NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama wao kwanza ,wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa vayama vingi nchini.
Akifungua
mafunzo kwa waandishi wa habari, huko katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani
Chake chake Pemba, mkufunzi wa mafunzo hayo Mwandishi Maryam Nassor ambae amejengewa uwezo na Umoja wa vilabu vya waandishi wa Habari
Tanzania (UTPC) . na yeye kutakiwa kuipeleka elimu hiyo kwa waandishi wengine
Mkufunzi huyo, amesema kuwa, ulinzi na usalama wa mwandishi wa
Habari unaanza na mwandishi mwenyeye , hivyo kuwataka waandishi hao kuwa makini
wanapotimiza majukumu yao.
“
Waandishi wa Habari lazima Kujifunza kusoma mazingira kwa haraka (kama
vile maandamano au machafuko) ili kubaki salama wakati munatimiza majukumu
yenu”
Amesema kuwa, tafiti zinaonesha katika kipindi hichi waandishi wengi huingia matatizoni
na wengine kupoteza maisha.
Aidha
ameongeza kuwa, ni vyema waandishi wa
Habari kutoa taarifa kwa watu wao wa
karibu , wanapokwenda kwenye kazi
hatarishi, ili kuepuka hatari zinazoweza kujitokeza endapo watapatwa na
hatari wakiwa pekee yao
“
Ulinzi na Usalama wa mwandishi wa Habari huanza na mwandishi mwenyewe hivyo ni lazima kutambua mazingira tunayofanyia
kazi na watu tunaofanya nao kazi, ili kujihakikishia Ulinzi na Usalama wakati
tunatimiza majukumu yetu” amesema .
Aidha amewataka waandishi wa Habari Kujua namna ya kushughulikia msongo wa mawazo
baada ya kazi (trauma) na kupata mud awa kupumzika.
Mkufunzi huyo,
amewaasa Waandishi wa habari
kupata elimu ya saikolojia kwa sababu taaluma yao
inawahusisha moja kwa moja na mazingira yenye changamoto nyingi za kiakili,
kihisia, na kijamii.
Baadhi ya waandishi
wa Habari waliohudhuria mafuzo hayo, Fatma Hamad mwandishi wa blog ya Pemba ya
leo na Is’haka Mohamed wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha usalama
wao sehemu za kazi.
Kwa
upande wake mshiriki wa mafunzo hayo Salum Hamad, amesema mafunzo hayo
yamemuongezea uwelewa mkubwa wa kujua mipaka yake kama mwandishi katika kutekeleza
majukumu yake
Mafunzo hayo, ya ulinzi na usalama wa kimwili, kimtandao na
kisaikolojia yametolewa kwa baadhi ya waandishi wa Habari wa klabu ya waandishi
wa Habari ya Pemba (PPC).
Comments
Post a Comment