa
zinazosababisha majanga.
Aidha alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo serikali
itahakikisha inapambana katika kupunguza na kuzuia atahari hizo ili kuona nchi
haiathiriwi na mabadiliko hayo kama vile kujenga matuta katika sehemu
zilizoathirika kama vile Kilimani kwa
Unguja na Kojani,Mzingani,na Sipwese kwa Pemba
“Miaka 30 iliyopita wastani wa kiwango cha juu cha joto
kimeanda na kuanza kufikia nyuzi 39 na kusababisha majanga, ambapo Zanzibar
maeneo 148 yameathirika, 125 Pemba na 23 Unguja,” Waziri Harusi.
Hivyo aliwasisitiza wadau wa mazingira kushirikiana na
serikali katika kutoa elimu kwa wananchi ili kuona athari hizo zinaendelea
kulindwa ili kuweka ustawi mzuri wa taifa.
Mkururugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Mazingira Zanzibar
(ZACCA) Mahafudhi Shaaban Haji alisema lengo la mkutano huo ni kuiunga mkono
serikati katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, hivyo jumuiya hiyo
itahakikisha Zanzibar inakua ya kijani katika kuleta maendeleo ya kimazingira
nchini.
“Serikali kuangalia uwezekano
wa kufanya mkutano huo kila mwaka ili
kuongeza uwelewa kwa jamii na taifa kwa ujumla katika kupunguza na kudhibiti
athari za kimazingira ambapo Zanzibar kuna uharibifu mkubwa wa kimazingira,”
Mahfoudh.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo Mkururugenzi Mkuu
Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Sheha Mjaja Juma, alisema miongoni mwa athari
za mabadiliko ya tabianchi pamoja na utupaji wa taka hali ambayo inachangia
uharibifu mkubwa wa mazingira katika sehemu mbali mbali ikiwemo za kiuchumi,
kijamii na maeneo mengine.
Hivyo alizitaka jamii na wadau wa mazingira kuendelea
kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na kuacha kufanya uharibifu wa mazingira
katika makaazi ya watu na maeneo ya kiuchumi ikiwemo bahari na hifadhi za
misitu.
Afisa mradi wa Mabadilko ya Tabianchi (ZANZIADOPT) kutoka
Chama cha Waandishi wa habari Wanawawake
Tanzania, TAMWA ZNZ Nayrat Abulla Ali alisema mabadiliko ya tabianchi ni jambo
linalomuhusu kila mmoja, hivyo ameiasa jamii kushirikiana kwa pamoja kuyatunza
mazingira.
Washiriki wa mkutano huo walisema athari za mabadiliko ya
tabianchi zinawaathiri zaidi kina mama na watoto hasa wa vijijini kwa kukosa
hewa safi,lishe bora pamoja na ukosefu wa nishati isiyo salama ya kupikia.
Walisema athari nyengine pia zinawaathiri zaidi wavuvi na
wakulima wa mwani kwa kupoteza ajira zao na kushuka kipato chao siku hadi siku.
Mkutano huo wa siku tatu ulioandaliwa na Taasisi ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, (ZACCA) kwa kushirikiana na Ofisi ya
Makamo wa kwanza wa Rais Zanzibar, umewashirikisha wadau wa mazingira wakiwemo
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA ZNZ, na kuhudhuriwa na
washiriki 250 wa ndani na nje ya Zanzibar ambapo mada 15 zinazohusiana na
masuala ya uhifadhi, athari na mikakati ya kitaifa na kimataifa zitawasilishwa.
MWISHO
Comments
Post a Comment