NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SHIRIKA la Ndege la Tanzania 'ATCL' limerejesha tena huduma zake za usafiri kisiwani Pemba, baada ya miaka 30.
Shirika hilo limekuja kivyengine kisiwani Pemba, maana limeanza na punguzo maalum la nauli, na ili kulijua punguzo hilo, unatakiwa kuzitembeleza ofisi zao zilizopo mjini Chake chake mkabala na Ofisi ya CCM.
Kwa taarifa zaidi soma hapo chini......
WAZIRI wa
Uchukuzi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Prf: Makame Mbarawa Mnyaa, amesema kuanza
kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania ‘ATCL’ kisiwani Pemba, ni eneo
jingine la kukifungua kisiwa cha Pemba, kiuchumi, kama ilivyokuwa ahadi ya
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema ATCL, sasa litawarahisihia zaidi wananchi wa Pemba, wakiwemo wafanyabiashara, kufika safari zao kwa wakati, ikiwa ni hatua muhimu ya kufikia ndoto zao za kiuchumi.
Alieleza kuwa, ndege hiyo itafanya safari zake mara tatu kwa wiki ndani ya siku za
Jumanne, Ijumaa na Jumapili na zitachukuwa abiria kati ya 76 na nyingine hadi 50.
"Niwatake wananchi wa Pemba, muitumie ndege hii kutokana ubora na
umathubuti wake na uhakika wa safari zake za kuanzia, hapa Pemba, Unguja, Dar-es
Saalan na mikoa mingine kadhaa ya Tanzania," alieleza.
Alifafanua kuwa, ndege hiyo imekuja baada ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha
Mapinduzi kwa viongozi wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari.
Aidha, Waziri
huyo aliipongeza hatua ya serikali ya kuona sasa inatanua mbawa zake kwa shirika
hilo la ndege, jambo linalokuza pato la nchi.
kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege Tanzania Peter Ulanga, alisema kupitia shirika hilo, mwezi Machi mwaka huu, lilizindua safari katika mikoa ya Mtwara na Iringa na kupitia mji Kinshasha ya Kidemokrasia ya Congo.
Alisema safari hizo ziliweza kupokekewa vizuri sokoni humo, na zaidi ya abiria
320 hutumia Air Tanzania, katika safari zao na wastani wa abiria 370 wakitokea
upande wa mkoa wa Mtwara na 500 kwa DR. Congo kila wiki katika vituo hivyo.
Alifafanuwa kuwa, kupitia shirika hilo, wanajivunia mno, kuwepo kwa ndege mpya
15, ambazo zinafanya kazi, pamoja na ile moja maalum kwa ajili ya mizigo.
"Niwajulishe kuwa, katika ndege hizo, saba zimenunuliwa na serikali ya
Jamuhuri ya awanu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia, jambo linalotupa ari
ya kufanyakazi kwa bidii na hamasa,"alieleza.
Mkuu wa wilaya ya Chake chake Mgeni Khatib Yahya alisema, Pemba ni kisiwa cha kikubwa chenye historia ya kitalii kinachounganisha kivutio cha kiuchumi kama vile fukwe.
Alisema imeweza kufunguka kiuchumi na kuunganishwa sehemu mbali mbali, kutoka nchi na ndani ya Zanzibar, jambalo ambalo kuja kwa ndege hiyo, ni
hatua nyingine.
"Tunamshukuru sana Rais wa Zanzibari kwa kukifungua Pemba kiuchumi tena
kwa vitendo, kutokana na usafiri huu, utaweza kurahisisha na uchumi kukua
kwa kasi," alifafanua.
Aliongeza kuwa, kuwepo kwa ndege hiyo na kuanza safari zake kisiwani humo, italeta maendeleo makubwa kwa wananchi na kurahisisha safari zao mbali mbali.
Ilifahamika kuwa, kampuni hiyo, imefanikiwa kuongeza miinuko, kutoka 20 kwa
siku hadi 140 kwa wiki, katika maeno mbali ya ndani ya nje na kuweza kuiunganisha
Tanzania na dunia.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni
ATCL linamiliki ndege 16, ikiwemo aina ya Bombardier Dash 8 Q400, Bombardier
CS300 (Airbus A220-300) na Boeing 787 Dreamliner.
Aidha inafahamika kua, Julai 2019, ATCL lilizindua safari baina ya Tanzania kwenda Mumbai- India.
Hata hivyo, mwezi Machi 2021, BBC
Swahili, iliripoti kuwa, ACTL lilipata hasara ya shilingi bilioni 60, kwa
miaka mitano iliyopita, ambapo ni kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
mkuu wa hesabu za serikali ‘CAG’ ya mwaka 2019/20120.
MWISHO
Comments
Post a Comment