MFUMO mpya wa kidigitali utasaida kuhifadhi fedha za vikundi vya kuweka na
kukopa vya watu wenye ulemavu kwa usalama zaidi, na kuondokana na kuhifadhi
kwenye masanduku kama ilivyo sasa.
Ameyasema hayo Meneja program wa shirikisho la jumuiya za watu wenye ulemavu (SHIJUWAZA)
Sophia Azidihery Leghela, alipokuwa akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vikundi
vya watu wenye ulemavu na wawakilishi wao, ukumbi wa Samail Chake chake Pemba.
Alisema mfumo mpya wa digital utasaidia watu wenye ulemavu
kuhifadhi pesa zao kiusalama zaidi wa kuweka na kukopa, ili kuondosha hofu ya
kupotea kwa fedha zao.
Alieleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kujifunza kuhusiana
na mfumo wa kuhifadhi, kuweka na kukopa, kwenye vikundi vya kijaluba kwa njia
ya digitali kwa watu wenye ulemavu.
"Niwatake mutumie mfumo huu wa kidigitali wa kuweka na kukopa kwa
kuhifadhi fedha zenu, ili kuondoka na kutia ndani ya masanduku,"
alifafanua.
katia hatua nyingine, alieleza kuwa lengo la kuingia kwenye mfumo huo, ni
kuhakikisha usalama wa fedha za watu wenye ulemavu wanaimarishwa hali ya
kiuchumi na kiustawi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la jumuiya za watu wenye
ulemavu Ali Machano, alisema lengo la kuundwa vikundi hivyo, asili yake ni watu
wenye ulemavu pamoja na mjumuisho wao.
Alifafanuwa kuwa asilimia 60 ya vikundi hivyo ni watu wenye ulemavu na asilimia
40 ni walezi, wazazi na watoa huduma kwa watu wenye ulemavu.
Alieleza kuwa ndani ya kikundi cha watu 30, ni lazima watu wenye ulemavu
wawe 18 na wasimamizi wao wawe 12.
"Lengo la vikundi hivi, tumewalenga watu wenye ulemavu kwa asilimia kubwa, hasa kutoka na ulemvu wa aina tofauti ndio tukapendekeza wasaidiwe na wasaidizi wao wa karibu," alifafanua.
Mjumbe wa shirikisho la Jumuiya ya watu wenye ulemavu Aziza Mussa Alawi,
alisema watu wenye ulemavu ni watu muhimu, na wamekuwa wakifanya vizuri
kutokana vikundi vivyoundwa.
Alfafanuwa kuwa, jamii ielewe kuwaunga mkono watu wenye ulemavu, ili kuondokana
na dhana mbaya itayowaharibia maisha yao.
"Ni vizuri kumsaidia mtu mwenye ulemavu kwa kuwaunga mkono na kumsaidia
katika miradi kadhaa ya maendelo,"
alifafanua.
Aliongezea kuwa mtu mwenye ulemavu anapaswa kuwekwa mbele katika kumuwezesha
masuala ya ajira, taaluma, uwezeshaji na afya.
Mradi huo unaendeshwa kwa pamoja na Shijuwaza, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, Jumuiaya ya wasioona ZANAB, kwa unafadhiliwa Norway umekuja baada ya mafanikio ya majaribio, kwenye kijaluba kwa miaka miwili na sasa umeongezwa hadi mitano ijayo.
MWISHO
Comments
Post a Comment