NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema ajenda ya Wanawake,
Amani na Usalama ni matokeo ya Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Na. 1325 (2000) ambalo linazitaka nchi wanachama kuandaa na Kutekeleza mipango
ya Kitaifa kwa ajili ya kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamikifu katika
nyanja zote za amani na Usalama.
Mhe. Riziki ameyasema
hayo leo katika Uzinduzi wa Mpango kazi
wa Kitaifa wa Kutekeleza ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 2025-2029 katika
ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania, Kunduchi Jijini Dar es
salaam, wakati akitoa salamu za Zanzibar juu ya ushiriki wake katika uandaaji
wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Kutekeleza ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama
2025-2029.
Amesema Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Kupitia Sera na Mipango mbali mbali, imetekeleza
ajenda hiyo kwa vitendo katika nyanja mbali mbali ikiwemo ushiriki wa wanawake
katika uongozi na kuongoza katika nafasi muhimu Serikalini.
“Sheria mbali mbali
ikiwemo Sheria ya Mtoto namba (6) ya mwaka (2011), sheria ya kumlinda Mwari na Mtoto
wa mzazi mmoja ya mwaka (2004) na Sera ya Jinsia ya mwaka (2016) pamoja na
uzingatiaji wa bajeti kwa Wizara zote 18 za Zanzibar ili kustawisha usawa wa
kijinsia pamoja na kutunza maslahi bora ya Wanawake na Watoto SMZ Imetekeleza
kwa vitendo” Amesema Pembe.
Pia amesema Wizara hiyo imetengemea kuzindua Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji
wa Kijinsia (NPQ-VAWC II 2025-2030) dhidi ya Wanawake na Watoto.
Ameeleza katika maandalizi ya Mpango kazi huo, Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeshiriki kikamilifu, hivyo
amewaomba wadau wote Kutekeleza kwa vitendo ajenda za mpango kazi huo badala ya
kubaki kuwa katika makaratasi.
Aidha Mhe Riziki ameshukuru
ushirikiano unaondelea kati ya Wizara anayoisimamia na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Makundi Maalumu ya Tanzanzia Bara pamoja na kuomba mashirikiano hayo kuzidi kuendelea kwa lengo
la kuleta Maendeleo katika Taifa.
Uzinduzi wa Mpango kazi
wa Kitaifa wa Kutekeleza ajenda ya Wanawake Amani na Usalama 2025-2029,
umezinduliwa na Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Nishati, ambapo viongozi mbali mbali wa Kitaifa pamoja na viongozi wa Mashirika
mbali mbali ya Ndani na nje ya nchi wamehudhuria.
Mwisho
Comments
Post a Comment